Ushauri kuanzisha dry cleaner | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kuanzisha dry cleaner

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mayu, Jan 3, 2011.

 1. M

  Mayu JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Wadau naombeni msaada wenu wa mawazo kwani naamini yupo mwenye kujua kuhusu hili.
  Nini capital kama 7milion nataka kuanzisha dry cleaner katika sehemu ambayo hakuna kabisa hiyo kitu.
  je capital hiyo inaweza kutosha, pia sijui ni mashine gani nzuri ya kufulia bei ya wastani.
  pia nahitaji kujua nahitaji washing machine kama ngapi kuanzia labda ya kufulia nguo za kawaida suti, na kusafisha macarpet.
  Nawasilisha
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,602
  Trophy Points: 280
  Labda ungeongeza hiyo capital maana hapo pango bado...machines ni bei kidogo...kama ukiagizaa...kuna watu wanagiza au kama unaweza uagize mwenyewe ila kwa 7m nakushauri uongeze kama 7m zingine....la sivyo badilisha biashara! Nunua bajaj 2 ndio size yako...kwa pesa hiyo....ni ushauri wangu tuu...nami nilifanya research 2yrs back....
   
 3. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Thanks,
  Hata mie nina wazo la hiyo biashara. Sasa ni vizuri umesema umefanya research miaka miwili iliyopita....unaweza tumegea mchanganuo wake japo roughly?
  Thanks
   
 4. M

  Mayu JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Asante mkuu namimi nilitaka kujua hivyo.
  Mimi yangu nataka kufungulia mkoani na haswa kinacho nitatiza ni suti, siitaji kubwa sana kama za huku dar siunajua tena mambo ya mkoa
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,602
  Trophy Points: 280
  Wana JF wajasirimali...kwanza unatakiwa ujue kuwa kila dry cleaner machines zina kilo tofauti bei yake inatokana na hizo kilo kuanzia 10kg and above....

  Kama unataka ziwe mbili ina maana utaagiza set hizo 2 na machine za kusuuza...kunyooshea...pia...

  Nawapa link kwanza msome mjue hata zina hitaji nini...pia umeme lazima uwe 3phase line...

  Dry Cleaning Machine (Series CBC-4) - China Dry Cleaning Machine, Washing Machine, Dryer Machine in Washing & Drying Machine

  Dry Cleaning Machine (22kg) - China dry cleaning machine, industrial dry cleaning machine, industrial washing machine in Cleaning Machine

  Sasa anzia pango la sehemu..vibalii...umeme na kuagiza kutoa bandarini....na kuzifunga....then cost za ndani sasa....sabuni etc...

  Jipange sawa sawa....all the best$
  Uliza bei kwa hizo link watakupa....haraka sana ila FOB ni kama 5,000 hivi dola
   
 6. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Good info:
  Hebu saidia zaidi
  1) Hii machine inanyoosha nguo automatically? Naona kwenye hiyo ya 22Kg inaonyesha hivyo.
  2) Ina hitaji chumba cha ukubwa gani kwa mujibu wa utafiti wako?
  3) Nini conditions zingine ambapo hiyo machine inatakiwa iwekwe?

  Thanks
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,602
  Trophy Points: 280
  1.Ukubwa unategemea na unataka machine ngapi...na pia machine huwa zinakaa kwa nyuma...kumbuka mbele si mapokezi...unaweka partition...ili wakati mchakato(usiku) unafua..wateja hawaoni....pia lazima kunakuwa sehemu kutolea mvuke...

  Hiyo machine ni ya kisasa zaidi...na ndio ya katikati...kwa kuanzia sio mbaya..

  Wakati mwingine unahitaji generator(onana watalam wa umeme na size hizo ujue ukubwa wa generator)...kama umeme unasumbuaa maana kazi za watuu zitalala...
   
