Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vile vya kawaida) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vile vya kawaida)

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kifulambute, Aug 29, 2011.

 1. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,512
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Wana jamii jamani hebu nisaidieni
  Nataka kufanya hii biashara ya kuuza vinywaji jumla kwa arusha inakuwaje?

  Twilumba post:
  Wana JF habari za Jumapili!

  Naamini na ntaendelea kuamini kuwa JF ni kisima cha hekima na ushauri na ndio maana naleta kwenu ombi la ushauri juu ya uaanzishaji wa duka la vivywaji vya jumla.

  Kimsingi eneo nilipo linauhitaji wa duka la vinywaji vya jumla, baada ya kugundua hilo nimeona nipate ushauri namna ambavyo naweza kuanzisha duka hilo
  Kwa haraka haraka eneo (Location) kwa ajili ya biashara hiyo ipo na ni centre nzuri tu.

  Mwenye uzoefu namna ambavyo naweza kuanza biashara hiyo, kiasi cha mtaji , vinywaji kipaumblele, namna ambavyo naweza ku-link na depo za makapuni ya vinywaji hasa kwa mkoa wa (Arusha) kwa ajili ya ununuzi na la msingi kabisa upatikaji wa cret kwa ajili ya kuanzia, namna ya ununuzi wa pombe kali yaani gin, grands, wine na jamii zake.

  Kwa mawazo na uwezo wangu nilitaka nianze na cred 100 za beer, 100 za soda, kuhusu vinywaji vikali ntaomba kushauriwa zaidi!

  Nashukuru kwa ushauri ambao utatolewa!!
  Karibuni kwa ushauri.

  RUDVANNESTROOY post:

  Msaada kwa mtu yeyote anayejua Biashara hii ya Vinywaji vikali na Luxury (mf. wisk na wine), Naomba anieleweshe kwa kina.Mimi nipo hapa Dar na mtaji wa million 5.
  Vitu ninavyohitaji kufahaumu kwa kina ni:-
  1.Mtaji wa kuanzisha duka la biasahara hii (initial capital.
  2.Mazingira yanayo faa kwa Bisahara hii, je ni karibu na bar kama ninavyofikilia mm?
  3.Mahali zinako patikana bidhaa kwa urahisi na kwa bei nafuu
  4.Utaratibu wa kupata leseni wa hii biashara pamoja na gharama zake
  5.Ni bidhaa zipi zinakua na wateja sana hasa zinazofaa kwa kuanzia biashara?
  6.Faida na Changamoto zake.
  7.Nini ushauri wako kuhusiana na wazo hili na bishara hii?

  Natumaini wenye kufahamu zaidi juu ya bishara hii na ni serious people watanisaidia mawazo bora na kujibu maswali hayo hapo juu.
  Nitashukuru kwa ushirikiano wako.


  ================================================
  MAJIBU KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI KUHUSU BIASHARA HII
  ================================================

   
 2. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  inakuwa poa, tafuta frem/pango, nunua vinywaji kwa wakala wakubwa au kiwandani, anza kuuza
   
 3. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,512
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Sijaifanyia research vizuri kama M ngapi hivi nitahitaji kuinvest?
   
 4. snochet

  snochet JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 1,271
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  duh,mkuu unahitaji pesa mingi,na kwa jinsi arusha ninavyoijua l;abda utafute kifaru muungane,cz lazma uwe na kausafiri cha kusupply kwa wateja wako,tena bureee,hapo ndo utapata watu,sikukatishi tamaa,kaza buti
   
 5. u

  ureni JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Sema unataka kuuza vinywaji gani manake kuna vinywaji vingi sana hapa duniani.
   
 6. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kifulambute, nadhani hiyo taito inahitaji marekebisho "Biashara ya vinyaji jumla"!
   
 7. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,641
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mkuu Uko sahihi sana....mtaji wa vinywaji jumla ni mkubwa sana halafu faida yake ni ndogo sana. labda uuegemee zaidi kwenye pombe kali ndo zenye faida ila nazo ziko nyingi feki. pia ushindani ni mkubwa sana sana..hao wakala wanaochukua moja kwa moja kiwandani pia husambaza mitaani kwa bei ambayo angekuuzia wewe ndo ukauze mitaani. cha msingi jitahidi uchukue moja kwa moja kama ni soda bonite au pepsi na kama ni bia basi SBL au TBL hapo ndo utauweza ushindani...otherwise it is very challengin biznez. talking from experience
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  watu mpo makini!
   
 9. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Wana JF habari za Jumapili!

  Naamini na ntaendelea kuamini kuwa JF ni kisima cha hekima na ushauri na ndio maana naleta kwenu ombi la ushauri juu ya uaanzishaji wa duka la vivywaji vya jumla.

  Kimsingi eneo nilipo linauhitaji wa duka la vinywaji vya jumla, baada ya kugundua hilo nimeona nipate ushauri namna ambavyo naweza kuanzisha duka hilo
  Kwa haraka haraka eneo (Location) kwa ajili ya biashara hiyo ipo na ni centre nzuri tu.

  Mwenye uzoefu namna ambavyo naweza kuanza biashara hiyo, kiasi cha mtaji , vinywaji kipaumblele, namna ambavyo naweza ku-link na depo za makapuni ya vinywaji hasa kwa mkoa wa (Arusha) kwa ajili ya ununuzi na la msingi kabisa upatikaji wa cret kwa ajili ya kuanzia, namna ya ununuzi wa pombe kali yaani gin, grands, wine na jamii zake.

  Kwa mawazo na uwezo wangu nilitaka nianze na cred 100 za beer, 100 za soda, kuhusu vinywaji vikali ntaomba kushauriwa zaidi!

  Nashukuru kwa ushauri ambao utatolewa!!

  Karibuni kwa ushauri.
   
 10. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Waungwana nasuburi ushauri wenu tafadhali!!
   
 11. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  sina uzoefu sana na mambo ya biashara lakini pamoja na kuwa umezingatia location, lakini pia angali unatarget nani awe mteja wako kwa mahali hapo,
  suala la crates kampuni za vinywaji wanaweza kukuazima,
  na pombe kali ukiwa nazo za aina mbalimbali i.e. gin, whisky, brandy, rum, liquer, champagne, nk.
  itakuwa ni nzuri na bei iwe reasonable,
  kwa maoni yangu labda wadau wengine wanauzoefu na haya mambo watakuelewesha
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Wadau salama !
  Naombeni mawazo yenu ya kina kabla sijaamua kujikita kwenye hii business
  Je ni mtaji kiasi gani unaweza kunitosha kufungua duka au store ya vinywaji Kwa jiji la DSM au Mwanza ..
  Vinywaji kama:-
  Whisky
  Wine..
  Nk ..
  Nk..
  Naomba pia muongozo kwani sijawahi fanya business hii ila wazo limenijia na nafikilia kuifanya.
  Naomba tuwezeshane kimawazo kwa wale mliona uzoefu wa mabusiness.
  **Natanguliza shukrani **
  FL1
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Fungua Bar tuwe tunakuja kunywa, mi niweke kaunta
   
 14. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Inahitaji mtaji mzito kidogo . Kama ni duka la saizi ya kati sio chini ya 100m .
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  hahaha Fidel80 am serious bana ,Bar mie siiwezi kukimbizana na wahudumu
  Nipe mawazo najua utakuwa mteja wangu mkubwa ,,,Huduma mpaka mlangoni
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Huo mtaji si bora afungue Bar tu
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Bucho bana Misri haikujengwa siku moja hebu punguza na fanya calculation zako upya
   
 18. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kwa mimi binafsi nilishindwa kuendesha duka la Wines &Spirits kutokana na kuwa ni mnywaji mno, nikaishia kulifilisi flat kabisa! KWAHIYO SITOONGEA NENO!

  Lakini ukiwa na nia ya kufungua duka la aina hiyo kwanza ujiridhishe sana na sehemu husika!
  Duka la Wines and Spirits linatakiwe liwe strong sana, lakini liwe na system ya surveilance maana mtu akichukua katoni moja ya eg Barcadi au Amarula, then ana uhakika kula siku kadha.
  Ni njema kama litakuwa mjini, au eneo lenye constant patrols za wanausalama, hii ni kutokana na Sales zake kuwa za amounts kubwakubwa, na ni rahisi sana kuingiliwa na wajasiriamali wenye mtaji AMBAO NI NGUVU YAO WENYEWE!
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mi ukiniweka meneja kazi itafanyika kwa ufanisi alafu Asprin anakuwa jikoni
  Hapo inategemea na mtaji wako unaweza anza kidogo kidogo huku ukiendelea kuongeza mtaji.
  Unaweza anza na creti 200 za bia ili wateja wasikose biya na unaweka mavinywaji yanayo nyweka sana kama mdogo ake safari, mjomba ake safari, binamu yake safari bila kusahau viloba vya kutosha kwa bei ya jumla hayo maBallantines mdogo mdogo
   
 20. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  huu ndo ukweli FL . Huwezi kuamini lakini chunguza utakuja kuniambia . Pombe sio chai .
   
Loading...