Kilimo bora cha Mananasi: Uandaaji wa shamba, upandaji, utunzaji wa mimea na uvunaji wa mananasi

Nimeipanda hii Januari. Ekari moja inatafuna miche 14,000 nami nimepanda ekari 20. Kuna suala la mbolea na upaliliaji pamoja na kushed jua wakati wa kiangazi. Hopefully ntavuna around July 2013. Nanasi moja kwa sasa ni TZS 300 likiwa shambani au unaweza kuuza eka moja 3,000,000
mkuu lete mrejesho
 
Wana JF.

Naombeni mnifahamishe kilimo cha mananasi ni utaratibu unaotakiwa kufuatwa naombe mwogozo wenu wakulima.

Nanasi inavunwa kwa muda gani na kuna mbegu za aina ngapi.

Shukurani.
 
kuna kipindi kuna juice za mananasi kutoka zambia zilikuwa zinauzwa kwa wingi hapa Dar es salaam katika kufatilia niligundua zilikuwa zinatengenezwa toka kiwanda kidogo tu ambacho teknologia yake ni rahisi ningeshauri mkaangalia na namna ya kusindika mananasi ili kupata juice ili muongeze thamani ya mazao yenu

hiii nchi yetu tupo nyuma sana tuna utajiri wa kila kitu lakini tunazidi kuwa masikini .kama suala la mananasi watu wanalima wengi bora liende hawatilii mkazo sababu ya hilo soko lake ni magumashi lakini walaji ni wengi na wanayahitaji sana nchi za wenzetu wanahitaji sana matunda.

uzalishaji wetu ungekuwa kwa wingi naninaona kitu cha msingi ni kufikilia kwanza kujenga viwanda vidogo vidogo vya kusindika mazao yetu wenyewe na baada ya hapo hakika wakulima wengi watavutika sana kulima.
maana kwakuwa kiwanda cha kusindika kipo juu ya utauza wapi au mazao yataharibika itakuwa haina shida kwa kuwa pakuyapeleka papo.

na vile vile wale wenye utaalam wa masoko pia nao wawe mchaka mchaka kutafuta wanunuzi ndani na nje ya nchi hasa ili kuinua uchumi wetu wasiishie kuwaa madalali wa wakulima wetu tuuu.

leo hii tanga wanalima sana machungwa na maembe lkn hakuna hata.kiwanda cha kusindika machungwa na maembe huko sasa hiyo sihatari kweli.mwisho wa siku yanaoza tuu
 
Matokeo mazuri utayapata ukipanda kwa matuta. Matuta yanakuwa na udongo mwingi uliotifuliwa hivyo hurahisisha mizizi ya muhogo (ambayo ndo mihogo yenyewe) kupenya kwa urahisi na kutafuta chakula ardhini, tofauti na yule atakayetumia kilimo cha sesa ambacho huifanya mizizi ifike kwenye ardhi ngumu haraka na hivyo kusababisha mzizi kudumaa. Hivyo muhogo utakaotoka kwenye kilimo cha matuta utakuwa muhogo ulioshiba. Faida nyingine pia matuta yanahifadhi maji kwa muda mrefu tofauti na Sesa.

Hivyo ndugu nakushauri utumie kilimo cha Matuta. Katika kutumia Cuttings ni vizuri ukitumia ndefu kama futi moja hivi au sm 30 na uchomeke kiasi cha sm 15 ardhini kwa kuulaza katika pembe ya nyuzi 45. Ni vizuri kupanda mihogo mara tu mvua zinapoanza hasa kwa maeneo yenyewe mvua za taabu hii itasaidia mihogo kushika vizuri ardhini na hivyo kuweza kushindana na jua mara msimu wa mvua unapoisha. Maana itakuwa imeshakuwa na mizizi mingi na yakutosha kuutafutia mmea chakula na maji ardhini.

Utapata na kwa wengine.

Dah! Mkuu umenikumbusha mbali sana.O'level Kwamkoro Secondary.Style hiyo ya kulima matuta ndiyo tuliyokuwa tunatumia.
 