 8. M

  Mayu JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2011
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Mkuu asante kwa info nzuri sasa umenipa mwangaza zaidi, nadhani nimepata pa kuanzia.
  ingawa bei inaonekana kama imesimama, vipi uliwahi kujaribu kucheck amazon na ebay kwa used mashine?
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hii biashara ya dry cleaner inabidi uwe umejipanga kisawasawa hasa kwenye suala la generator maana umeme wa bongo ni kama ugonjwa wa moyo at any time you get screwed so namshauri angalie genrator zinaoendana na capacity ya hizo mashine anazotaka kuagiza all in i think for 7 million capital bado ni ndogo sana unless kama target ya biashara yake iko tofauti
   
 10. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Bado unaweza kuanza, kimkakati - mkoani sidhani kama italipa.

  Kama upo Dar chagua eneo moja la kuhudumia kwa mfano vyuoni ukaanzania Mlimani ukaunganisha na vyuo vya jirani au nenda kwenye hostels kubwa kubwa. Hauhitaji kufungua duka ila unatakiwa kununua bajaj moja kuifanya kuwa duka la kutembea. Bajaj yako jaribu kuijengea ka-body and then tenga sehemu mbili; upande mmoja ya kuchukulia nguo chafu na upande wa pili kuchukulia nguo safi zinazorudishwa.

  Kwa kuanza huhitaji mashine, ili kukupunguzia gharama za uendeshaji. Ajiri watu wawili wa kufua na mmoja wa kunyoosha na ku-pack nguo vizuri. Kazi hizi unaweza kuzifanya kutokea nyumbani (kama haukupanga chumba). Maji Dar ni mgao itakubidi kununua tank la kuhifadhia maji, ukipata ya kubeba lita 5000 itafaa sana. Ajiri mlinzi mmoja kukuangalizia nguo zilizoanikwa.

  Hii ni biashara kama zingine hakikisha unapata vibali na kujitambulisha kama mlipa kodi ili kuhalalisha shughuli zako. Tafuta label yako ya kukutambulisha eg DOWANS Laundry Services. Label na contact zako zote ziweke kwenye bajaj, zing'arishe kadri utakavyoweza. Kazi kubwa utakayofanya mwanzo mwanzo ni kutambulisha biashara (promotion) na kazi hii itabidi uifanye bila kuona aibu. Kwa huo mtaji nakushauri kazi ya promotion ufanye mwenyewe na jinsi hiyo itakubidi pia uwe dereva bajaj.

  Nakutakia mafanikio mema.
   
 11. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,602
  Trophy Points: 280
  Kama unataka used ones nenda www.alibaba.com hapoo dubai utapat*....all the best...mimi nilipata wazimu...na biashara upate sehemnu nzuri ya kuiweka...utashangaa..baada mwezi linatokeaa jitu lenye pesa...halikujuaa,..wapi aka invest utakoma jibu lake next 2 doors balaa ndio linaanzia hapo
   
 12. M

  Mayu JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2011
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Hii mitaji itatuua jamani.
  Mkuu mfano kama unaanzisha na mashine moja tu na ikitokea umeme hamna unafua manual tabu ipo kwa makoti ya suti,
  target yangu ni mikoa ya singida au tabora najua wateja sio wengi sana, just kuanzia. hii imekaaje?
   
 13. M

  Mayu JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2011
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Mkuu wazo lako angalau limenitia moyo.
  Mimi nimehamishiwa mkoa kikazi hivyo baada ya kutafiti nikaona biashara hii hakuna ndio maana nikaona nitumie nafasi hii kuanzisha.
  Tatizo wanasema kufua makoti ya suti mashine ni lazima
   
 14. M

  Mayu JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2011
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Mkuu kweli huo ni mtihani mgumu, unaangaika kuanzisha kitu, ukianza tu from no where wenye mihela yao wanakuja hivyo hivyo.
  Lakini ndio hivyo tunaambiwa wajasiriamali sikuzote ni ma risk taker
   
