USHAURI: Kilimo cha Mananasi na masoko yake Tanzania | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI: Kilimo cha Mananasi na masoko yake Tanzania

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by kanyagio, Nov 27, 2010.

 1. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 985
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Jana niliwasilisha mkusanyiko wa mada zinazohusu ufugaji wa kuku..

  Leo naomba niweke mkusanyiko wa mada za kilimo.. nimeamua kufanya hivi ili kusaidia wale ambao ni wanachama wapya na wanachama wengine ambao wanataka kujikumbusha mada hizo na kuchukua hatua:  ARDHI
  1. Ardhi ya kilimo: Ardhi ya kilimo
  2. Ardhi ya kilimo!!! Natafuta ardhi ya kilimo ya bei nafuu
  3. Shamba kwa ajili ya kilimo Shamba kwa ajili ya kilimo
  4. Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga
  5. Ardhi kwa Kilimo cha Kitunguu Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na masoko
  MAZAO
  1. Mazao gani yanafaa kwa kilimo chalinze? Part 1 Mazao gani yanafaa kwa kilimo chalinze?
  2. Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze? Part 2 Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze?
  3. Kilimo cha Mitiki: Utaalamu Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe
  MIKAKATI KATIKA KILIMO
  1. kilimo-wakulima wa jf getting together Wakulima wa JF getting-together
  2. Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali? Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali?
  3. Power tiller na dhana ya kilimo kwanza Power tiller na dhana ya kilimo kwanza
  4. Kwanza Kilimo? https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/31557-kwanza-kilimo.html
  5. Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo... Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo...
  haya ndo nimeweza kukusanya kwa leo.. hopefully hii itasaidia kutoa mwanga kwa wale wanaotaka kuperuzi posts mbalimbali..


  tukumbuke!! TUKIWEKA JITIHADA.. KILIMO KINALIPA!!.nawapeni mfano: unaenda Kiwangwa bagamoyo unanunua ekari moja ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha nanasi.  Gharama zitakuwa hivi:
  1. ununuzi wa ardhi kwa Tsh. 300,000-- (ekari ni hatua 70x70)
  2. utayarishaji wa shamba Tsh 150,000/=
  3. gharama ya miche na upandaji miche 15,000 kwa ekari Tsh 750,000 (i.e.50 x 15,000 ikijumuisha ununuzi wa mbegu na upandaji),
  4. Mbolea 100,000.
  5. matumizi mengine 200,000 (ikiwa ni pamoja ni vibarua, na kuleta mzigo sokoni).
  6. jumla 1,500,000/-
  Mapato
  nanasi unavuna baada ya miezi 18. kwa hesabu za chini kabisa unauza nanasi moja kwa Tsh 500 na assume unapata nanasi 12,000 utapata Tsh 6,000,000/=. (assumption ni kuwa si rahisi kupata mavuno 100%- bali inaweza kuwa 80%)

  Faida :
  ukiondoa matumizi (Tsh 1,500,000) unapata faida 4,500,000 ukiwa na ekari tano bila shaka utapata zaidi ya milioni 20 (na hapo hujaweka economy of scale). --though unaweza kupunguza au kuongeza asilimia fulani kutegemeana na risks zilizopo na uzoefu wako katika kusimamia na kutafuta masoko..

  soko likoje
  Kuna atakayeuliza je soko lipo-- mimi nasema soko lipo huko huko shamba au unaleta kwa BAKHRESA anayenunua matunda kwa ajili ya kutengeneza natural juice i.e. azam box juice). nasikia kuna kiwanda kingine kinaanzishwa bagamoyo (siyo bakhresa). ila tukumbuke kwa sasa ambapo nanasi ni chache ukienda sokoni huwezi pata nanasi chini ya 1,500/-

  Mfano hai
  Kamuulize ndugu Eric Shigongo mambo anayofanya Kiwangwa na anapata nini?-

  Mwenye taarifa zaidi au anayetaka kukosoa ni vema amwage hapa..

  Mkuu Malila upo?
   
 2. eselungwi

  eselungwi Member

  #61
  Jan 1, 2016
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  thanks
   
 3. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #62
  Jan 13, 2016
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,687
  Likes Received: 12,208
  Trophy Points: 280
  Hivi inawezekana ukaanzisha ufugaji wa mbuzi wa nyama kwa large scale?

  Masoko ya uhakika yapo?
   
 4. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #63
  Jan 13, 2016
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,687
  Likes Received: 12,208
  Trophy Points: 280
  Una connection na wateja wa middle east?
   
 5. n

  nangapake Member

  #64
  Jan 14, 2016
  Joined: Jan 12, 2016
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Masoko yapo tena mengi sana
   
 6. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #65
  Jan 19, 2016
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,546
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280

  Mkuu yako wapi hayo masoko?
   
 7. n

  nyakanazi JF-Expert Member

  #66
  Jun 2, 2016
  Joined: Jul 28, 2013
  Messages: 286
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 80
  Mkuu uhali gani bana. Asante sana kwa kuanzisha hii kitu juu ya suala la kilimo ila nimesikitishwa sana kuona kuwa washiriki wa mada hii muhimu inayoweza kuwatoa watu kwenye umasikini ni mdogo sana ukilinganisha na watu wanavyochangia mada za kijinga kwa wingi wao. Sasa ingawa ni mada ya muda mrefu ila ipo na itaendelea kuwa valid siku zote.
  Mimi binafsi ni mtoto wa Mkulima na ninapenda kilimo na nimeamua kuanza kilimo. Kwakuwa nafanyakazi nje ya nchi nikiwa narudi nyumbani mara kwa mara nikaamua nianze na kilimo ambacho hakitaniumiza kichwa sana hususan juu ya kuibiwa au kusimamiwa vizuri hivyo nikaamua nianze kidogo na mazao ambaya hayahitaji usimamizi wa karibu sana wa kila siku na mazao yanayostahamili maradhi na ukame kidogo.
  1). Nimeanza na miwa huko Kilombero. Nimelima takribani hekari 20 za miwa. Sina usumbufu kwenye hili kwakuwa gharama za kila kitu katika kuzihudumia zinafahamika. Nasoko lake ni Kilombero sugar na bei inafahamika hivyo sina haja ya siku zote kuwepo kwenye field. Natembelea mara chache na ninahakikisha wakati nina family member hasa huwa wife wakati wa kunyunyuzia dawa, kuweka mbolea na kukata miwa otherwise kijana wangu wa shamba anasimamia kazi zingine zote. Angalizi, ni ukweli kuwa uingizaji horera wa sukari toka nje kulituathiri sana na nilishindwa kuuza miwa yangu kwa miaka miwili mfululizo, nilipata hasara. Ninaimani kwa sasa kwa uongozi huu mpya huenda mambo yakawa safi kwa sisi wakulima. Kilimo cha miwa kama utauza kila mwaka ni kilimo kizuri sana na kina lipa kwakuwa gharama kubwa ni mwaka wa kwanza tu kwakuwa ukishapanda unaendelea kukata miwa kila mwaka kwa muda si wa chini ya miaka mitano mfululizo kutegemea na matunzo ya shamba. Agalizi hapa ni kuwa makato wakati wa kuuza kiwandani ni mengi sana kwa kiwanda, Serikali na vyama vya ushirika wa kilimo unakuta zaid ya 40% ya mauzo inakwenda huko, ni suala la kuangaliwa. Vilevile Kiwanda kinatakiwa kutoa kilimo cha mkataba such that kama miwa yangu haivunwi kwa mwaka mmoja au miwili vipi kuhusu gharama nilizoziingia? Vilevile vyama vile havina wasomi kabisa na hasa wanasheria wa kutetea maslahi ya wafanyakazi, haiwezekani kwenye business kubwa kama ile ikafanyika kienyeji hivyo, ingefaa chombo kinachohusika na masuala ya kilimo kuangalia jinsi gani ya kusaidia wakulima masikini wa Kitanzania ambao wengi kutokana na ujinga wa kutokwenda shule hawajui mambo mengi ya msingi ya haki zao. Niishie hapa juu ya kilimo cha miwa.

