Ushauri: Korosho si nguvu za kijeshi, Ni somo la uchumi

nikisoma hzi thread za korosha nazidi kuchanganyikiwa

tatizo moja la raisi wetu wanaomshauri wanamshauri kisiasa hilo tu na si vingonevyo
Mimi nachanganyikiwa mtu anaposema
" wanaomshauri Rais wanampotosha"
Hivi malaika /Jabari la Chato si lilishswakanya nyie kuhusu suala la yeye kushauriwa?

Magu hana mshauri zaidi ya Bashite...saaana akizidiwa anavuta waya kwa Mkwere.
 
Amiri jeshi mkuu kaagiza eti jeshi likae standby huku logistical arrangements za kwenda kusomba Korosho zikiwekwa sawa. Sasa wanaisomba kuzipeleka wapi?? wanazinunua au wanachukua kwa mkopo wawasaidie wakulima kuziuza nje?

Sometimes unaweza kujiuliza bwana mkubwa a.k.a Jiwe huwa anawaza nini? hana washauri? au ni wale watu ambao wao ndo huwashauri washauri wao?
 
introvert ,

..kwenye nchi za wenzetu bei inaposhuka na serekali huwa inawasaidia wakulima namna gani?

..je, hutumia utaratibu kama huu anaotumia JPM au huchukua hatua tofauti?

..Zaidi, wakulima wa mazao mengine kama kahawa, pamba, mahindi, etc na wao watasaidiwa ikiwa bei zitaporomoka?
 
Kwa mfano, hitaji (demand) ya korosho kwa walaji ni tani 100 na uzalishaji ni tani 200 mwaka huu lakini mwakani hitaji (demand) ya korosho kwa walaji ni tani 150 na uzalishaji ukaongezeka ukawa tani 400, ni lazima bei ya korosho (malighafi) ishuke.

uzalishaji umezidi mahitaji misimu yote miwili, kwa hiyo bei ilikuwa ndogo misimu yote miwili, sasa tofauti ya hiyo misimu miwili ni nini?

unatoa scenario ambayo uzalishaji ni double the levels of mahitaji miaka yote miwili, halafu unasema ni mfano. Don't be silly
 
WanaJF,

Leo tumesikia/tumeona hotuba ya Rais Magufuli juu ya korosho. Serikali itanunua korosho, takribani tani 210,000, iwapo wafanyabiashara hawatazinunua kwa bei ya TZS 3,000/kilo itakapofika Jumatatu saa kumi jioni. Rais ameandaa jeshi kusaidia zoezi hili.

Pia Rais Magufuli amemfuta kazi Waziri wa Kilimo Charles Tizeba kutokana na sakata hili.

Hatari ya kuingiza siasa kwenye uchumi ni kupata mafanikio ya muda mfupi na hasara kubwa sana ya muda mrefu - short termism.

Tani 210,000 kwa bei ya TZS 3,000 kwa kilo ni sawa na Shilingi bilioni 630. Karibia nusu ya bajeti ya wizara ya elimu kwa mwaka. Ukizingatia wizara zinapata asilimia 50% ya bajeti basi hii ni sawa na bajeti halisi ya wizara ya elimu.

Swali la kwanza, Je, serikali ikinunua hizi korosho kwa kodi za wananchi itamuuzia nani na kwa bei ipi? Kununua kwa wakulima kwa bei ya TZS 3,000 kwa kilo ina maana inapaswa kuuza kwa bei zaidi ya hiyo kwa wafanyabiashara wa nje, Je, inawezekana?

Kwanza kabisa, korosho ya Tanzania hainunuliwi na mlaji wa mwisho (consumer). Korosho ya Tanzania ni malighafi (raw product) inayonunuliwa na makampuni ya korosho kutengeneza final product kwa mlaji.

Wateja (makampuni) ya korosho zetu ni India na Vietnam. Makampuni haya yananunua korosho (malighafi) sehemu tofauti duniani. Formula ni rahisi kwao, wanahitaji kununua kwa bei rahisi ili kupata faida kubwa. Huu ni ubepari hauna kuoneana huruma.