Mtaalam nanasi zinazolimwa pwani zinatoka november-December na May-June baada ya miezi hiyo zinaadimika kabisa sokoni, ukiipata nanasi utaambiwa inatoka Geita..
Wazo langu: Ninahisi inakua hivyo kwa sababu zifuatazo
1. Kwa sababu wakulima wengi mkoa wa pwani hupanda nanasi December-January na june-July kwa sababu ndo kipindi ambacho mbegu hupatikana, kutokana na maelezo yako kwamba nanasi huvunwa baada ya miezi 18 hivyo ni lazima watu hawa wavune kipindi hicho.
2. Baada ya mchumo wa kwanza Nanasi huvunwa kila baada ya miezi sita na ili iweze kuzaa inahitaji mvua/ maji(ubichi) hivyo haiwezi kuzaa kipindi cha August to october kwa sababu ya ukame.
Swali: Nikijarib kukwepa kipindi hiki kwa kubadili miezi ya kupanda na kufanya umwagiliaji inawezekana?
 
Mtaalam nanasi zinazolimwa pwani zinatoka november-December na May-June baada ya miezi hiyo zinaadimika kabisa sokoni, ukiipata nanasi utaambiwa inatoka Geita..
Wazo langu: Ninahisi inakua hivyo kwa sababu zifuatazo
1. Kwa sababu wakulima wengi mkoa wa pwani hupanda nanasi December-January na june-July kwa sababu ndo kipindi ambacho mbegu hupatikana, kutokana na maelezo yako kwamba nanasi huvunwa baada ya miezi 18 hivyo ni lazima watu hawa wavune kipindi hicho.
2. Baada ya mchumo wa kwanza Nanasi huvunwa kila baada ya miezi sita na ili iweze kuzaa inahitaji mvua/ maji(ubichi) hivyo haiwezi kuzaa kipindi cha August to october kwa sababu ya ukame.
Swali: Nikijarib kukwepa kipindi hiki kwa kubadili miezi ya kupanda na kufanya umwagiliaji inawezekana?
Hivi mkuu nanasi halinyeshewi kama hamna mvua?
 
Kwa sasa nakamilisha banda la kufugia mbuzi wa maziwa na wanaozaa pacha,kama likikamilika kabla ya desemba hii wale mbuzi huwakuti,nimepita novemba na nikawaona wako vizuri. Hata kama nikiwalamba wote nitakuuzia mbegu.

Hivi inawezekana ukaanzisha ufugaji wa mbuzi wa nyama kwa large scale?

Masoko ya uhakika yapo?
 
Ukitaka kulima kilimo cha kibiashara ni muhimu kwanza kuangalia soko linataka bidhaa ya aina gani na kiasi gani. Soko rahisi na la haraka ni hapo Middle east lakini pia ni lazima uwe tayari kuwekeza vya kutosha.

Una connection na wateja wa middle east?
 
Kuna jamaa alitoa mchanganuo wake mwaka 2016 hebu soma kidogo
gharama zitakuwa hivi:

ununuzi wa ardhi kwa Tsh. 300,000-- (ekari ni hatua 70x70)
utayarishaji wa shamba Tsh 150,000/=
gharama ya miche na upandaji miche 15,000 kwa ekari Tsh 750,000 (i.e.50 x 15,000 ikijumuisha ununuzi wa mbegu na upandaji),
Mbolea 100,000.
matumizi mengine 200,000 (ikiwa ni pamoja ni vibarua, na kuleta mzigo sokoni).
jumla 1,500,000/-


Mapato
nanasi unavuna baada ya miezi 18. kwa hesabu za chini kabisa unauza nanasi moja kwa Tsh 500 na assume unapata nanasi 12,000 utapata Tsh 6,000,000/=. (assumption ni kuwa si rahisi kupata mavuno 100%- bali inaweza kuwa 80%)

Faida :
ukiondoa matumizi (Tsh 1,500,000) unapata faida 4,500,000 ukiwa na ekari tano bila shaka utapata zaidi ya milioni 20 (na hapo hujaweka economy of scale). --though unaweza kupunguza au kuongeza asilimia fulani kutegemeana na risks zilizopo na uzoefu wako katika kusimamia na kutafuta masoko..

