Ushauri kuhusu BILLION 19.5 za gawio la serikali toka CRDB

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,514
Habari zilizopo ni kwamba serikali imelipwa jumla ya Tsh Bilioni 19.5 kamili kama gawio/rejesho lake toka bank ya CRDB... Pesa hiyo serikali iliipa bank hiyo mwaka 1994 ili kuinisuru isifilisike
Naomba serikali isiitume pesa hiyo kwenye mambo makubwa tafadhali, kama ushauri wangu ukizingatiwa natoa rai sehemu ya pesa hiyo itumike kuboresha mochwari zetu za hospitali za SERIKALI sehemu mbalimbali nchini
Hizo mochwari nyingi zinahitaji kupanuliwa kwakuwa ni ndogo na hazitoshi..... Mochwari nyingine nyingi tu majokofu yake yameharibika ama hayafanyi kazi vizuri na kusababisha kero kubwa kwa wahudumu wake pamoja na ndugu wa marehemu
Hili si la SIASA bali ni letu site... Jamii isiyo na kipato kikubwa inateseka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fedha hizo zirudishwe bank kwa mfuko maalum kukopesha wajasiliamali na wakulima kuboresha uchumi wa taifa.
 
Back
Top Bottom