Msimu huu wa korosho, uzalishaji upo juu kutokana na nchi nyingine kuzalisha kwa wingi. Hii imepelekea bei kushuka.

Hii haihitaji nguvu ya jeshi, ni kanuni za uchumi.

Serikali leo hii ikishindwa kuuza korosho kwa bei ya faida, itaweka kwenye ghala isubiri msimu ujao. Hii itakosesha Tanzania fedha za kigeni kwa msimu huu na pia ni pata potea (speculating) ya pesa za walipa kodi. Hususani thamani ya pesa mwaka huu si sawa na mwakani.

Swali la pili, iwapo uzalishaji ukaongezeka zaidi ya uhitaji msimu ujao, Serikali itafanya nini? Kwa sababu wakulima watakuwa wana korosho kwenye maghala na serikali itakua na korosho kwenye maghala. Moja kwa moja bei itazidi kushuka na wakulima watategemea Serikali inunue kwa bei ileile. Hasara zaidi kiuchumi.

Swali la mwisho, wakulima wa mazao mengine kesho na kesho kutwa watataka Serikali inunue kutoka kwao. Serikali itaweza?

Huu ni mtego. Hili ni suala la uchumi si siasa. Wanasiasa wamemtega na ametegeka.

Njia bora ya kusaidia mkulima ni kumpunguzia gharama za kilimo kwa kumpatia ruzuku au kumpunguzia bei ya inputs, si kununua mazao yake.

Muda ni hakimu.
anaelewa, unampigia mbw. Gitaa.
 
introvert ,

..kwenye nchi za wenzetu bei inaposhuka na serekali huwa inawasaidia wakulima namna gani?

..je, hutumia utaratibu kama huu anaotumia JPM au huchukua hatua tofauti?

..Zaidi, wakulima wa mazao mengine kama kahawa, pamba, mahindi, etc na wao watasaidiwa ikiwa bei zitaporomoka?
Wanunuzii, wakanunua kwa Tshs 2700 na wewe unawafidia kwa tshs 300, kutoka kwenye mfuko wa korosho, ambao umemezwa na chatou piga mwenyewe hesabu uone nani ana akili.
 
105926.jpg

Nakumbuka wakati nalima mahindi mkoani Rukwa miaka hiyo, kuna jamaa walikuwa wanatubania sana katika bei. Kuna bwana mmoja akaamua kununua mahindi yetu kwa bei nzuri akahifadhi hadi bei ilipokuwa nzuri. Wale waliokataa kununua awali walipokuja kutulazimisha tulime na kuuza kwao, tuliwaeleza sisi tunataka kumuuzia yule yule huwa ananunua kwa bei nzuri. Jamaa wakaanza wao wenyewe pia kulima ili wakamuuzie yule bwana na yule bwana akagoma kununua kwa wale wauzaji wapya. Historia hii inanikumbusha yanayojiri sasa. Licha ya kwamba serikali imeamua kununua sasa(kama wanunuzi waliotarajiwa hawataonesha nia), ni imani yetu kuwa misimu ijayo masoko ya dunia yatakuwa katika hali nzuri. Zipo nchi nyingi duniani zenye uhitaji wa korosho. Kuuza si Tanzania tu, bali hata nje ya Tanzania. Zingatia kwamba, 'serikali ina mkono mrefu'. Inaweza kutafuta nchi yoyote duniani yenye uhitaji na kuingia makubaliano rasmi na muuzaji mkuu akawa serikali. Ananunua korosho 3000 anauza 5000. Hapo sasa ndio wakulima tutaongezeka ili tuuze nje...Tuunge mkono hatua ya kuwanusuru wakulima wetu, tusibeze hatua hiyo ya serikali yenye tija kwa wanyonye washindao mashambani. Nimetafakari sana baada ya kuona wanaobeza hatua hiyo ni watu wa mijini (wanunuzi wa korosho za kwenye pakiti kwa 'matumizi ya nyumbani na mahotelini').
 
Vichaa mara nyingi brain power yao inakuwaga low.. yaani very low. Ni rahisi sana kwa serijali ku cover variance ya TZS 300 kwani itagharim close to 60BN kuliko kununua mzigo mzima kwa 600BN wakati hujui utamuuzia nani na kwa sh ngapi na lini.. Huu ndo ukichaa halisi.. jiwe atakuwa kichaa kwa sababu anashindwa hata arithmetic rahisi kiasi hiki?

