USHAURI: Kilimo cha Mananasi na masoko yake Tanzania | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI: Kilimo cha Mananasi na masoko yake Tanzania

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by kanyagio, Nov 27, 2010.

 1. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 985
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Jana niliwasilisha mkusanyiko wa mada zinazohusu ufugaji wa kuku..

  Leo naomba niweke mkusanyiko wa mada za kilimo.. nimeamua kufanya hivi ili kusaidia wale ambao ni wanachama wapya na wanachama wengine ambao wanataka kujikumbusha mada hizo na kuchukua hatua:  ARDHI
  1. Ardhi ya kilimo: Ardhi ya kilimo
  2. Ardhi ya kilimo!!! Natafuta ardhi ya kilimo ya bei nafuu
  3. Shamba kwa ajili ya kilimo Shamba kwa ajili ya kilimo
  4. Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga
  5. Ardhi kwa Kilimo cha Kitunguu Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na masoko
  MAZAO
  1. Mazao gani yanafaa kwa kilimo chalinze? Part 1 Mazao gani yanafaa kwa kilimo chalinze?
  2. Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze? Part 2 Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze?
  3. Kilimo cha Mitiki: Utaalamu Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe
  MIKAKATI KATIKA KILIMO
  1. kilimo-wakulima wa jf getting together Wakulima wa JF getting-together
  2. Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali? Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali?
  3. Power tiller na dhana ya kilimo kwanza Power tiller na dhana ya kilimo kwanza
  4. Kwanza Kilimo? https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/31557-kwanza-kilimo.html
  5. Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo... Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo...
  haya ndo nimeweza kukusanya kwa leo.. hopefully hii itasaidia kutoa mwanga kwa wale wanaotaka kuperuzi posts mbalimbali..


  tukumbuke!! TUKIWEKA JITIHADA.. KILIMO KINALIPA!!.nawapeni mfano: unaenda Kiwangwa bagamoyo unanunua ekari moja ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha nanasi.  Gharama zitakuwa hivi:
  1. ununuzi wa ardhi kwa Tsh. 300,000-- (ekari ni hatua 70x70)
  2. utayarishaji wa shamba Tsh 150,000/=
  3. gharama ya miche na upandaji miche 15,000 kwa ekari Tsh 750,000 (i.e.50 x 15,000 ikijumuisha ununuzi wa mbegu na upandaji),
  4. Mbolea 100,000.
  5. matumizi mengine 200,000 (ikiwa ni pamoja ni vibarua, na kuleta mzigo sokoni).
  6. jumla 1,500,000/-
  Mapato
  nanasi unavuna baada ya miezi 18. kwa hesabu za chini kabisa unauza nanasi moja kwa Tsh 500 na assume unapata nanasi 12,000 utapata Tsh 6,000,000/=. (assumption ni kuwa si rahisi kupata mavuno 100%- bali inaweza kuwa 80%)

  Faida :
  ukiondoa matumizi (Tsh 1,500,000) unapata faida 4,500,000 ukiwa na ekari tano bila shaka utapata zaidi ya milioni 20 (na hapo hujaweka economy of scale). --though unaweza kupunguza au kuongeza asilimia fulani kutegemeana na risks zilizopo na uzoefu wako katika kusimamia na kutafuta masoko..

  soko likoje
  Kuna atakayeuliza je soko lipo-- mimi nasema soko lipo huko huko shamba au unaleta kwa BAKHRESA anayenunua matunda kwa ajili ya kutengeneza natural juice i.e. azam box juice). nasikia kuna kiwanda kingine kinaanzishwa bagamoyo (siyo bakhresa). ila tukumbuke kwa sasa ambapo nanasi ni chache ukienda sokoni huwezi pata nanasi chini ya 1,500/-

  Mfano hai
  Kamuulize ndugu Eric Shigongo mambo anayofanya Kiwangwa na anapata nini?-

  Mwenye taarifa zaidi au anayetaka kukosoa ni vema amwage hapa..

