Ushauri: Kila wakitaka kujenga ndugu/wazazi wa mume wanahitaji mume awasaidie

Bi dentamol

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
987
1,912
Changamoto za ndoa, dada yupo na stress za kufa mtu.

Iko hivi, kuna hawa wanandoa wameoana wana miaka karibia 2 sasa ya ndoa yao baba mwalimu wa secondary na mama mwalimu wa primary.

Dada anadai alipoolewa walikaa baadae mwanaume akamwambia ili wae huru kufanya maendeleo ya familia yao inabidi wawajengee wazazi wake mwanaume kwanza maana walipokua wanaishi mazingira hayakua mazuri, dada kweli kapima kaona ni sawa.

Mwaka Jana kweli wakajenga nyumba kufika October jamaa akamwambia ujenzi tumemaliza inabidi tulime kijijini kwa wazazi wake ili wazazi wasitusumbue chakula.

Dada kakubali mishahara yao ikatumika katika kilimo anavyodai kipindi wanafanya hayo yote ndani hakuna kununua kitu zaidi ya chakula na kulipa kodi na vitu vidogo vidogo.

Mwaka huu baada ya kumaliza kilimo dada kamwambia mwanaume sasa tuanze na sisi kujenga tununue kiwanja mwanaume kakubali.

Akaenda kwao kusalimia alivyorudi akamwambia baba yaake kamwambia nyumba moja haitoshi watu ni wengi wanabanana na hata wenyewe wakienda kusalimia watakosa pa kulala inabidi wajenge tena nyingine kubwa.

Dada akaomba basi kabla ya ujenzi angalau wanunue kiwanja chao mwanaume akamwambia asiwe na haraka watanunua viwanja hata 10 atulie kwanza.

Dada kakubali lakini kinachomuuma yeye anapigana angalau ujenzi wa kwa wakwe uishe na yeye aanze wake, mara jamaa anapigiwa simu anatakiwa ampeleke mdogo wake shule ambae alikataa ila sasa kaona umuhimu.

Jamaa katoa gharama zote kama laki 7 hivi hapo ujenzi unasimama,
mishahara ikitoka wanaendelea tena na ujenzi pole pole wakikaa kidogo kaka yake hua anaumwa, sasa watoto wake wapo shule wamekwama kaambiwa awalipie ada inabidi ujenzi usimame tena. Sasa dada anachanganyikwa anafanya kazi haoni maendeleo, anaomba ushauri afanyeje?

Kumbuka huyo ni mume wake wa ndoa tena ya RC.

Karibuni
 
Mmmh kuna wanawake wana uvumilivu jaman

Hio nyumba haitaisha kamwe,ndugu wa mume wameshaona ndugu yao ana hela nyingi hivyo matatizo yataongezeka siku hadi siku. Waafrika haturidhikagi kwa misaada ya ndugu na kubweteka ndo zetu. Wamewazoesha wenyewe wapambane tu na hali zao
 
Changamoto za ndoa, dada yupo na stress za kufa mtu.

Iko hivi, kuna hawa wanandoa wameoana wana miaka karibia 2 sasa ya ndoa yao baba mwalimu wa secondary na mama mwalimu wa primary.

Jamaa katoa gharama zote kama laki 7 hivi hapo ujenzi unasimama,
mishahara ikitoka wanaendelea tena na ujenzi pole pole wakikaa kidogo kaka yake hua anaumwa, sasa watoto wake wapo shule wamekwama kaambiwa awalipie ada inabidi ujenzi usimame tena. Sasa dada anachanganyikwa anafanya kazi haoni maendeleo, anaomba ushauri afanyeje?

Kumbuka huyo ni mume wake wa ndoa tena ya RC.

Karibuni

Ngoja siku Mwanamke akiamka Usingizi ataiona Ndoa chungu. Miaka hiyo miwili ya Ndoa ndiyo ya wao kujiimarisha na si kuimarisha Miji ya Watu wengine. Wataishia Kupanga huko mbele ya safari wasipokuwa makini.
 
Watu wengine walizaliwa jumapili nini? Au kawekewa limbwata na mumewe?
 
Back
Top Bottom