soko likoje
Kuna atakayeuliza je soko lipo-- mimi nasema soko lipo huko huko shamba au unaleta kwa BAKHRESA anayenunua matunda kwa ajili ya kutengeneza natural juice i.e. azam box juice). nasikia kuna kiwanda kingine kinaanzishwa bagamoyo (siyo bakhresa). ila tukumbuke kwa sasa ambapo nanasi ni chache ukienda sokoni huwezi pata nanasi chini ya 1,500/-
 
Kiutaalamu fuata muongozo huu

UESDAY, JULY 30, 2013
KILIMO BORA CHA MANANASI
Zao la mananasi hulimwa sana hapa nchini maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Geita, Mwanza, Tanga, Mtwara, Lindi na maeneo mengine. Zao hili lina kiasi kikubwa cha vitamini A na B na kiasi kidogo cha vitamini C, pia kuna madini kama potasiam, kalsiam, chuma na magnesiam


HALI YA HEWA
Manansi hustawi sana ukanda wa pwani usawa usiozini mita 900 toka usawa wa bahari ambapo kuna mvua nyingi kiasi cha milimita 1500 na unyevu wa kutosha, pia unaweza kupanda kwenye maeneo yenye mvua chache lakini kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, Hali ya joto ni kuanzia sentigredi 15 - 32, huwa haya stahimili baridi

UDONGO
Udongo wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji ndi unaofaa kwa ajili ya kilimo cha mananasi, unaweza kutumia samadi au mbole vunde ili kuongezea rutuba ya udongo wako.

MSIMU
Kwa ukanda wa pwani wenye mvua mbili kwa mwaka upandaji wa mananasi huanza mara baada ya mvua za kwanza kuanza, ni vizuri kupanda kwa muda mfupi ili uzaaji usipishane sana na pia kusaidia kupata mvua za kutosha kabla ya msimu kuisha.

UPANDAJI
Tumia miche ya aina moja na yenye umri sawa ili huduma zifanane na pia uzaaji uwe wa mpangilio, umbali toka mmea hadi mmea ni sentimeta 30 na mstari hadi mstari ni sentimeta 60, na umbali kila baada ya mistari miwili miwili ni sentimeta 90


Kwa ekari moja unaweza kupanda miche 25,200 na kwa hekta moja unaweza kupanda miche 44,000. ili mananasi yako yastawi vizuri basi tengeneza kama mtaro mdogo na kwenye mitaro ndio upande mananasi yako, hii husaidia kupata unyevu zaidi

MBOLEA
Kwa wale wanaotumia mbolea za viwandani, ni vizuri kutumia NPK na DAP ambazo utaweka miezi miwili baada ya kupanda na miezi 12 baada ya kupanda baada ya hapo hautahitaji mbolea tena, lakini ni vizuri zaidi kama utatumia mbolea za asili

WADUDU
Wadudu wanaoshambulia mananasi ni aina ya mealybug ambao huondolewa kwa kupulizia dawa kama dume na karate.


Ugonjwa wa kuoza moyo wa miche unaweza kuzuiwa kwa kupiga dawa za copper oxychloride au kwa kuzamisha miche kwenye dawa za fungasi (fungicides)kabla ya kupandwa shambani

UVUNAJI
Mananasi huwa tayari kuvunwa miezi 18 mpaka 24 baada ya kupandwa kutegemeana na mbegu na matunzo ikiwemo kiasi cha mvua, mbolea na unyevu shambani, Uvunaji hufanyika kwa kutumia visu na vibebeo maalum kuhakikisha ubora wa zao hili.
Kwa taarifa zaidi tembelea mitiki.blogsports.com
 
Jana niliwasilisha mkusanyiko wa mada zinazohusu ufugaji wa kuku..