Hizo 250BN alizokwapua kwa wenye korosho alimhonga nani?

Kingine ni kwamba hii issue siyo ya kisheria, maana yake hakuna sheria iliyotumika na inayompa mamlaka ya kufanya anavyotaka kufanya. Bunge lipo, mahakama ipo.. lakini ndo walamba viatu wanapiga makofi. Hivi amekosekana mbunge mmoja mwenye akili hata kidogo tu ya kuanzisha motion ya kuzuia ukichaa huu? Namkumbuka sana shujaa TL
 
View attachment 929380
Nakumbuka wakati nalima mahindi mkoani Rukwa miaka hiyo, kuna jamaa walikuwa wanatubania sana katika bei. Kuna bwana mmoja akaamua kununua mahindi yetu kwa bei nzuri akahifadhi hadi bei ilipokuwa nzuri. Wale waliokataa kununua awali walipokuja kutulazimisha tulime na kuuza kwao, tuliwaeleza sisi tunataka kumuuzia yule yule huwa ananunua kwa bei nzuri. Jamaa wakaanza wao wenyewe pia kulima ili wakamuuzie yule bwana na yule bwana akagoma kununua kwa wale wauzaji wapya. Historia hii inanikumbusha yanayojiri sasa. Licha ya kwamba serikali imeamua kununua sasa(kama wanunuzi waliotarajiwa hawataonesha nia), ni imani yetu kuwa misimu ijayo masoko ya dunia yatakuwa katika hali nzuri. Zipo nchi nyingi duniani zenye uhitaji wa korosho. Kuuza si Tanzania tu, bali hata nje ya Tanzania. Zingatia kwamba, 'serikali ina mkono mrefu'. Inaweza kutafuta nchi yoyote duniani yenye uhitaji na kuingia makubaliano rasmi na muuzaji mkuu akawa serikali. Ananunua korosho 3000 anauza 5000. Hapo sasa ndio wakulima tutaongezeka ili tuuze nje...Tuunge mkono hatua ya kuwanusuru wakulima wetu, tusibeze hatua hiyo ya serikali yenye tija kwa wanyonye washindao mashambani. Nimetafakari sana baada ya kuona wanaobeza hatua hiyo ni watu wa mijini (wanunuzi wa korosho za kwenye pakiti kwa 'matumizi ya nyumbani na mahotelini').

Kwa bajeti ipi? Kwa utaratibu upi? Serikali haina competency katika ku trade commodities... itaishia tu kupigwa tena vibaya zaidi..

Kwa sababu serikali ya vichaa haitabiriki, ni vigumu sana hata wawekezaji kujenga viwanda hapa nchini vya kuongeza thamani ili badala ya kuuza korosho ghafi, iuzwe bidhaa iliyokuwa tayari kutumika na mlaji..

Kutotabirika kwa shi.t.ho/e governments ni hasara sana.. na ndo ilivyo kwa nchi nyingi za Afrika. Hakuna institutions za kufanya "checks and balances" kwa hiyo unakuta hata mtu akifanya maamuzi akiwa kwenye mwezi mchanga hakuna wa kuhoji. Maamuzi kama haya yanasababisha shi.th.o/lers kwenda mbele hatua moja na kurudi nyuma hatua tano..

Kwa ufupi uamuzi wa jiwe ni wa kukurupuka na wa kipuuzi usiokuwa wa tija kwa taifa wala kwa wakulima.. kwani mbaazi ziliishia wapi? Mbona hajawahi kujenga kiwanda cha biscuits?
 
Katika hili mkuu kategwa nae kategeka, kasahau rules of the game kaamua kutumia nguvu bila kujua nguvu zake zinaweza kumuumiza yeye mwenyewe.
 
WanaJF,

Leo tumesikia/tumeona hotuba ya Rais Magufuli juu ya korosho. Serikali itanunua korosho, takribani tani 210,000, iwapo wafanyabiashara hawatazinunua kwa bei ya TZS 3,000/kilo itakapofika Jumatatu saa kumi jioni. Rais ameandaa jeshi kusaidia zoezi hili.

Pia Rais Magufuli amemfuta kazi Waziri wa Kilimo Charles Tizeba kutokana na sakata hili.

Hatari ya kuingiza siasa kwenye uchumi ni kupata mafanikio ya muda mfupi na hasara kubwa sana ya muda mrefu - short termism.

Tani 210,000 kwa bei ya TZS 3,000 kwa kilo ni sawa na Shilingi bilioni 630. Karibia nusu ya bajeti ya wizara ya elimu kwa mwaka. Ukizingatia wizara zinapata asilimia 50% ya bajeti basi hii ni sawa na bajeti halisi ya wizara ya elimu.

Swali la kwanza, Je, serikali ikinunua hizi korosho kwa kodi za wananchi itamuuzia nani na kwa bei ipi? Kununua kwa wakulima kwa bei ya TZS 3,000 kwa kilo ina maana inapaswa kuuza kwa bei zaidi ya hiyo kwa wafanyabiashara wa nje, Je, inawezekana?

Kwanza kabisa, korosho ya Tanzania hainunuliwi na mlaji wa mwisho (consumer). Korosho ya Tanzania ni malighafi (raw product) inayonunuliwa na makampuni ya korosho kutengeneza final product kwa mlaji.

Wateja (makampuni) ya korosho zetu ni India na Vietnam. Makampuni haya yananunua korosho (malighafi) sehemu tofauti duniani. Formula ni rahisi kwao, wanahitaji kununua kwa bei rahisi ili kupata faida kubwa. Huu ni ubepari hauna kuoneana huruma.

Msimu huu wa korosho, uzalishaji upo juu kutokana na nchi nyingine kuzalisha kwa wingi. Hii imepelekea bei kushuka.

Kwa mfano, hitaji (demand) ya korosho kwa walaji ni tani 100 na uzalishaji ni tani 200 mwaka huu lakini mwakani hitaji (demand) ya korosho kwa walaji ni tani 150 na uzalishaji ukaongezeka ukawa tani 400, ni lazima bei ya korosho (malighafi) ishuke.

Hii haihitaji nguvu ya jeshi, ni kanuni za uchumi.

Serikali leo hii ikishindwa kuuza korosho kwa bei ya faida, itaweka kwenye ghala isubiri msimu ujao. Hii itakosesha Tanzania fedha za kigeni kwa msimu huu na pia ni pata potea (speculating) ya pesa za walipa kodi. Hususani thamani ya pesa mwaka huu si sawa na mwakani.

Swali la pili, iwapo uzalishaji ukaongezeka zaidi ya uhitaji msimu ujao, Serikali itafanya nini? Kwa sababu wakulima watakuwa wana korosho kwenye maghala na serikali itakua na korosho kwenye maghala. Moja kwa moja bei itazidi kushuka na wakulima watategemea Serikali inunue kwa bei ileile. Hasara zaidi kiuchumi.

Swali la mwisho, wakulima wa mazao mengine kesho na kesho kutwa watataka Serikali inunue kutoka kwao. Serikali itaweza?

Huu ni mtego. Hili ni suala la uchumi si siasa. Wanasiasa wamemtega na ametegeka.

Njia bora ya kusaidia mkulima ni kumpunguzia gharama za kilimo kwa kumpatia ruzuku au kumpunguzia bei ya inputs, si kununua mazao yake.

Muda ni hakimu.
Dah umekonga roho yangu kwa ufafanuzi maridadi; natamani tungekuwa na watu kama wewe kwenye NATIONAL ECONOMIC COUNCIL badala ya Kamati za ulinzi na usalama utafikiri nchi iko vitani!!!
Big up man!
 
Yote unayoongea yanaweza yakawa sawa lakini kama nchi hatuwezi kuwa bulldozed na wafanyabiashara.Kuna vitu kaka vinahitaji maamuzi magumu.

Hakuna mfanyabiashara anayetaka kupata hasara. Hivyo, huwezi kumlazimisha mfanyabiashara anunue kwa bei isyokuwa na faida kwake. Si suala la kuburuzana, hizo ni fikra potofu.