  2). Kilimo cha mananasi. Najaribu kulima mananasi. Miaka mitatu iliyopita nilinunua hekari tani katika kijiji cha Mwavi huko Kiwangwa Bagamoyo. Nililima mananasi kwa majaribio na niligundua kuwa kilimo hiki kikilimwa kwa umakini wake na kupata soko la uhakika watu wanaweza kabisa kuachana na umasikini. Faida uliyoielezea si kitendawili baili ni kweli. Nililima hekari chache tano ili kutafiti na nilipata vilevile bahati ya kutembelea shamba la Shigogo na nilinunua mbegu toka kwake na kujifunza na nilielimika sana na kushawishika kuwekeza zaidi. Januari mwaka Jana nilinunua virgin land yenye ukubwa wa hekari 60, kilomita 6 toka barabara kubwa ya lami (Bagamoyo-Msata) kuelekea Mkenge. Nilijipinda kufyka, kung'oa visiki, kulima na hatimae kupanda hekari 25. Hivi ninavyosema nimetoka Bongo juzi na nimemaliza kuweka mbolea shamba zima baada ya kwisha kwa mvua. Ni uwekezaji mkubwa kwa kiwango cha umaskini wa sisi Watanzania. Na kwasasa nimeweza kumaliza awamu nyingine ya kusafisha sehemu ya shamba iliyobaki (hekari 35) zote zimeng'olewa visiki na shamba lipo jeupe, kinachoendelea ni shughuli za kuchoma mkaa katika kulisafisha maana kuna miti mingi sana na baada ya hapo ni kuingiza trekta. Ila bado sijapanga nilime nini, nataka nitembelewe na wataalam wa kilimo kwa ushauri kabla sijaanaza uwekezaji wa ziada.
  Ila kwakweli nimelima mananasi na kama watu wengine nimelima bila kufanya utafiti mkubwa sana juu ya masoko makubwa na mapana ya mananasi na hii ni kwasababu nafanyakazi nje ya nchi na muda wangu ni mfupi sana wa kufuatilia mambo haya kwa kina. Lakini nikaona siwezi kusubiri hilo wakati nina ardhi nikaona nifanyekitu na mambo mengine yatakuja baade na wakati naendelea kulihidumia shamba nitakuwa nikiendelea kutafuta taarifa juu ya masoko kama ninavyofanya hapa. Kwaheshima na taadhima naomba sana kwa wale walio na taarifa za uhakika wa masoko ya mananasi Wakati nilopokuwa nikiuza mananazi toka kwenye shamba langu la hekari tano soko halikuwa tatizo wanunuzi ni wengi wamekuwa wakizunguka mashambani kutafuta mananasi na wakati mwingine wamekuwa hawapati na hawawezi hata kujaza magari yao, hiyo ilinitia moyo sana wa kuendelea kulima. Lakini kwa sasa nazungumzia shamba lenye mananazi zaidi ya 700,000 sio mchezo najua hayazai yote kwa wakati mmoja lakini kwenye 300,000 lazima niuze na nitaanza kuuza Nov-Dec mwaka huu. Kwa yeyote anayefahamu soko la uhakika anitaarifu ili tuweze kusuma gurudumu hili. Huwa najisikia fahari sana ninapofika shambani kwangu na kukuta watu zaidi ya 20 wakifanyakazi na kupata ridhiki ya halali wanayoitumia kwa ajili ya kukuidhi mahitaji mbalimbali ya familia zao, i feel so proud that kuna mchango ingawa mdogo lakini nasaidii nchi na ninasaidia jamii yangu. Tusaidiane ndugu zangu kwa roho safi katika kupambana na umasikini huu mzito.

  3) Hatua inayofuatia in the near future nangalia uwezekano wa kutumia drip irrigation technology. Sasa nataka nianze kufanya utafiti wa upatikanaji wa underground water ili niweze kuchimba visima virefu. Kwa mtu yeyote mwenye taarifa ya kuwa maji yanaweza patikana ardhini katika maeneo ya Bagamoyo hususan Kiwangwa na kuelekea Mkenge naomba anitaarifu na kama kuna yeyote anayefahamu juu ya Bore-hole drilling companies in Bagamoyo naomba anifahamishe pia.

  TOGETHER WILL MAKE IT HAPPEN
   
 8. Anwar2012

  Anwar2012 Member

  #67
  Sep 5, 2016
  Joined: Nov 25, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Kilimo cha nanasi, ni zaidi ya ulivyoandika. atakaefuata mchanganuo huo ameliwa
   
