Kilimo bora cha Mananasi: Uandaaji wa shamba, upandaji, utunzaji wa mimea na uvunaji wa mananasi

Nawashauri mjifunze elimu mbalimbali za ujasiliamali za usindikaji na utengenezaji wa bidhaa kutokana na kilimo hicho kisha muandae mchanganuo mzuri wa investment hiyo then mnaweza kwenda bank kuombea mkopo mradi huo na kuanzisha kiwanda chenu kidogo cha kutengeneza bidhaa mbalimbali kuokana na kilimo hicho kama wanavyofanya hao mnaowauzia, then kwa upande mwingine ningewashauri mtafute kijiofisi maeneo ya mjini kisha muwaajiri watu waliobobea katika taaluma ya masoko ili kuwatafutia masoko ya bidhaa zenu kutokana na kilimo hicho, mfano mnaweza kuuza katika migahawa, mahoteli, majumbani, supermarkets na kusafirisha mikoani na nchi za jirani endapo mtajipanga kiofisi zaidi kama kampuni. Mwisho nawashauri vijana hasa mliomaliza chuo na mliosomea taaluma za masoko na ICT muweze kuwasaidia wakulima wetu hapa nchini ambao hawana elimu ya kutosha kuhusu kutafuta na kumudu masoko ya mazao yanayotokana na kilimo chao kwa kuandaa semina za kuwaelimisha, kufanya biashara ya kuwatafutia masoko wakulima kama wanavyofanya madalali wa bidhaa nyingine kama magari, nyumba , viwanja nk.

Nawasilisha.
 
Kiwanda cha coca cola wameanzisha kitengo cha kusindika matunda jaribu kuwaona kiwandani Mikocheni.
 
kuna kipindi kuna juice za mananasi kutoka zambia zilikuwa zinauzwa kwa wingi hapa Dar es salaam katika kufatilia niligundua zilikuwa zinatengenezwa toka kiwanda kidogo tu ambacho teknologia yake ni rahisi ningeshauri mkaangalia na namna ya kusindika mananasi ili kupata juice ili muongeze thamani ya mazao yenu
 
nenda kwenye kiwanda cha bakheresa pale vikindu kajenga kiwanda kwa ajili yenu tena kuna kipindi alikuwa anatafuta mashamba makubwa kuanzia heka 5 ili aingie nao mkataba wa uvunaji mananasi. big up mkuu.
 
think of processing pineapple pulp ..... hii ni raw material ya kutengenezea juice ya nanasi ..... hii inaweza kuwa processed wakati wa msimu wa nanasi na kuihifadhi kwenye matanki makubwa kwa muda mrefu na kuiuza kadiri ya mahitaji ya soko lako
 
Mkuu Hongeleni sana Kwa kilimo Kwanza,

Mkuu mimi nianze kwa kuwalaumi nyie/wewe kwa kuingia shambani kulima bila kujua utamzia nani, hili ndo Tatizo la wakulima wengi sana Tanzania, tunasukumwa kulima kitufulani na bei na sio soko, Bei ya Nyanya ikiwa juu kila mtu anataka alime bila kujalisha atamzia nani,

Matokeo ya kulima bila kujua utamzuia nani ndo haya ya madalali kuneemeka na product zako, na tumeshindwa kupiga hatua kwa sababu hizi za kulima kwa kusikia kwa wenzetu,

Mkuu ni lazima mbadilike, make wakati wa sasa sio wa miaka ya 90, kilimo ni biashara kama ilivyo biashara nyingine so ni lazima kabla ya kulima ujiridhishe kwamba umepata soko la uhakika la mazao yako, ni lazima ufanye Tafiti kwanza, ni lazima uje ni nani atakuwa consumer wako na kwa nini,

Tunaingia kilima na kuguga bila kwanza kufanya tafiti za masoko matokeo yake ni either mazo kuozea shambani, au mfugaji kuishia kumwaga maziwa chini, Na hata hayo mananasi it means usipo pata soko yataozea shambani au utakuja kuuza kwa hasara, na hapo utaanza kuilaumu serikali hijatafuta soko la mananasi,

Mkuu hakikisha mnafanya tafiti za kutosha za

1, Nani atanunua mazao yenu

2. Kwa kiwango gani atanunua

3. Kwa bei gani atanunua

4. Kwa mashariti yapi,

Inakuwa inashangaza hata wafugaji mtu akisha fuga kuku na kutaga mayai ndo anaanza kutafuta soko lakini wakati hajaanza kufuga hakutafuta soko,

