USHAURI: Kila baba wa familia awaapishe watoto wake kutoipigia kura CCM 2015...

Hapa kwangu wanafamilia wote, watoto wa kaka zangu, mama yangu mzazi , msichana wa kazi na wapwaa zangu nimewaeleza kuwa CCM hawastahili kuchaguliwa katika nafasi zozote zile, nao wakanijibu kuwa hata nisingewaambia wasingeichagua CCM.

Nilifarajika sana, nikaamuru wakanunue keki na soda kufurahia kuwa ndani ya nyumba yangu hakuna aliyekosa akili.

Kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa sitapiga kura naelekea kijiji kwetu kuhakikisha wagombea wa UKAWA wanapita. Napoteza kura yangu moja kwaajili ya kwenda kutafuta kura zaidi ya 1000 za wanakijiji.

Sijaombwa na yeyote, nafanya haya yote kwa faida ya Taifa langu. Wazalendo tuungane, tukusanye nguvu zetu, kila mmoja kwa namna yake ili tuondokane na hili balaa liitwalo utawala wa CCM. CCM ni mchongoma. Hata tusubiri miaka mingapi hatuwezi kupata machungwa toka kwenye huu mchongoma.

Tuanzie za mitaaa kutekeleza azimio hilo....
 
Upo sahihi mkuu,huu ni wakati wa kuipumzisha ccm na kuwakamata mafisadi wote warudishe pesa zetu!
 
usitegemee kumtimua mkoloni mweusi kwa kura bila kuingia magogoni sahau

Si tunaanzia hapo kabla ya kuingia barabarani. Kama akina Mzee Karume wameitwa Mashujaa wa Mapinduzi kwa nini kizazi hiki pia kisipate mashujaa wa mabadiliko nchini
 
Hivi bado kuna vise...nge bado vinaleta ukabila hapa? Wachaga ndio nani? Hebu peleka tigo yako huko kama inawasha eboooo.
 
Watanzania wote wapenda mageuzi wahakikishe wana wahamasisha wapenzi na wanachama wa vyama vya upinzani wajiandikishe kwenye daftari la wapiga kura, ili waweze kutumia haki yao ya kuchagua viongozi wa vijiji na mitaa hapo disemba 14.
 
Back
Top Bottom