Majigo
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 5,519
- 1,825
Wakuu kwa mtu yeyote mwenye ujuzi kuhusu biashara hii hasa samaki wa maji baridi huko Dodoma.
Soko lake vipi lina upinzani mkubwa?
Mimi niko Mbeya. Nawasilisha kwa salamu na shukrani kwenu!
WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUJUA KUHUSU BIASHARA HII
Salamu wana JF.
Nimepata mchongo, kuna mtu toka nchi za northern Africa anataka nifanye nae biashara ya samaki. Yaani namtumia samaki toka huku TZ kwa ndege.
Swali langu ni je, kama unataka ku-export samaki ni vibali gani vinatakiwa? Je unaweza ku-export kama individual bila kuwa na kampuni hasa kwa kuanzia?
Kama kuna mzoefu naomba anisaidie.
Pia kama kuna mtu anazo samaki toka lake victoria tunaweza kuongea jinsi ya kufanya hii biashara.
Asanteni sana
Wakuu,
Kwa wale wataalam wa biashara ya samaki wabichi naomba mwongozo wenu wa namna ya kuendesha hiyo biashara.
Naombeni maoni na ushauri pia.
- Ni kiasi gani cha mtaji kinahitajika?
- Ni wapi ambapo soko ni zuri kwa biashara hizi?
- Kuna tofauti yoyote ya biashara hizo za samaki wabichi kutegemeaa na maeneo ya bishara?
- Mambo gani ya muhimu nahitajika kuzingatia?
Asanteni.
Team Watafutaji
Kama title inavyosema hapo juu, naomba kufahamu hii biashara kwa undani kidogo, yaani recently tuliambiwa kuwa kwa kipindi hiki cha miaka mitano samaki wetu wameongezeka urefu/ukubwa.
Sasa basi nikawa interested kufahamu kama mtu anaweza kununua samaki (Sato/Sangara) kutoka kwa Wavuvi in bulk na kuziuza kwa makampuni ambayo tumeambiwa wanasafirisha kwenda nje ya nchi moja kwa moja.
Au kuanza kuvua na kuuza moja kwa moja kwa haya makampuni badala ya kununua kama middleman.
Moja, je ni changamoto gani kubwa zipo kwenye hii sekta?
Pili, upatikanaji wa vibali ukoje!?
Tatu, je hivi viwanda vinanunua hao samaki kwa mfumo gani? Cash on delivery au on credit?
Nne, je mtu anaweza kuingia mkataba na hivi viwanda ili kuwa-supply mzigo?
Tano, ni fursa gani (fursa ndani ya fursa) zinaweza kupatikana kwenye hii biashara?
Sita, modality yao (kama ipo), ipoje? Je wanaweza kukudhamini vifaa ili mzigo uwapelekee wao na kukatana kidogo kidogo?
Saba, ni viwanda (kwa majina) vipo kati ya Mwanza, Bukoba na Musoma au around maeneo hayo ambao wanaweza kupokea mzigo?
Nane, je upatikanaji wa samaki una msimu? High season na low seasons?
Maswali yangu hayajakaa kwa mtiririko maalum hivyo tusaidiane tu kadiri tutakavyoona inafaa.
Kwa hili tutaweza kusaidiana na kuwasaidia vijana wetu/wenzetu pia
MICHANGO YA WADAU KUHUSU BIASHARA YA SAMAKI
MAMBO 3 UNAYOHITAJI KUFAHAMU KATIKA BIASHARA
Mkuu katika uanzishaji wa biashara kuna vitu vi3 vya msingi unatakiwa kuvijua au kuwa navyo
1. Capital
2. Market
3. Knowledge
Capital: Ya kuanzisha Bucha/Samaki unahitaji kuwa na Fremu ya kisasa yenye A/C,Mashine ya Kukata Nyama(Unaweza kununua sido) hapo Vifaa A/C+Mashine+Fremu(kodi 6months) unahitaji si chini ya 1.2m,Mtaji wa kilo 500 nyama sh 2.3m,mtaji wa samaki kilo 100,Sh 500,000/=,Deepfreezer kubwa 400,000/=,Stand za vyuma pamoja na Hooks 100,000/=,Grand Total~4.5m
Market: Inabidi butcher lako litageti soko la mama ntilie/wauza chips na makazi ya watu,mama ntilie ndio wanunuaji wakubwa wa nyama kwani wanapika Supu na pili mboga kwa wateja,wauza chips stake wanatengenezea mshikaki!
Knowledge: Mkuu hapa inabidi uwe unaamka saa 3 kwenda kufata nyama au uwe unaagiza kwenye vigari vile special kwa ajili ya kubebea nyama,saa kumi na 1 alfajiri uwe upo buchani unaanza kuuza,uhifadhi wa samaki na nyama inayolala unabidi uhuzingatie,Nyama kilo moja ni kuanzia 6000 hadi 7000 na samaki sato kilo 8000 hadi 9000 wakati sangala 7000 hadi 8000.
Kazi ni kwako mkuu.
NI WAZO ZURI, SONGA MBELENi wazo zuri mkuu songa mbele. Ila jitahidi ujue ni samaki ya aina gani utakuwa unapeleka kutoka Mwanza kwa sababu samaki aina ya sangara ni bei kubwa sana mwanza kwa sababu ya kuwepo kwa viwanda, so wasi wasi wangu usije ukawanunua then ukienda kuuza wananchi wako wakaona ni bei kubwa. Jaribu kuangalia samaki aina ya sato na wengine ila sangala fikiria mala mbili kabla ya kuuza.
Kama utakuwa unanunua Mwanza tafuta ofisi weke frige na kuwa unakusanyia mzigo hapo hata kwa muda mfupi. Jambo lingine jitahidi kujiridhisha na usafiri wa kudumu. Haya malori hayafai kabisa yameisha tia watu hasara. hata samaki wakiwa wamekaushwa gari ikiharibika usababisha hasara sana. Ila hizo ni changamoto ambazo ukizijua mapema ni vyema kuzitafutia ufumbuzi haraka.
Kama utapata soko zuri za sangala uko arusha, kumbuka sangala mwanza anakuwa na thamani kwa vitu vikuu viwili.
Kwanza mnofu kwenye viwanda na pili ndani ya sangala tumboni kuna kitu wanaita bondo sijajua kama ni kiswahili au la ila nimezoea kusikia wanaita hivyo, hii kitu ni hela sana kwa sangala alie mkubwa. watu wa Arusha usiwauzie na hilo bondo litoe na ukaliuze Mwanza kwa Wachina hela nzuri.
Nahisi usingize ngoja nilale nitakupa data kesho tena.
PACKAGE NZURI NA MTINDO WA DELIVERY NI MUHIMUWazo zuri ndugu, kama walivyopita washauri wengine. Kwanza unatakiwa utembelee eneo husika na kuangalia uhitaji gharama za usambazaji, pia kwa ushauri wangu kwa kuwa arusha ni jiji kubwa package yako na deliver transit inabidi iendane na mandhari ya sehemu unayopeleka, e.g serena hotel uki delivery kwa head hiyo ni soo. Usafi ni kitu muhimu katika biashara ya chakula. ili ufanye biashara yenye tija obseve this.
1. Tafuta sare yako ili uonekane uko serious na kazi yako
2. Kama una usafiri hata (pikipiki yenye refrigerator) kwa ajiri ya ku distribute orders
3. Kumbuka utahitaji watu wa kukusaidia ili kuendana na mda wa order husika
4. Je, utakuwa unauza kwa jumla au reja reja
All the best.
UTOFAUTI WA SANGARA NA SATOBei ya sangara na sato inatofautiana. Sato siku zote iko juu. Kwenye kipindi cha mvua samaki wanapatikana wengi na kwa Bei nafuu. Kipindi hiki samaki sangara kilo kwa jumla ni 4500. Wakati sato anaenda mpaka 5500.
Samaki wanapimwa kwa kilo. Unaweza kununua moja kwa moja kutoka kwa wenye mitumbwi yao au kutoka kwa walanguzi ambao wao huzinunua kwa wingi na kuzihifadhi Kwenye mafriza baada ya kuwatoa mautumbo na mabondo.
Hawa walanguzi ndiyo wenye Bei niliyokupa hapo juu. (Ukumbuke Bei hubadilika ) walanguzi hawahawa ukitaka samaki wanakufungia vizuri na kuwapakiza Kwenye mafuso. Fuso zote zinapakulia pale urafiki freti. Ila unalipia usafiri mwenyewe.
Kuhusu kibali mlanguzi huwa anakibali na mwenye fuso anakibali cha usafirishaji. Na ushuru utalipwa na mlanguzi. (Ukitaka namba ya mlanguzi utaniambia).
Bei ya kuuza huku samaki mbichi kilo ni kuanzia elf 8-10.
Of course ukitaka kuwa na frem lazima uwe na leseni nenda halmashauri na tra lazima ikuhusu.
Ukitaka nafuu sambazia mzigo ukiwa home kwako.
UZOEFU KATIKA UVUAJI NA UUZAJI WA SAMAKI
Mimi Nimevua SANGARA ziwa Victoria, Sato tulikuwa tukiwakamata mara chache kwasababu tulikuwa tuna vua maji ya kina kirefu.
Mimi nimewahi kuvua ziwa Victoria kisiwa cha kome na visiwa jirani huko. Biashara ya uvuvi siyo rahisi na siyo ngumu. Urahisi wa biashara hii ikiwa wewe mwenye mtaji utaamua kuishi kambini na wavuvi wako, ukisimamia ukiwa site kabisa, yani anzisha kambi, wavuvi wengi tu, wanakuja wenyewe mnaanza kazi.
Malipo inategemea na wewe mwenyewe, unaweza kuwaliapa pesa, au ukawapa siku zao za uvuvi kama sehemu ya malipo yao. Yaani wanakuvulia Jumatatu mpaka Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wanavua lakini nizao au ndio malipo yao, wakipata sawa wakikosa pia wanelewa. Ila gharama za kuwalisha ni zako mwenye kambi, unanunua Unga tu, samaki wanapatikana ziwani kama kitoweo.
Unaweza ukawa unauza samaki wabichi, kwa wamiliki wa viwanda au kuna wachuuzi wa wenye viwanda wanazunguka na mzani wananunua na kupeleka kiwandani, ama unaweza wachana samaki ukawatia chumvi na kuwakausha juani kule wanaitwa Kayabo, soko lao ni Zaire, na Zambia kwa sana.
Unahitaji kuwa na mitumbwi ya kuvulia kadhaa kutokana na mtaji wako na mahitaji yako, unahitaji kuwa na Injini za boti atleast Mbili. Kwasababu unahitaji pia kufanya doria ya nyavu zako, wavuvi ni wezi kama ilivyo kwa sehemu zingine, kama huna speed bot na hufanyi doria, hao hao wavuvi wako wanongea na wenzao wa maeneo mengine wanakuja kukuibia nyavu zote.Lakini wakijua una speed boti na unafanya doria pia umiliki bunduki wataogopa. Nimefanya kazi hizo za usimamizi miaka mingi kidogo imepita lakini huo ni uzoefu nilio upata huko.
Najua uzi huu labda ume expire lakini niliona ni shere labda uhitaji bado upo.
Naomba kuwasilisha.