Maaumuzi magumu ambayo si sahihi anaumia mlipa kodi. Kwa nini tufanye maamuzi, kisa tu ni magumu, yamzidishie mzigo mlipa kodi? Hii si sawa.

Hapa issue nikuonyesha msimamo wote kwa wafanyabishara, kumnusuru mkulima then mambo mengine tuta angalia ili kuweza ku recover gharama na kutengeneza margin.

Ni vizuri tuangalie kama tutarudisha gharama na kupata faida kabla ya kuweka msimamo ili mradi "tuwakomoe" wafanyabiashara. Shilingi bilioni 630 si pesa ndogo. Hasara ya shilingi 100 tu kwa kilo ni hasara ya Shilingi bilioni 21. Haihitaji maamuzi magumu na misimamo, inahitaji maarifa na busara zaidi.

I thought you would have raised the issue of budget allocation???

Hatuna bajeti Tanzania. Serikali, muda wowote, inaweza kuamua pesa ziende wapi na zisiende wapi. Hususani, bajeti haijawahi kufikiwa asilimia 60 ya kinachosomwa na kinachofanywa.

Kuongelea bajeti allocation katika mazingira haya ni kupoteza nguvu tu.
 
introvert ,

..kwenye nchi za wenzetu bei inaposhuka na serekali huwa inawasaidia wakulima namna gani?

..je, hutumia utaratibu kama huu anaotumia JPM au huchukua hatua tofauti?

..Zaidi, wakulima wa mazao mengine kama kahawa, pamba, mahindi, etc na wao watasaidiwa ikiwa bei zitaporomoka?

Njia ya kwanza ni kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji. Hili linafanyika kwa kuwapatia ruzuku au kuwapunguzia kodi kwenye inputs za kilimo. Gharama za uzalishaji zikiwa chini hata bei ikishuka basi hasara haiwi kubwa sana.

Upande wa pili, wakulima wanafanya biashara ambayo bei inapanda na kushuka sana. Bei ikipanda kuna faida na bei ikishuka kuna hasara.

Hivyo njia bora ya kukwepa hasara inayofanywa na nchi nyingi ni kuingia mikataba ya kuuza mazao kabla hata hujapanda hayo mazao. Hii inamsaidia mfanyabiashara kudhibiti gharama zake kwa sababu anajua bei atakayouza mapema kabisa.

Mikataba hii inaitwa future and forward contracts na inatumika kwenye bidhaa za kilimo sana. Serikali inaweza kuwasaidia wakulima kwenye hili kwa kuwasaidia kujua bei gani nzuri ya kuuza na pia kuwawekea gurantee kwa wanunuzi.

Mfano, leo hii unaweza kuta kahawa au pamba ambayo itavunwa mwaka 2020 tayari imeshanunuliwa. Lakini anapotokea Waziri na kuzuia export za mazao anaharibu confidence yote kwenye soko kwa hali ya juu na kusababisha hasara kwa wakulima.

Historia imeonyesha pale Serikali inaponunua kwa bei juu zaidi ya bei ya kwenye soko ili kuwafurahisha wakulima (siasa), hasara inapata Serikali (walipa kodi) na si wafanyabiashara.
 
uzalishaji umezidi mahitaji misimu yote miwili, kwa hiyo bei ilikuwa ndogo misimu yote miwili, sasa tofauti ya hiyo misimu miwili ni nini?

unatoa scenario ambayo uzalishaji ni double the levels of mahitaji miaka yote miwili, halafu unasema ni mfano. Don't be silly

Hujaelewa. Rudia kusoma tena. Scenario zote mbili uzalishaji umezidi mahitaji. Lakini msimu unaofuatia uzalishaji unapozidi zaidi mahitaji basi bei inashuka zaidi.
 
Ananunua korosho 3000 anauza 5000.

Ukisoma nashauri kabla ya kununua Serikali ihakikishe inasoko la kuuza kwa bei zaidi ya wanayonunulia. Mpaka sasa, kuna soko hilo?

Ni rahisi kusema unanunua 3,000 unauza 5,000. Ukienda sokoni ukakuta ni 2,700 utafanyaje?
 
Back
Top Bottom