  Mkuu Malila upo?
   
 2. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #21
  Dec 8, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 985
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  ubarikiwe sana mkuu Malila
   
 3. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #22
  Dec 8, 2010
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mkuu malila nadhani Hiyo library yako itakuwa na mambo mazuri sana. Kama unayo online, type link tukachote ujuzi.
   
 4. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #23
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 7,948
  Likes Received: 4,079
  Trophy Points: 280
  Matokeo mazuri utayapata ukipanda kwa matuta. Matuta yanakuwa na udongo mwingi uliotifuliwa hivyo hurahisisha mizizi ya muhogo (ambayo ndo mihogo yenyewe) kupenya kwa urahisi na kutafuta chakula ardhini, tofauti na yule atakayetumia kilimo cha sesa ambacho huifanya mizizi ifike kwenye ardhi ngumu haraka na hivyo kusababisha mzizi kudumaa. Hivyo muhogo utakaotoka kwenye kilimo cha matuta utakuwa muhogo ulioshiba. Faida nyingine pia matuta yanahifadhi maji kwa muda mrefu tofauti na Sesa.

  Hivyo ndugu nakushauri utumie kilimo cha Matuta. Katika kutumia Cuttings ni vizuri ukitumia ndefu kama futi moja hivi au sm 30 na uchomeke kiasi cha sm 15 ardhini kwa kuulaza katika pembe ya nyuzi 45. Ni vizuri kupanda mihogo mara tu mvua zinapoanza hasa kwa maeneo yenyewe mvua za taabu hii itasaidia mihogo kushika vizuri ardhini na hivyo kuweza kushindana na jua mara msimu wa mvua unapoisha. Maana itakuwa imeshakuwa na mizizi mingi na yakutosha kuutafutia mmea chakula na maji ardhini.

  Utapata na kwa wengine.
   
 5. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #24
  Dec 13, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,364
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kwa karibu na Dar muhogo umepanda thamani sana,sasa hivi kipande cha muogo ni sh500 kwenda juu,hiyvo kwa mkulima itakuwa ni around 200sh kwa ukubwa/ujazo huo huo
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #25
  Dec 15, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,479
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Nakushukuru kwa mchango mzuri ndugu yangu.
   
 7. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #26
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 985
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  umefikia wapi na mchakato wako wa kilimo cha mihogo?
   
 8. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #27
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 985
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  malila, MIGINDU Ipo maeneo gani mzee????
   
 9. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #28
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 985
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  wazee mpo.. hivi nikitaka ramani ya mikoa mbalimbali ya Tanzania inayoonyesha mito (RIVERS) hasa ile midogo midogo nitaipata wapi.. hii itasaidia sana katika kutafuta maeneo ya kilimo cha umwagiliaji
   
 10. M

  Malila JF-Expert Member

  #29
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,479
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Ukifika Chalinze kama unakwenda Morogoro, kushoto kwako baada ya kuipita njia panda ya kwenda Moshi, kuna njia kubwa inaingia kushoto. Ukifuata barabara ile utafika Migindu na Gwata. Huko kuna ardhi ya nanasi na mhogo ya kutosha. Na sasa hivi serikali inapeleka maji toka Wami na umeme, kwa hiyo ni potential location kwa siku za usoni.
   
 11. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #30
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,364
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mkuu i doubt kama ipo ramani kama hiyo serikalini,labda ramani za awali enzi za wajerumani/waingereza
  utakapo pata tafadhali nami nijulishe ,kwani nhhitaji ramani kama hiyo in the mean time jaribu google earth
   
 12. M

  Malila JF-Expert Member

  #31
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,479
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Wizara ya maji ina hizo ramani na locations za mabonde yenye mito yote Tanzania, ila urasimu unaweza kukukimbiza, jipe moyo nenda.
   