 15. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60


  Interesting, though painfully true!
  Hata hivyo, ndivyo law of demand and supply in a perfect competion market inavyotuonya. Mnapouza bidhaa zinazofanana kunatokea price war, na hiyo hushusha bei ya vitu. Lakini linapokuja jamaa lenye mtaji mkubwa, litashusha bellow economic level, na litakuwipe out kutoka kwenye soko.
  Hata hivyo, unaweza survive na kamtaji kako kwa njia nyingi, na ya juu zaidi ni customer care na uaminifu. Kama una jina zuri, hata kama akaja mtu mwenye pesa pale, watu wataendelea kuwa Royal kwako bila kujali ukisasa wa machine ya rival wako.
  Mfano mzuri, ni Salon za kunyolea nywele mijini, zipo zingine za kisasa kabisa, lakini hazina wateja na zingine ndogo zinafurika: Sababu ni kwamba custors wameshaipenda kazi yako hivyo wamejenga bond iliyo zaidi ya biashara !
  So jirushe tu kama unaweza, na jitu likija na mipesa yake we unaweza ku-relocate au kubuni biashara mbadala......au kuingia naye ubia kama yuko tayari!
   
 16. Baiskeli

  Baiskeli JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 335
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  sikiza mkuu usikate tamaa 7m unaweza kabisa anzisha hiyo kazi, tafuta machne ndogo tu ya kawaida kama hizi za majumba unapata machine nzuri tu kwa 1m inayofua na kukausha. haitaji 3phase. inauwezo wa kufua jeans 20 kwa saa. Muhimu ni sehemu ya biashara na matangazo. tengeneza office kali sana especially mapokezi fenicha zilizoenda shule, print bango moja kali sana liwe na picha ya mrembo mkali, bango liwe kubwa lijae pote kwa nje usiku liwake taa kali. usisahau kuandika unafua kwa machine za kisasa na wataalamu kutoka dar. tafuta mtu wa kunyoosha nguo mzuri asiwe wa hapo singida. usiruhusu watu kujua siri ya urembo wa ndani we wacha wababaike na urembo wa nje. weka na mfuaji 1 Wa mikono standby umeme ukikatika anacover. print vipeperushi vikali sambaza maotelini na maofisini. toa muda kwa mteja unaowezeka. mkuu mwanzo mgumu 7m kwa style hii utaweza. mwaka 1 utakuwa ushafunga hizo mashne.
   
 17. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu, mkoa suti si nyingi sana labda Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma - zipotezee kwanza. Mkakati ni ule ule, badala ya kwenda vyuoni au kwenye hostels zungusha bajaj mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba huko ulipo utafanikiwa. Anza kwanza, utajiimarisha kadri siku zinavyoenda.
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,602
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakushaurii pia angaliaa hata biashara zingine hapo vipi car wash...??nayo ni nzurii tafuta bar maarufu,,......fungua kwa pembeni...utapata hata gari 5 tu kwa siku za kawaida na hata 10 kwa kila week end inatosha kwa 7m unapata machine na kujenga /tank lako la maji na pump machine..saafii kabisaa........fikiriaa na hii piaa dry cleaner inasum bua kidogo kwa vimitaji vyetu.....maana ukikwama utashindwa kuuza....kirahisi hizo machine
   
 19. P

  Paul S.S Verified User

  #19
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mayu nataka nikutie moyo kuwa unaweza kabisa kufungua hiyo biashara kwa huo mtaji wako wa m7 (nahisi ni hela yako ya uhamisho ).
  Chakufanya kwanza anza na mashine ndogo ya wastani najua mkoani wateja mwanzo hawatakuwa wengi kivile, nunua washing mashine ya kama m1 hadi m2, inatosha sana kwa kufulia nguo za kawaida kama mashati, suruali, magauni, sketi, bauzi.pia mashuka, mapazia,nk.
  Makoti hayafuliwi na washing mashine yana utaratibu wake wa ku dry clean, waweza tafuta kuna dry cleaner simple kwa aajili ya kusafishia makoti manual.
  Pia tafuta mshine ya kusafishia makarpet ya kama lk5 inatosha sana nahii unaweza kuwafuata wateja hata majumbani si lazima walete ofisini.
  Cha umuhimu tengeneza ofisi kali inayovutia nje na ndani, weka muudumu smati hakikisha unatoa muda sahihi kwa mteja kuja kuchukua nguo zake.
  Hakikisha unapata mifuko ya plastiki na enga simple kuwekea nguo za wateja.
  Siku za mwanzo uwe kipromotion zaidi kwa kutoa viofa vya hapa na pale mfano, mteja kaleta nguo kumi basi mbili mwambie unamfanyia free.
  Mikoani kuna tv cable zinafanya matangazo bei powa sana, peleka matangazo,tengeneza vipeperushi vizuri jisifie sana kuwa unafua kutumia mashine na utaalamu wa kisasa zaidi.
  Kaunta ukiweza weka ka pc pale, feed kila kitu ili uwe unatoa risiti nk utaonekana makini na smati zaidi.
  Hakikisha at start zoezi unalisimamia wewe mwenyewe na hakikisha customer care ndio silaha yako no moja.
  Jitahidi upate ofisi sehemu nzuri kama katikati ya mji, unahitaji ofisi kwa maana ya sehemu ya kupokelea na kutoa nguo, hii ndio inayohitajika iwe ya viwango.
  pia unahitaji sehemu ya kufulia na kuanikia hii inaitwa factor, hapa inaweza kuwa hata nyumbani kwako kama utakosa sehemu utakayoshindwa kuigawa ofisi na factory.
  Pia kuwa mjanja si kila mara uwe unatumia washing mashine wakati mwingine tumia watu wako kufua kawaida labda kwa nguo maalum.
  Google namna mbali mbali za kufua aina mbali mbali na kupiga basi even how to dry clean suit nk jifunze mwenyewe kisha wafundishe watu wako na wasimamie.
  Mwisho nakutakia kila la heri ndugu yangu na usisite kurudi ukumbini kutujuza yaliyojiri
   
 20. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,455
  Likes Received: 2,038
  Trophy Points: 280
  ulichoongea ni sahihi kabisa hata mimi nilitaka kumpa ushauri huu huu, Milioni 7 inatosha kabisa kuanzisha biashara ya Dry Cleaner ndogo ya kawaida tu kwani kwa mkoa uliopo nina uhakika kodi za vyumba vya biashara si kubwa kama DSM na pia kwa kuanzia nunua mashine za kawaida tu kama tunazotumia majumbani ila ziwe zenye capacity kubwa kidogo ambazo bei yake ni kuanzia laki 6 mpk milioni 1 nunua kama 3 hivi moja ya milioni na nyingine say za laki 8 na 6. Hakikisha mojawapo iwe inafua na kukausha kwa ajili ya wateja wenye haraka na hizo nyingine unatumia wakati mtu hana haraka kwa mfano akileta suti leo unamwambia aje kuchukua kesho kutwa

  pia uwe na mtu (dobi) ambaye atakuwa anafua kawaida nguo za kawaida na kuzianika na kupiga pasi vizuri kisha kuzihifadhi kwenye mifuko maalum yenye nembo ya Dry Cleaner yako.

  Mtaji ulionao ni mkubwa sana wala watu wasikukatishe tamaa ila cha muhimu ni kuangalia demand ya hiyo huduma ktk sehemu uliyopo ndio itakayokuahakikishia kuendelea kwa biashara yako

  Kwa kuanzia jaribu kuwa na mashine moja ya milioni yenye kufua na kukausha halafu ukiona soko ni zuri ongeza nyingine mbili kama nilivyokushauri hapo juu na kama ikichanganya zaidi ndipo ufikirie kuagiza mashine kubwa kutoka nje kama wengine walivyoshauri ila kwa sasa anza na mashine za kawaida za majumbani ambazo bei yake ni nafuu na zinafanya kazi vizuri tu maana mie nina mashine nilinunua laki 5 Mlimani City wakati ndio imeanzishwa na inatumika mpk leo na inafua vizuri tu na nina uhakika hata ningeitumia kwa biashara ingemudu vizuri tu kwani inafanya kazi poa sana

  Pia ukishaanza hiyo kazi tafuta tender kwenye mahospitali ya kufua mashuka na nguo zingine zinazotumika hospitali unaweza kutoka ila anza kidogo usiweke hizo hela zote mpaka usome soko kwenye ndio uweke hiyo M7 yote

  Wengi humu wanakuchuuza kwa kufikiria maofisi makubwa kwa zile dry cleaner za Shoppers Plaza au Namanga wakati mikoani wala hmna wateja kihivo

  Kwa ushauri wa kibiashara: funzadume@yahoo.com
   
Loading...