Ushauri: Kitu gani mdogo wangu afanye ili arudi kwenye ndoa yake

Baikije

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
437
498
Huyo Dogo anataka ukimwi ama kitu gani? Maana mwana kashakaa na manzi 6 ndani ya miezi 11 tafsiri yake mwamba ni kitombi ki**nge aachane nae afanye mambo yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,392
2,000
Mwehu alioa dada yako.

Miezi 11 wanawake 6😁 bado dada yako anamzimia?!
Aisee mna matatizo makubwa sana (genetically)
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,257
2,000
Mdogo wangu ni mwajiriwa na amepanga chumba chake kwa sasa na analipa kodi na kujihudumia mwenyewe wala haitaji msaada wa ndugu ila tu anampenda mme wake na hapendi kona wanae wanaishi malezi ya wazazi kutengana, tulishamshauri juu ya kumuacha ila akijaribu ni wiki moja anadai hawezi

Basi mdogo wako labda anahitaji zaidi msaada wa Kiroho na Kisaikolojia kuliko hiyo ndoa ya Kishetani na siajabu hata haelewi maana ya ,,kumpenda mume wake” , ...
 

Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
19,346
2,000
Hebu tujifunze kuheshimu misimamo ya wenzetu!
Mtu mzima akikwambia sikutaki inafaa uelewe na ujiongeze.

Maisha ni mafupi kuishi katika maumivu unayoweza kuyakwepa.
 

fimboyaasali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
2,843
2,000
dada yako aende kanisani walipofunga hiyo ndoa ili watafute suluhu,kama ni mwislamu aende bakwata na iqapo itashindikana happ watapewa barua ya kwenda mahakamani kuivunja hiyo ndoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

ILISACHA

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
294
500
Maelewano yakikosekana kwenye ndoa mpaka ikafikia wanandoa wakatengana, muda wa kutengana usizidi wiki 1 hadi mwezi 1 suluhu iwe ishapatikana zaidi ya hapo kila 1 wa wana ndoa ataanza kuzoea maisha ya upweke huko aliko kiasi cha kuona mwenzie wa kazi gani na maisha yanasonga. (Japo mtoto/watoto wanakosa malezi na upendo wa mzazi 1wapo)

Sasa kila 1 akiikubali hiyo hali ya upweke ni ngumu kurudi muwe pa1 ila 1 akishindwa kuikubali hiyo hali ya upweke ndiye huanza kuitafuta suluhu.

Kwa hiyo mme pengine aliudhiwa kiasi cha kushindwa samehe mke wake ila mke nae si wa kumwamini kirahisi tu umkubalie ombi lake la arudi muishi pa1.

Yawezekana mke kuna sehemu au kuna kitu hajakamilisha kaamua kujirudi ili lengo lake litimie au kweli kapigwa na maisha kaona mwenyewe hawezi kujihudumia kakubali matokeo.

Ushauri wangu waondoe tofauti zao warudiane ila mume atambue kuanzia sasa anaishi na nyoka ndani, saa yo yote anaweza kung'atwa na hiyo nyoka (mke wake)
 

alubati

JF-Expert Member
May 29, 2016
2,858
2,000
Hapana chanzo cha ugomvi ni mwanaume kuchepuka na wakawa hawapatani wanagombana
Sasa basi atakufa ukimwi akirudi,kama ulivyosema ameshapita na wanawake kibao kwa huu muda mfupi wa miezi 11,huwezi jua amejipaka nini kwao,muda mwingine likuepukalo lina kheri.apige moyo konde huyo ndugu yako,asonge mbele,sidhani kama kutakuwa na marlewano hata wakirudiana,labda mwanaume aamue kutulia mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
5,477
2,000
Hakuna tena ndoa hapo.
Yaani nyote nyinyi mnajua huyo mwanaume ni malaya wa kawaida na mkorofi, na ndoa haiwezi. Sasa mnalazimisha mdogo wenu arudiane na huyo mwanaume ili iweje?

Mdogo wako ajitambue sasa, asepe zake akapambana na maisha yake.
Heri nusu shari kuliko shari kamili.
 

Castle_Lite

JF-Expert Member
Sep 10, 2016
547
1,000
Mwanaume Mpumbavu tu.

Mdogo wako kama ana uwezo aombe kukaa na watoto wake,
Aachane na Mwanaume wa namna hiyo,.

Kufunaniwa ufumaniwe alaf ww ndio uwe mgomvi, na hata baada ya kuombwa msamaha bado kichwa ngumu.


Chaaa! Mpumbavu mmoja tu huyo.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,453
2,000
Ndoa hailazimishwi, kwa mujibu wa maelezo yako inaonesha huyo mwanaume ni kit0mbi sana wa wanawake (ndani ya miezi 11 ameshabadili wanawake kibao kama vile anabadili nguo)!

Huyo dada yako asipokuwa na msimamo atauawa kwa aidha magonjwa ya kuambukiza au vinginevyo. Maamuzi ya mwisho yapo mikononi mwa mwanamke na mwanaume
hii sidhani kama ni kweli, amesema hakujua hata mmewe yuko wapi, hao wanawake aliwajuaje?
 

naiman64

JF-Expert Member
Nov 22, 2013
5,433
2,000
Hapana chanzo cha ugomvi ni mwanaume kuchepuka na wakawa hawapatani wanagombana
Hebu kaa na nduguyo mweleze Kwa upole kwamba maisha ni popote atulie asiendelee kumuwaza huyu jamaa aaangalie maisha yake, Asim bembeleze hata akirudishwa bado Ile tabia hatoiacha na dharau itaongezeka, atafute.mtu mwenye uhakika awe naye maisha yaendelee. kama kweli mnampenda ndugu yenu, Sisi tulimchekea wetu sasa hivi hazimo kabisa Hana anachowaza zaidi ya huyu me na huyo jamaa kisha fariki zamani tatizo hajawahi kuwa na me mwingine zaidi ya huyo mumewe, walikutana shule walipomaliza tu akaolewa, hakukata tamaa ndugu yetu, jamaa anamtishia kumuua anamletea wanawake yeye katulia tu, sina cha kueleza kuhusu ndugu yetu yote umeleza wewe hakuna kasoro, haraka kaa naye mweleze ukweli na nyie msimpe moyo kuhusu huyo me mkatisheni tamaa ajijue hana mume.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

MCHEZA KAMARI

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
580
1,000
Heb tueleze chanzo cha kuachana kwao Ni nn? Naamin chanzo haiwez kuwa kuzidisha chumv kwenye mboga hapo kuna tatzo tu either mdogo wako alichepuka

Sent using Gun Trigger
 

sjosh4

JF-Expert Member
Apr 10, 2020
646
1,000
Habari wadau,

Poleni na mihangaiko ya kila siku na pia endeleeni kuchukua tahadhali maana Corona bado ipo

Niende kwenye mada mdogo wangu alifunga ndoa na mmewe na kupata watoto wawili lakini ndoa yao ilikuwa ya misukosuko ya magomvi kama mjuavyo ndoa zilivyo na changamoto

Ikafikia hatua mwanaume akachukua maamuzi ya kumuacha mkewe na kukata kabisa mawasiliano na mkewe hata mwanamke akawa hajui mmewe anaishi wapi maana aliondoka nyumbani na watoto tu na kumuacha bila kumuaga.

Basi ikawa ndugu jamaa na marafiki wakijaribu kuongea na wote wawili mwanaume anajibu hataki kusikia habari za mwanamke yule, mpaka ikapita miezi 11 mwanaume akawa na mwanamke mwingine lakini alikaa nae wiki 3 wakaachana akachukua mwingine hivyo hivyo kifupi ndani ya miezi 11 kashaishi na wanawake 6 na wote kaachana nao

Baada ya hapo mdogo wangu alianza kumtafuta kwa njia ya simu na akaanza kupokea (kipindi cha nyuma alikuwa hapokei simu kabisa wala kuongea nae na akipigiwa simu kwa namba ngeni akijua ni mdogo wangu alikuwa anakata na kublock namba) ila kwa sasa anapokea na kuongea nae hata akimtumia wasap meseji anajibu japo kwa kuchelewa ila anajibu.

Akiulizwa kuhusu swala la ndoa yao au kumacha kwa talaka anajibu hayuko tayari kutoa majibu apewe muda ajitafakari, mdogo wangu anampenda sana mme wake ila ndio mme hataki suluhu na kwa sasa mdogowangu amekuwa akimtumia msj za kuomba msamaha ila mwanaume anajibu muda bado wa kuzugumza.

Kwa upande wa ndugu wa mme wanampenda mdogo wangu na hata alipoachika walisema hawatakanyaga kwa shemeji akiwa na wanawake hao wengine wao wanamtambua mdogo wangu.

Kufupisha je, bado kuna uwezekano wa ndoa hii kuokolewa au mdogo wangu nae aamue maisha mengine, maana mwanaume anasema yeye kwa sasa haishi na mwanamke ila anataka kutulia ndio anamjibu mdogo wangu hivyo anamwambia asifikiri kuwa anaishi na mwanamke hapana, ila anataka muda wa kufikiria na imepita miezi 11.

Ushauri wenu muhimu sana.

Nyongeza ndoa ni ya kanisani
Kwanini walitengana, tupo source kwanza,
Au alichepuka
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,857
2,000
HUYO "MDOGO WAKO" NDIO WEWE KUMBE?? HALAFU UNATUPANGA HAPA:D:D:D

ILA MKUU TUKIACHA UTANI KIDOGO, CHANZO CHA MUME KUHAMA NA KUTOKOMEA HUKO MBALI NI NINI? KUNA KITU HUJATUWEKA WAZI NAHISI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom