USHAURI: Kilimo cha Mananasi na masoko yake Tanzania

kanyagio

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2009
Messages
986
Likes
45
Points
45

kanyagio

JF-Expert Member
Joined Dec 10, 2009
986 45 45
Jana niliwasilisha mkusanyiko wa mada zinazohusu ufugaji wa kuku..

Leo naomba niweke mkusanyiko wa mada za kilimo.. nimeamua kufanya hivi ili kusaidia wale ambao ni wanachama wapya na wanachama wengine ambao wanataka kujikumbusha mada hizo na kuchukua hatua:ARDHI
 1. Ardhi ya kilimo: Ardhi ya kilimo
 2. Ardhi ya kilimo!!! Natafuta ardhi ya kilimo ya bei nafuu
 3. Shamba kwa ajili ya kilimo Shamba kwa ajili ya kilimo
 4. Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga
 5. Ardhi kwa Kilimo cha Kitunguu Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na masoko
MAZAO
 1. Mazao gani yanafaa kwa kilimo chalinze? Part 1 Mazao gani yanafaa kwa kilimo chalinze?
 2. Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze? Part 2 Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze?
 3. Kilimo cha Mitiki: Utaalamu Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe
MIKAKATI KATIKA KILIMO
 1. kilimo-wakulima wa jf getting together Wakulima wa JF getting-together
 2. Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali? Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali?
 3. Power tiller na dhana ya kilimo kwanza Power tiller na dhana ya kilimo kwanza
 4. Kwanza Kilimo? https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/31557-kwanza-kilimo.html
 5. Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo... Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo...
haya ndo nimeweza kukusanya kwa leo.. hopefully hii itasaidia kutoa mwanga kwa wale wanaotaka kuperuzi posts mbalimbali..


tukumbuke!! TUKIWEKA JITIHADA.. KILIMO KINALIPA!!.nawapeni mfano: unaenda Kiwangwa bagamoyo unanunua ekari moja ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha nanasi.Gharama zitakuwa hivi:
 1. ununuzi wa ardhi kwa Tsh. 300,000-- (ekari ni hatua 70x70)
 2. utayarishaji wa shamba Tsh 150,000/=
 3. gharama ya miche na upandaji miche 15,000 kwa ekari Tsh 750,000 (i.e.50 x 15,000 ikijumuisha ununuzi wa mbegu na upandaji),
 4. Mbolea 100,000.
 5. matumizi mengine 200,000 (ikiwa ni pamoja ni vibarua, na kuleta mzigo sokoni).
 6. jumla 1,500,000/-
Mapato
nanasi unavuna baada ya miezi 18. kwa hesabu za chini kabisa unauza nanasi moja kwa Tsh 500 na assume unapata nanasi 12,000 utapata Tsh 6,000,000/=. (assumption ni kuwa si rahisi kupata mavuno 100%- bali inaweza kuwa 80%)

Faida :
ukiondoa matumizi (Tsh 1,500,000) unapata faida 4,500,000 ukiwa na ekari tano bila shaka utapata zaidi ya milioni 20 (na hapo hujaweka economy of scale). --though unaweza kupunguza au kuongeza asilimia fulani kutegemeana na risks zilizopo na uzoefu wako katika kusimamia na kutafuta masoko..

soko likoje
Kuna atakayeuliza je soko lipo-- mimi nasema soko lipo huko huko shamba au unaleta kwa BAKHRESA anayenunua matunda kwa ajili ya kutengeneza natural juice i.e. azam box juice). nasikia kuna kiwanda kingine kinaanzishwa bagamoyo (siyo bakhresa). ila tukumbuke kwa sasa ambapo nanasi ni chache ukienda sokoni huwezi pata nanasi chini ya 1,500/-

Mfano hai
Kamuulize ndugu Eric Shigongo mambo anayofanya Kiwangwa na anapata nini?-

Mwenye taarifa zaidi au anayetaka kukosoa ni vema amwage hapa..

Mkuu Malila upo?
 

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,487
Likes
909
Points
280

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,487 909 280
Kwanza nikushukuru kwa kazi nzuri sana hii ya kujitolea kuweka threads hizi pamoja,

Pili,niwahakikishie wadau wa kilimo kuwa tukilima kwa kumaanisha,kila kitu kinalipa. Siku moja nilikwenda Talawanda karibu na Kiwangwa kwa mzee mmoja,nanasi ni noma,kuna mayahudi yananunua shambani huna haja ya kupeleka sokoni hata kidogo. Mimi nilikuwa nimefuata mbuzi kwa huyo babu, nilipojaribu kupata mawili matatu kuhusu nanasi,nikaona inawezekana nikalima.

Hesabu zako Mkuu zinakaribiana sana na yule mzee pale Talawanda. Nilipanga kwenda Migindu,lakini muda hautoshi kukamilisha ratiba,ila nikifika migindu ndio nitajua bei ya Kiwangwa na Migindu tofauti ni nini?
 

newmzalendo

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2009
Messages
1,369
Likes
78
Points
145

newmzalendo

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2009
1,369 78 145
Asante sana,kwa hii breakDown
hivi nanasi mche unaupanda kila baada ya hatua ngapi?mbolea ya aina gani inatumika,kipindi kipi ni muafaka kupanda nanasi(mwezi gani)
 
Joined
Nov 22, 2010
Messages
31
Likes
9
Points
0

udasa99

Member
Joined Nov 22, 2010
31 9 0
kanyagio

Mchanganuo mzuri na wa kutia moyo. Nadhani kuna gharama nyingi ambazo hujazionyesha kwenye mchanganuo wako. Kwa mfano, gharama za kusafirisha miche (na assume miche haitapatikana hapo shambani), gharama za upaliliaji (yawezekana zaidi ya palizi moja kwa miezi 18), na gharama zingine nyingi ndani ya miezi 18. Ila kwa ujumla ni mchanganuo mzuri ya kuanzia.

Nawasilisha.
 
Last edited by a moderator:

Mutensa

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2009
Messages
426
Likes
13
Points
35

Mutensa

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2009
426 13 35
Waheshimiwa,
Namshukuru Mungu nimepata ardhi Kama hekari tano hivi na ningependa kufanya kilimo cha kisasa cha nanasi ila sina utaalamu wowote.
1. Mbegu za mananasi zinapatikana wapi?
2. Je ni lazima kiwe cha umwagiliaji, na kuna risk gain Kama ukiamua kitegemea mvua?
3. Kuna washauri wa kilimo cha aina hii hapa dsm na wanapatikana wapi?
 

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,487
Likes
909
Points
280

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,487 909 280
Waheshimiwa,
Namshukuru Mungu nimepata ardhi Kama hekari tano hivi na ningependa kufanya kilimo cha kisasa cha nanasi ila sina utaalamu wowote.
1. Mbegu za mananasi zinapatikana wapi?
2. Je ni lazima kiwe cha umwagiliaji, na kuna risk gain Kama ukiamua kitegemea mvua?
3. Kuna washauri wa kilimo cha aina hii hapa dsm na wanapatikana wapi?
Vipi mbuzi ulishapata mkuu?

Tuje kwenye nanasi, kama uko serious, nenda regional block Kibaha idara ya kilimo,pale watakupa kila kitu sawa na eneo ulilopata shamba kwa ukanda huu wa Dsm/Pwani. Kama hutajali nenda Kiwangwa bagamoyo ukajifunze kwa vitendo kwa wakulima, watakwambia faida ya mbegu za kisasa na faida ya mbegu za kienyeji kwa vitendo,naamu pia wakati na udongo gani unafaa.

Mbegu za nanasi ziko barabarani nyingi tu zinauzwa, ila kabla hujanunua fika Kibaha kwanza. Ukame unapunguza mavuno na kama unaweza nenda pale Mwenge njia ya Coca cola, kuna kituo cha serikali kwa ajili ya miche ya minazi/embe uliza kituo cha minazi. Pale kuna watalaamu kibao.

Mkuu kazi njema.
 

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,487
Likes
909
Points
280

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,487 909 280
bahati zijui kilimo cha mhogo.. mzoefu naomba asaidie katika hili
Kilimo cha mhogo si kigumu kama ambavyo wengi tunadhani, tatizo ni kwamba huko nyuma mhogo ulikuwa unadharauliwa sana, lakini cha msingi ni kujua kanuni za kilimo bora yaani shamba bora, mbegu bora, upandaji wa kitalaamu kama spacing, na wakati gani uvune, ulinzi dhidi ya wanyama, haya ndio mambo muhimu kwa mkulima. Sasa unataka kupanda kwenye matuta au sesa. wengi wanapenda kupanda mhogo ktk matuta zaidi japokuwa hata ktk sesa mihogo inazaa vizuri. Mihogo inapandwa kwa kutumia cuttings, yaani unachomeka mbegu zake kwenye shamba lililotayarishwa vizuri kwa mistari. Mhogo unapandwa wakati wo wote ili mradi shamba lina unyevunyevu wa kutosha. Urefu wa mbegu hutofautiana hasa kwa sababu ya mazoea yetu,wengine hupenda vipande vifupi na wengine hupenda virefu.

Nikutajie baadhi ya mbegu zetu, kibangameno ni mtamu sana na kwenye mvua nyingi sana hausumbuliwi na maji, yaani mkavu, Binti athumani huu ni mtamu na kisamvu chake kinalika sana na hauwi mkubwa kwa umbile na mwingine ni Bonga na butu( kigoma) huu una starch nyingi na unahitaji udongo mweusi.

Haya na wengine waseme.
 

kanyagio

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2009
Messages
986
Likes
45
Points
45

kanyagio

JF-Expert Member
Joined Dec 10, 2009
986 45 45
Kilimo cha mhogo si kigumu kama ambavyo wengi tunadhani, tatizo ni kwamba huko nyuma mhogo ulikuwa unadharauliwa sana, lakini cha msingi ni kujua kanuni za kilimo bora yaani shamba bora, mbegu bora, upandaji wa kitalaamu kama spacing, na wakati gani uvune, ulinzi dhidi ya wanyama, haya ndio mambo muhimu kwa mkulima. Sasa unataka kupanda kwenye matuta au sesa. wengi wanapenda kupanda mhogo ktk matuta zaidi japokuwa hata ktk sesa mihogo inazaa vizuri. Mihogo inapandwa kwa kutumia cuttings, yaani unachomeka mbegu zake kwenye shamba lililotayarishwa vizuri kwa mistari. Mhogo unapandwa wakati wo wote ili mradi shamba lina unyevunyevu wa kutosha. Urefu wa mbegu hutofautiana hasa kwa sababu ya mazoea yetu,wengine hupenda vipande vifupi na wengine hupenda virefu.

Nikutajie baadhi ya mbegu zetu, kibangameno ni mtamu sana na kwenye mvua nyingi sana hausumbuliwi na maji, yaani mkavu, Binti athumani huu ni mtamu na kisamvu chake kinalika sana na hauwi mkubwa kwa umbile na mwingine ni Bonga na butu( kigoma) huu una starch nyingi na unahitaji udongo mweusi.

Haya na wengine waseme.
Duu Malila, nimekuvulia kofia.,. maana taarifa ulizo nazo si mchezo!!!. utadhani una BSc Agriculture toka sokoine, kumbe mzee utaalamu umeupata shambani na ofisi za serikali ambazo walio wengi hatuzitumii aidha kwa kutokuwa na taarifa au kwa uzembe wetu.Thanks kwa taarifa...


kama nilivyoeleza hapo awali, mimi si mtaalamu wa kilimo cha mihogo... ila ni mtaalamu wa kutafuta taarifa mtandaoni.. na nimeona haka kajarida kafupi na kameandikwa kwa lugha rahisi katika mazingira ya africa kanaweza kusaidia kutoa taarifa zaidi kwa wanaohitaji... kanaiitwa starting a cassava farm na kanapatikana hapa: http://www.infonet-biovision.org/res/res/files/1855.Starting.pdf
 

Mutensa

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2009
Messages
426
Likes
13
Points
35

Mutensa

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2009
426 13 35
Amazing!!! Yaani hamuwezi kujua jinsi gani mmegusa maisha yangu leo, mmenisaidia sana.
@Malila - Mbuzi bado sijachukua, nilizama sehemu kishule kupunguza buibui ili nijitambue zaidi. Sasa nimerudi ulingoni, ni kilimo kwanza kwenda mbele.
 

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,487
Likes
909
Points
280

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,487 909 280
Kwa sasa nakamilisha banda la kufugia mbuzi wa maziwa na wanaozaa pacha,kama likikamilika kabla ya desemba hii wale mbuzi huwakuti,nimepita novemba na nikawaona wako vizuri. Hata kama nikiwalamba wote nitakuuzia mbegu.
 

Mutensa

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2009
Messages
426
Likes
13
Points
35

Mutensa

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2009
426 13 35
Hiyo Bomba mkuu, mie naendelea kukusanya nguvu kwanza kwa kukusanya ardhi. Baada ya Hapo nitakutafuta unipe uzoefu. Ningepe pia kujua zaidi juu ya hao Mbuzi wa wanaozaa mapacha. Wake mule kule mbezi Louis au?
 

Forum statistics

Threads 1,203,564
Members 456,824
Posts 28,118,974