 9. n

  nyakanazi JF-Expert Member

  #68
  Sep 30, 2016
  Joined: Jul 28, 2013
  Messages: 286
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 80
  Ulichaandika hakijitoshelezi, sisi sote tupo kwenye kujifunza kwakuwa ndio tunaanza. Kwahiyo
  kama unautaalam juu ya kilimo cha nanasi ni bora uutoe hapa ili sote tunufaike na kama la tuelekeze wapi pa kupata ushauri huo. Lakini manano matupu tu kuwa "kilimo cha mananasi ni zaidi ya ilivyoandikwa" haileti tija yeyote na wala husaidii Watanzania wenzako. Mimi kwa mfano, nipo nje ya nchi, najaribu kutafuta taarifa zinazoweza kunisaidia kuboresha kilimo hiki ila tatizo ni muda wa kuwa Bongo, sasa nikipata watu wa msaada kama ninyi mnaweza kusaidia. Ninauwezo wa kupand ahadi miche milioni moja bila shida lakini soko ni lipi la uhakika. Tunapozungumzia ajira hata sisi wengine tunaweza tengeneza ajira. Nilipofika shambani kwangu kwa project hii niliyoianza tu nilifarijika kuona takribani watu 20 wakifanyakazi shambani, nikajivunia kuwa ninatoa mchango tu. Kwahiyo tatizo ni jinsi gani ya kufanya na wala sio mtaji. Toa ushauri jinsi ya njia bora ya kulima mananasi. Natoa hoja.
   
 10. n

  nyakanazi JF-Expert Member

  #69
  Sep 13, 2017
  Joined: Jul 28, 2013
  Messages: 286
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 80
  Wakulima wenzangu,ngoja nikili kuwa nililima kilimo cha kiswahili sana. Sikufanya utafiti wa soko kabla ya kulima, nililima tu kwakuwa nina ardhi na sikutaki ardhi ikae bure. Sasa natarajia kuvuna nanasi zaidi ya 200, 000 mwaka huu kuanzia Nov. Nahitaji yeyote anayefahamu soko la uhakika la nanasi na kama kuna mteja mkubwa tunayeweza kukubaliana katika reasonable price tuingie makubaliano. Bei ya viwandani siitaki kwakuwa ni dhuluma kubwa sana kwa mkulima.
   
 11. CityHunter1

  CityHunter1 JF-Expert Member

  #70
  Sep 13, 2017
  Joined: Feb 25, 2016
  Messages: 558
  Likes Received: 340
  Trophy Points: 80
  Umelima wapi?
   
 12. n

  nyakanazi JF-Expert Member

  #71
  Sep 13, 2017
  Joined: Jul 28, 2013
  Messages: 286
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 80
  Bagamoyo
   
 13. Jabman

  Jabman JF-Expert Member

  #72
  Sep 13, 2017
  Joined: Jul 27, 2016
  Messages: 1,017
  Likes Received: 1,306
  Trophy Points: 280
 14. M

  Mtalula Mohamed Member

  #73
  Mar 8, 2018
  Joined: Jan 25, 2018
  Messages: 14
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 5
  Kwa anayehitaji kupata ELIMU YA UZALISHAJI WA NANASI (general Knowlegde) mzigo huu hapa kwa kiswahili:

  Utangulizi
  Nanasi ni tunda la kitropiki, linapendwa na walaji wengi kwa sababu ya ladha yake tamu na harufu yake nzuri. Tunda hili laweza liwa mara tu baada ya kuvunwa, baada ya kulipika, au kama juisi. Nanasi ni chanzo kizuri cha vitamin A na B, pia inakiwango kingi tu cha vitamin C pamoja na madini kama vile: patasiam, magnesiam, kalsiam, na madini chuma. Asili ya nanasi inaaminika kuwa ni Brazil na Paraguay huko Amerika ya Kusini. Hapa Tanzania, nanasi hulimwa zaidi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha (Pwani), Tanga, Mtwara, Lindi, Geita na Mwanza. Lakini pia maeneo yote ya pwani ya Tanzania yanafaa kwa kilimo cha nanasi.

  Hali ya hewa inayofaa kwa ukuaji wa nanasi
  Kilimo cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita 1300 hadi 1750 hufaa zaidi kwa uzalishaji wa nanasi kwaajili ya kusindika na mwinuko chini ya hapo hufaa zaidi kwaajili ya ulaji wa moja kwa moja. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C.

  Udongo unaofaa kwa kilimo cha nanasi
  Kwa kilimo cha nanasi chachu (pH) ya udongo inayofaa ni 5.5 hadi 6.0, na hustawi vizuri zaidi katika udongo tifutifu na udongo wenye kichanga usiotuamisha maji. Ingawa nanasi huweza kustawi katika udongo wa aina yoyote ile, udongo wa mfinyanzi haufai kwa kilimo cha nanasi.