 13. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #32
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 985
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  mbegu za miche ya nanasi umepata?. kiwangwa mbegu zinauzwa Sh 30 kwa moja na ekari moja unapanda miche ipatayo 10-15,000. unavyoziidi kupanda nyingi kwa ekari ndivyo unavyohitaji kuweka mbolea nyingi or kupata nanasi ndogo ndogo
   
 14. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #33
  Jan 17, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nashukuru sana mkuu
   
 15. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #34
  Jan 17, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu naomba maelezo kidogo kuhusu upatikanaji wa mbuzi wa maziwa, mbegu nitapata wapi na wanauza kiasi gani. Ahsante sana kwa msaada wako unaotoa.

  Kazwile
   
 16. Kifuniko

  Kifuniko Member

  #35
  May 23, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF nawapa heshima kwa kutoa ushauri na kupean mawazo mbalimbali, mimi nipo Geita Mwanza na nina shamba hekta 5 ninataka kuandika mchnganuo wa kuanzisha kilimo cha kisasa cha mananasi. Malengo ni kufikia hekta 100 in future lakini hizi ni kwa kuanzia. Naomba ushauri namna ya kuandika mchanganuo ili hata nikitafuta soko la bidhaa kwenye kampuni za juice na nyinginezo unisaidie kuwasilisha.
   
 17. L

  LAT JF-Expert Member

  #36
  May 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,412
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
 18. S

  Shaabukda Member

  #37
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Nawasalimu nyote.

  Tunahitaji ‘mbegu' (suckers au slips) kama elfu arobaini (40,000) hivi za mananasi aina ya ‘mpingo' kwa ajili ya kupanda ndani ya miezi miwili kuanzia sasa (18 April 2012 katika shamba lililopo kata ya Pembamnazi, Manispaa ya Temeke (DSM).

  Kwa yoyote ambaye angependa na anao uwezo wa ku-supply mbegu hizo na/au mbolea katika ubora, mahali na bei nilizotajata fadhali tuwasiliane kwa namba hii: +255-78-4308682. Kama unahitaji maelezo ya ziada kuhusu suala hili usisite kutuuliza.

  Karibuni, biashara ni maelewano. Tupo tayari kupokea ushauri wenu pia.
   
 19. S

  Shaabukda Member

  #38
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Nawasalimu nyote.

  Tunahitaji ‘mbegu' (suckers au slips) kama elfu arobaini (40,000) hivi za mananasi aina ya ‘mpingo' kwa ajili ya kupanda ndani ya miezi miwili kuanzia sasa (18 April 2012) katika shamba lililopo kata ya Pembamnazi, Manispaa ya Temeke (DSM).

  Kwa yoyote ambaye angependa na anao uwezo wa ku-supply mbegu hizo na/au mbolea katika ubora, mahali na bei nilizotajata fadhali tuwasiliane kwa namba hii: +255-78-4308682. Kama unahitaji maelezo ya ziada kuhusu suala hili usisite kutuuliza.

  Karibuni, biashara ni maelewano. Tupo tayari kupokea ushauri wenu pia.
   
 20. S

  Shaabukda Member

  #39
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu mbona kimyaa.....hakuna wakulima wa nanasi humu ndani?
   
 21. b

  beko Senior Member

  #40
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 186
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF,Binafsi
  Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 30 zilizopandwananasi hivi sasa, ambalo lina uwezo wa kuuza hadi tani 200 za mananasi kilamwaka. Nia yangu ni kupanua mradi huu mpaka ekari 100 ambazo zitakua na uwezowa kuzalisha hadi tani 700 kwa mwaka.Tuko kikundi cha watu nane na wote wanamalengo kama ya haya. Tuna mkakati wa kushirikiana na wakulima wengine ilituweze kuwa na uzalishaji mkubwa na wa kitaalamu endapo tuu, tutakuwa nauhakika wa soko la kudumu na la uhakika. Hivi sasa soko ni la msimu na sio la kuaminika hasaunapokua na volume kubwa, Mashamba yetu yapo huko Rufiji.Tunaomba mwenye mawazo kuhusu upatikanaji wa soko atujulishe.

   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...