Leo naomba niweke mkusanyiko wa mada za kilimo.. nimeamua kufanya hivi ili kusaidia wale ambao ni wanachama wapya na wanachama wengine ambao wanataka kujikumbusha mada hizo na kuchukua hatua:



ARDHI
  1. Ardhi ya kilimo: Ardhi ya kilimo
  2. Ardhi ya kilimo!!! Natafuta ardhi ya kilimo ya bei nafuu
  3. Shamba kwa ajili ya kilimo Shamba kwa ajili ya kilimo
  4. Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga
  5. Ardhi kwa Kilimo cha Kitunguu Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na masoko
MAZAO
  1. Mazao gani yanafaa kwa kilimo chalinze? Part 1 Mazao gani yanafaa kwa kilimo chalinze?
  2. Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze? Part 2 Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze?
  3. Kilimo cha Mitiki: Utaalamu Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe
MIKAKATI KATIKA KILIMO
  1. kilimo-wakulima wa jf getting together Wakulima wa JF getting-together
  2. Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali? Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali?
  3. Power tiller na dhana ya kilimo kwanza Power tiller na dhana ya kilimo kwanza
  4. Kwanza Kilimo? https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/31557-kwanza-kilimo.html
  5. Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo... Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo...
haya ndo nimeweza kukusanya kwa leo.. hopefully hii itasaidia kutoa mwanga kwa wale wanaotaka kuperuzi posts mbalimbali..


tukumbuke!! TUKIWEKA JITIHADA.. KILIMO KINALIPA!!.nawapeni mfano: unaenda Kiwangwa bagamoyo unanunua ekari moja ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha nanasi.



Gharama zitakuwa hivi:
  1. ununuzi wa ardhi kwa Tsh. 300,000-- (ekari ni hatua 70x70)
  2. utayarishaji wa shamba Tsh 150,000/=
  3. gharama ya miche na upandaji miche 15,000 kwa ekari Tsh 750,000 (i.e.50 x 15,000 ikijumuisha ununuzi wa mbegu na upandaji),
  4. Mbolea 100,000.
  5. matumizi mengine 200,000 (ikiwa ni pamoja ni vibarua, na kuleta mzigo sokoni).
  6. jumla 1,500,000/-
Mapato
nanasi unavuna baada ya miezi 18. kwa hesabu za chini kabisa unauza nanasi moja kwa Tsh 500 na assume unapata nanasi 12,000 utapata Tsh 6,000,000/=. (assumption ni kuwa si rahisi kupata mavuno 100%- bali inaweza kuwa 80%)

Faida :
ukiondoa matumizi (Tsh 1,500,000) unapata faida 4,500,000 ukiwa na ekari tano bila shaka utapata zaidi ya milioni 20 (na hapo hujaweka economy of scale). --though unaweza kupunguza au kuongeza asilimia fulani kutegemeana na risks zilizopo na uzoefu wako katika kusimamia na kutafuta masoko..

soko likoje
Kuna atakayeuliza je soko lipo-- mimi nasema soko lipo huko huko shamba au unaleta kwa BAKHRESA anayenunua matunda kwa ajili ya kutengeneza natural juice i.e. azam box juice). nasikia kuna kiwanda kingine kinaanzishwa bagamoyo (siyo bakhresa). ila tukumbuke kwa sasa ambapo nanasi ni chache ukienda sokoni huwezi pata nanasi chini ya 1,500/-

Mfano hai
Kamuulize ndugu Eric Shigongo mambo anayofanya Kiwangwa na anapata nini?-

Mwenye taarifa zaidi au anayetaka kukosoa ni vema amwage hapa..

Mkuu Malila upo?

Mkuu uhali gani bana. Asante sana kwa kuanzisha hii kitu juu ya suala la kilimo ila nimesikitishwa sana kuona kuwa washiriki wa mada hii muhimu inayoweza kuwatoa watu kwenye umasikini ni mdogo sana ukilinganisha na watu wanavyochangia mada za kijinga kwa wingi wao. Sasa ingawa ni mada ya muda mrefu ila ipo na itaendelea kuwa valid siku zote.

Mimi binafsi ni mtoto wa Mkulima na ninapenda kilimo na nimeamua kuanza kilimo. Kwakuwa nafanyakazi nje ya nchi nikiwa narudi nyumbani mara kwa mara nikaamua nianze na kilimo ambacho hakitaniumiza kichwa sana hususan juu ya kuibiwa au kusimamiwa vizuri hivyo nikaamua nianze kidogo na mazao ambaya hayahitaji usimamizi wa karibu sana wa kila siku na mazao yanayostahamili maradhi na ukame kidogo.

1). Nimeanza na miwa huko Kilombero. Nimelima takribani hekari 20 za miwa. Sina usumbufu kwenye hili kwakuwa gharama za kila kitu katika kuzihudumia zinafahamika. Nasoko lake ni Kilombero sugar na bei inafahamika hivyo sina haja ya siku zote kuwepo kwenye field. Natembelea mara chache na ninahakikisha wakati nina family member hasa huwa wife wakati wa kunyunyuzia dawa, kuweka mbolea na kukata miwa otherwise kijana wangu wa shamba anasimamia kazi zingine zote. Angalizi, ni ukweli kuwa uingizaji horera wa sukari toka nje kulituathiri sana na nilishindwa kuuza miwa yangu kwa miaka miwili mfululizo, nilipata hasara. Ninaimani kwa sasa kwa uongozi huu mpya huenda mambo yakawa safi kwa sisi wakulima. Kilimo cha miwa kama utauza kila mwaka ni kilimo kizuri sana na kina lipa kwakuwa gharama kubwa ni mwaka wa kwanza tu kwakuwa ukishapanda unaendelea kukata miwa kila mwaka kwa muda si wa chini ya miaka mitano mfululizo kutegemea na matunzo ya shamba. Agalizi hapa ni kuwa makato wakati wa kuuza kiwandani ni mengi sana kwa kiwanda, Serikali na vyama vya ushirika wa kilimo unakuta zaid ya 40% ya mauzo inakwenda huko, ni suala la kuangaliwa. Vilevile Kiwanda kinatakiwa kutoa kilimo cha mkataba such that kama miwa yangu haivunwi kwa mwaka mmoja au miwili vipi kuhusu gharama nilizoziingia? Vilevile vyama vile havina wasomi kabisa na hasa wanasheria wa kutetea maslahi ya wafanyakazi, haiwezekani kwenye business kubwa kama ile ikafanyika kienyeji hivyo, ingefaa chombo kinachohusika na masuala ya kilimo kuangalia jinsi gani ya kusaidia wakulima masikini wa Kitanzania ambao wengi kutokana na ujinga wa kutokwenda shule hawajui mambo mengi ya msingi ya haki zao. Niishie hapa juu ya kilimo cha miwa.

2). Kilimo cha mananasi. Najaribu kulima mananasi. Miaka mitatu iliyopita nilinunua hekari tani katika kijiji cha Mwavi huko Kiwangwa Bagamoyo. Nililima mananasi kwa majaribio na niligundua kuwa kilimo hiki kikilimwa kwa umakini wake na kupata soko la uhakika watu wanaweza kabisa kuachana na umasikini. Faida uliyoielezea si kitendawili baili ni kweli. Nililima hekari chache tano ili kutafiti na nilipata vilevile bahati ya kutembelea shamba la Shigogo na nilinunua mbegu toka kwake na kujifunza na nilielimika sana na kushawishika kuwekeza zaidi. Januari mwaka Jana nilinunua virgin land yenye ukubwa wa hekari 60, kilomita 6 toka barabara kubwa ya lami (Bagamoyo-Msata) kuelekea Mkenge. Nilijipinda kufyka, kung'oa visiki, kulima na hatimae kupanda hekari 25. Hivi ninavyosema nimetoka Bongo juzi na nimemaliza kuweka mbolea shamba zima baada ya kwisha kwa mvua. Ni uwekezaji mkubwa kwa kiwango cha umaskini wa sisi Watanzania. Na kwasasa nimeweza kumaliza awamu nyingine ya kusafisha sehemu ya shamba iliyobaki (hekari 35) zote zimeng'olewa visiki na shamba lipo jeupe, kinachoendelea ni shughuli za kuchoma mkaa katika kulisafisha maana kuna miti mingi sana na baada ya hapo ni kuingiza trekta. Ila bado sijapanga nilime nini, nataka nitembelewe na wataalam wa kilimo kwa ushauri kabla sijaanaza uwekezaji wa ziada.

Ila kwakweli nimelima mananasi na kama watu wengine nimelima bila kufanya utafiti mkubwa sana juu ya masoko makubwa na mapana ya mananasi na hii ni kwasababu nafanyakazi nje ya nchi na muda wangu ni mfupi sana wa kufuatilia mambo haya kwa kina. Lakini nikaona siwezi kusubiri hilo wakati nina ardhi nikaona nifanyekitu na mambo mengine yatakuja baade na wakati naendelea kulihidumia shamba nitakuwa nikiendelea kutafuta taarifa juu ya masoko kama ninavyofanya hapa. Kwaheshima na taadhima naomba sana kwa wale walio na taarifa za uhakika wa masoko ya mananasi Wakati nilopokuwa nikiuza mananazi toka kwenye shamba langu la hekari tano soko halikuwa tatizo wanunuzi ni wengi wamekuwa wakizunguka mashambani kutafuta mananasi na wakati mwingine wamekuwa hawapati na hawawezi hata kujaza magari yao, hiyo ilinitia moyo sana wa kuendelea kulima. Lakini kwa sasa nazungumzia shamba lenye mananazi zaidi ya 700,000 sio mchezo najua hayazai yote kwa wakati mmoja lakini kwenye 300,000 lazima niuze na nitaanza kuuza Nov-Dec mwaka huu. Kwa yeyote anayefahamu soko la uhakika anitaarifu ili tuweze kusuma gurudumu hili. Huwa najisikia fahari sana ninapofika shambani kwangu na kukuta watu zaidi ya 20 wakifanyakazi na kupata ridhiki ya halali wanayoitumia kwa ajili ya kukuidhi mahitaji mbalimbali ya familia zao, i feel so proud that kuna mchango ingawa mdogo lakini nasaidii nchi na ninasaidia jamii yangu. Tusaidiane ndugu zangu kwa roho safi katika kupambana na umasikini huu mzito.

3) Hatua inayofuatia in the near future nangalia uwezekano wa kutumia drip irrigation technology. Sasa nataka nianze kufanya utafiti wa upatikanaji wa underground water ili niweze kuchimba visima virefu. Kwa mtu yeyote mwenye taarifa ya kuwa maji yanaweza patikana ardhini katika maeneo ya Bagamoyo hususan Kiwangwa na kuelekea Mkenge naomba anitaarifu na kama kuna yeyote anayefahamu juu ya Bore-hole drilling companies in Bagamoyo naomba anifahamishe pia.

TOGETHER WILL MAKE IT HAPPEN
 
Kilimo cha nanasi, ni zaidi ya ulivyoandika. atakaefuata mchanganuo huo ameliwa
Ulichaandika hakijitoshelezi, sisi sote tupo kwenye kujifunza kwakuwa ndio tunaanza. Kwahiyo
kama unautaalam juu ya kilimo cha nanasi ni bora uutoe hapa ili sote tunufaike na kama la tuelekeze wapi pa kupata ushauri huo. Lakini manano matupu tu kuwa "kilimo cha mananasi ni zaidi ya ilivyoandikwa" haileti tija yeyote na wala husaidii Watanzania wenzako. Mimi kwa mfano, nipo nje ya nchi, najaribu kutafuta taarifa zinazoweza kunisaidia kuboresha kilimo hiki ila tatizo ni muda wa kuwa Bongo, sasa nikipata watu wa msaada kama ninyi mnaweza kusaidia. Ninauwezo wa kupand ahadi miche milioni moja bila shida lakini soko ni lipi la uhakika. Tunapozungumzia ajira hata sisi wengine tunaweza tengeneza ajira. Nilipofika shambani kwangu kwa project hii niliyoianza tu nilifarijika kuona takribani watu 20 wakifanyakazi shambani, nikajivunia kuwa ninatoa mchango tu. Kwahiyo tatizo ni jinsi gani ya kufanya na wala sio mtaji. Toa ushauri jinsi ya njia bora ya kulima mananasi. Natoa hoja.
 
Back
Top Bottom