NA MWISHO KAMA MNAONA SOKO LA MOJA KWA MOJA NI TATIZO BASI MNAWEZA NYIE WENYEWE KUONGEZEA THAMANI HAYO MANANASI YENU NA KUUZA EITHER JUICE YAKE AU HATA KUYAKAUSHA NA KUYAPAKI KWENYE PAKITI

mkuu sidhani kama una haja ya kulaumu sana...kwa uzoefu wangu naona jamaa amefanya vizuri sana kwa sababu kuna watu wanakuwa na bussiness plan nzuri lakini bila kuwa na uzoefu walau huyu jamaa ameshaanza na ameishapata uzoefu ndo sasa anataka kupanuka zaidi na kabla ya kufanya hivyo ndo maana anatafuta ushauri wa jinsi ya kuboresha ingekuwa vigumu sana kwakwe kuja na mawazo ya nini afanye kupanua shamba kama asingekuwa amepata uzoefu. Kwa uzoefu wangu ni vizuri uwe umeanza unapata uzoefu na kujifunza mambo muhimu katika kilimo cha nanasi hasa changamoto, utunzaji ikiwa ni pamoja na palizi na mengine...

Kuna wengine wanataka kufanya kilimo kwa njia ya mtandao, kwenye computer (excellent bussiness plan on papers) na kwa njia ya simu...hii haiwezekani kabisa na utachemsha...na kwa jinsi ninavyojua kilimo cha nanasi uwezi kukosa soko kabisa.

Kwa hiyo badala ya kulaumu ungempatia ushauri...lakini kama haujajihusisha na ukulima wa zao ili au jingine sidhani kama ushauri wako utasaidia...maana nimeona kuna watu wengine ni wazuri sana kuandika ushauri mzuri tu kumbe hawajawahi fanya kilimo hata cha robo eka.
 
kuna kiwanda muleba,kagera kinatengeza soda za mananasi kinaitwa Mali,namba za simu ni 0754 758818 apo lazima utapa soko mkuu,nakutakia mafanikio mema
 
Naombeni msaada kwa yeyote mwenye ujuzi wa kilimo cha mananasi! Nataka kupanda mananasi eneo la Bupu - Mkuranga je,
1. Itanigharimu muda gani na kiasi gani kuitunza hadi ikue na kufikia mauzo?
2. Shamba ninalo ekari 4 je kwa wastani nitahitaji miche mingapi?
3. Mbegu nzuri zake zinapatikana wapi zaidi?
4. Soko la mananasi kwa sasa?
5. Angalau kwa kiwango cha chini nanasi moja naweza kuiuza kwa shliingi ngapi??
Asanteni wapendwa!
 
Naombeni msaada kwa yeyote mwenye ujuzi wa kilimo cha mananasi! Nataka kupanda mananasi eneo la Bupu - Mkuranga je,
1. Itanigharimu muda gani na kiasi gani kuitunza hadi ikue na kufikia mauzo?
2. Shamba ninalo ekari 4 je kwa wastani nitahitaji miche mingapi?
3. Mbegu nzuri zake zinapatikana wapi zaidi?
4. Soko la mananasi kwa sasa?
5. Angalau kwa kiwango cha chini nanasi moja naweza kuiuza kwa shliingi ngapi??
Asanteni wapendwa!



Nitakujibu kama nijuavyo mimi (ila mimi sio mtaalamu ila nina experience)

1. Itakuchukua muda wa miaka 2 hadi mavuno
2. Kila ekari unahitaji miche 10,000 hadi 15,000
3. Mbegu nzuri - ni PM nitakuuzia
4. Soko - bei ya shambani - kama kubwa 1,000 dogo 500

Mungu akubarikis ana kwa kuchagua kilimo hiki - ni kizuri - mradi utumie mbolea - na utakapovuna WEWE utauza NANASI na MBEGU pia
Usikate tamaa kusubiri 2 years kabla ya kuanza kuuza

Soko - Kwa Bakhresa, Mahotelini, Masokoni na Mtaani pia.
 
Kwa ekari moja kwa hesabu za hapo juu inaonyesha unaweza kupata sio chini ya 5M ukiwa na ekari 10 unapata 50M
Duuuuu,sidhani kama hizi hesabu zipo realistic but all in all nisikukatishe tamaa just try but I'm sure kinalipa tu hicho kilimo
 
Nimenunua shamba la heka 16 katika kijii cha mkenge bagamoyo. lengo ni kuanza mradi wa kilimo cha nanasi nataka kuonana na wataalamu kwaajili ya kunishauri. kwa hapa Dar es salaam naweza kuwapata wapi???
 