  Maandalizi ya shamba
  Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45. Shamba la nanasi unaweza kulilima kwa sesa (flat-bed) au kwa matuta (furrows).

  Kwa sesa: chimba mashimo kwa nafasi ya sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya kila mistari miwili. Weka mbolea kianzio katika kila shimo na upande, hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda. Weka tani 10 hadi 15 za mbolea ya kuku, weka pia viganja 2 vya mbolea ya zizi katika kila shimo.

  Upandaji wa mananasi
  Zipo aina mbali mbali za ‘mbegu’ (machipukizi/maotea) lakini yale yanayochipua kutoka ardhini hufaa zaidi na hukomaa mapema. Chagua machipukizi mazuri yenye umri mdogo na yenye kulingana kwa ukubwa. Iweke miche kwenye kivuli kwa siku 3 kabla ya kuipandikiza iweze kutoa mizizi haraka. Pandikiza mwanzoni mwa mvua za masika. Nafasi iwe sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya mistari miwili. Pandikiza miche 50,000 katika hekta moja. Chovya miche kwenye dawa ya Diazinon au Fention kwa muda wa dakika 25 kabla ya kuipandikiza ili kuzuia mashambulizi ya wadudu.

  Palizi - Kudhibiti Magugu
  Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu. Katika kilimo cha nanasi magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. Matumizi ya viuagugu hurahisisha zaidi palizi ya nanasi ukizingatia kuwa nanasi huwa na miiba katika ncha za majani yake ambazo huchubua ngozi endapo palizi za jembe zitatumika. Njia nyingine ni matumizi ya matandazo (mulch) ya majani au plastiki (plastic mulch) maalum kuzuia magugu.

  [​IMG]
  Shamba la mananasi

  Mahitaji ya mbolea ya mananasi
  Weka mbolea ya NPK gramu 50 hadi 70 kwa kila mche wakati wa kupanda. Weka tena gramu 85 kwa kila mche baada ya miezi 3 na pia miezi 3 baadae.

  Wadudu na Magonjwa yanayosumbua minanasi
  Nanasi ni zao lisilosumbuliwa na wadudu ama magonjwa mara nyingi. Hii ni faida kubwa sna kwa wakulima wa nanasi! Hivyo endapo patatokea mashambulizi ya wadudu na magonjwa, ushauri zaidi wa kitaalam utafutwe kukabiliana na tatizo husika. Hakikisha unakagua shamba ili kuzuia wadudu kama wataonekana.

  Uvunaji wa mananasi
  Nanasi huanza kutoa maua miezi 12 hadi 15 baada ya kupanda kutegemeana na aina ya nanasi au maotea ya mbegu yaliyotumika, muda wa kupanda na joto la mahali husika. Kwa kawaida nanasi hukomaa miezi 5 baada ya kutoa maua, hivyo nanasi huchukua miezi 18 hadi 24 kukomaa/kuiva. Katika kilimo cha nanasi, mimea ikitoa maua kwa nyakati tofauti tofauti itasababisha kuvuna kidogo kidogo na kwa muda mrefu. Kwa sababu hiyo ndio maana ni muhimu kupanda kwa wakati mmoja mbegu zenye umri na ukubwa sawa.
  Kwa wanaofanya kilimo cha nanasi kibiashara (commercial pinapples production) hutumia kemikali aina ya Ethrel (@ 100 ppm) mwezi mmoja kabla ya kuanza kutoa maua ili mimea mingi iweze kutoa maua kwa wakaii mmoja, angalau 80% ya mimea yote. Vuna wakati kikonyo cha nanasi kimebadilika rangi kuwa njano ya dhahabu. Kata kikonyo cha nanasi chenye urefu wa sm. 30 kikiwa kimeshikana na nanasi na upunguzie majani ya kichungi chake.

  Utunzaji wa mananasi
  Hifadhi nanasi katika eneo lenye ubaridi huku kikonyo chake kikielekea juu. Hakikisha unauza nanasi mara tu au siku 2 hadi 3 baada ya kuvuna ili kutunza ubora wake.

  [​IMG]
  Mananasi yaliyovunwa

  Source: JInsi ya kufanya Kilimo cha Nanasi | Mogriculture Tz
   
 15. Thad

  Thad JF-Expert Member

  #74
  Jul 20, 2018 at 12:27 AM
  Joined: Mar 14, 2017
  Messages: 6,346
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  bachelor sugu, njoo huku kumenoga!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...