Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo sio Arusha, tatizo ni mahalh ilipo biashara yako, kwani Arusha yote kuna changamoto hizo hizo?
Video games zinafaida kwa akili, kwani nchi zilizoendelea mpaka wagonjwa wanashauriwa kuzicheza kwa ajili ya ubongo kuweza ku-charge zaidi kwa kufikiria kwa haraka, kufanya co-ordination kwenye mikono na pia kupunguza stress na depression, na sio kwa watoto tu. mimi nimekuwa nikifanya hii biashara kwa muda sasa, na nimekuwa nikifuatilia wanafunzi ambao wanakuja kucheza, matokeo yao shule vipi?
Wengi wao ni wenye kufaulu mitihani, na kama alikuwa anafeli matokeo ya mbele yanakuwa mazuri baada ya kucheza. Hatuwezi kuzuia maendeleo ya kidunia na technologia, na watoto wa siku hizi hawana michezo mingi nje kama zamani.
Ni kitu kigeni na mara nyingi kipya kinaonekana sio kizuri haswa kwa wasio fahamu. Upande wa tabia ya utoro na wizi, nasema, mtoto umleavyo ndio akuavyo. Matajiri wengi tu, wamewanunulia watoto wao hizi game kucheza nyumbani na wako vizuri tu kielimu, ni sisi walala hao ndio tunapigana wetu wasijue kitu, technologia hizi zipo, na zitaendelea kuboreshwa. mengine baadaye, hayo tu kwa sasa.
Kweli mahali nilipo mabadiliko naona wakati wake umefika, kwa arusha kuna maeneo mengine, lakini kutokana kupanda bei za tanesco, arusha hailipi sana, kwa sasa ninalipisha 500 kwa nusu saa, compare na dar, ambapo kuna sehemu nyingi tu, wanalipisha 500 kwa mechi moja ya mpira ambayo ni ya dakika 10 au 16 hivi kama sikosei. Mahesabu haya ndio naona inalipa zaidi dar, arusha maisha ni gharama sana na watu ni wachache wenye uwezo wa kuwapa watoto pesa.
ashukuru kwa maoni yote, je kwani dar si kuna sehemu zenye wakazi wengi zaidi, ni sehemu zipi na kodi ya kupanga je inakuwaje, naomba muendelee kunipa ushauri na maoni, hapa JF nimepakubali.
Pia niko tayari kuingia patnership na mtu wa dar ambaye ana interest na hii michezo na aliyekuwa na location available, games na tv ninazo za kutosha.
Kama kuna kifaa, nijuze, maana ndio maendeleo. Natumai kifaa chenyewe sio generator, hebu nieleweshe nifanyaje?
Haina shida mkuu, nakutakia kila la kheri.Nimekupata, haya mkuu huu ndio usaidizi.