Kwa ekari moja kwa hesabu za hapo juu inaonyesha unaweza kupata sio chini ya 5M ukiwa na ekari 10 unapata 50M
Duuuuu,sidhani kama hizi hesabu zipo realistic but all in all nisikukatishe tamaa just try but I'm sure kinalipa tu hicho kilimo

Mkuu tena hiyo hesabu iko chini. Nimesoma article moja yeye anasema unaweza kupanda miche Hadi 25,200 Kwa ekari which means ni mara mbili ya mahesabu ya huyu. Inaonyesha kilimo cha nanasi kinalipa. Nami naenda kulima aiseee. KILIMO BORA CHA MANANASI



Zao la mananasi hulimwa sana hapa nchini maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Geita, Mwanza, Tanga, Mtwara, Lindi na maeneo mengine. Zao hili lina kiasi kikubwa cha vitamini A na B na kiasi kidogo cha vitamini C, pia kuna madini kama potasiam, kalsiam, chuma na magnesiam

HALI YA HEWA
Manansi hustawi sana ukanda wa pwani usawa usiozini mita 900 toka usawa wa bahari ambapo kuna mvua nyingi kiasi cha milimita 1500 na unyevu wa kutosha, pia unaweza kupanda kwenye maeneo yenye mvua chache lakini kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, Hali ya joto ni kuanzia sentigredi 15 - 32, huwa haya stahimili baridi

UDONGO
Udongo wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji ndi unaofaa kwa ajili ya kilimo cha mananasi, unaweza kutumia samadi au mbole vunde ili kuongezea rutuba ya udongo wako.

MSIMU
Kwa ukanda wa pwani wenye mvua mbili kwa mwaka upandaji wa mananasi huanza mara baada ya mvua za kwanza kuanza, ni vizuri kupanda kwa muda mfupi ili uzaaji usipishane sana na pia kusaidia kupata mvua za kutosha kabla ya msimu kuisha.

UPANDAJI
Tumia miche ya aina moja na yenye umri sawa ili huduma zifanane na pia uzaaji uwe wa mpangilio, umbali toka mmea hadi mmea ni sentimeta 30 na mstari hadi mstari ni sentimeta 60, na umbali kila baada ya mistari miwili miwili ni sentimeta 90

Kwa ekari moja unaweza kupanda miche 25,200 na kwa hekta moja unaweza kupanda miche 44,000. ili mananasi yako yastawi vizuri basi tengeneza kama mtaro mdogo na kwenye mitaro ndio upande mananasi yako, hii husaidia kupata unyevu zaidi

MBOLEA
Kwa wale wanaotumia mbolea za viwandani, ni vizuri kutumia NPK na DAP ambazo utaweka miezi miwili baada ya kupanda na miezi 12 baada ya kupanda baada ya hapo hautahitaji mbolea tena, lakini ni vizuri zaidi kama utatumia mbolea za asili

WADUDU
Wadudu wanaoshambulia mananasi ni aina ya mealybug ambao huondolewa kwa kupulizia dawa kama dume na karate.

Ugonjwa wa kuoza moyo wa miche unaweza kuzuiwa kwa kupiga dawa za copper oxychloride au kwa kuzamisha miche kwenye dawa za fungasi (fungicides)kabla ya kupandwa shambani

UVUNAJI
Mananasi huwa tayari kuvunwa miezi 18 mpaka 24 baada ya kupandwa kutegemeana na mbegu na matunzo ikiwemo kiasi cha mvua, mbolea na unyevu shambani, Uvunaji hufanyika kwa kutumia visu na vibebeo maalum kuhakikisha ubora wa zao hili
 
Smahanimi kwa kuwahamisha kidogo kweli nanasi inalipa mf.huku kigoma lejaleja ni Tsh1000 je mtu akiwa na ekali zake 4,anaweza pata kama 4500000x2x4=36,000,000/= kama faida,sasa vp mimi nae nataka kulima TIKITI MAJI je,nitapata wapi soko la uhakika hasa kwa wasindikaji? ili wanipe tenda ya kuwapelekea mzigo? naomba musaada wenu dawati la masoko na mawasiliano ikiwezekana.
 
Ukitaka kulima kilimo cha kibiashara ni muhimu kwanza kuangalia soko linataka bidhaa ya aina gani na kiasi gani. Soko rahisi na la haraka ni hapo Middle east lakini pia ni lazima uwe tayari kuwekeza vya kutosha.
 
Tatizo mkiotea deal au kupoteza malengo hamleti feedback... mwalwisi Ngongo , tunaomba mrejesho
 
Last edited by a moderator:
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom