USHAURI: Kikwete asipokuwa mkaidi kwa hili 2015 atatufikisha salama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI: Kikwete asipokuwa mkaidi kwa hili 2015 atatufikisha salama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbaga Michael, May 3, 2012.

 1. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Nasaha yangu kwa mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali yake ya Chama cha Mapinduzi kama kweli wanayo nia na malengo ya dhati katika taifa hili.

  Juhudi yetu ya kutafuta fedha inazidi kuongezeka! Sio kwamba tuipunguze, bali, badala ya safari nyingi, ndefu na zenye gharama kubwa za kwenda katika miji mikuu ya mataifa ya kigeni kwenda kutafuta fedha za maendeleo yetu, itafaa kufunga safari kwenda vijijini kuwafahamisha na kuwaongoza wananchi katika kujiletea maendeleo kwa juhudi yao wenyewe. Ndiyo njia ya kweli ya
  kuleta maendeleo kwa kila mtu.

  Hii maana yake si kwamba tangu sasa hatutajali fedha, wala hatutajenga viwanda au kufanya mipango yo yote ya maendeleo inayohitaji fedha. Wala siyo kusema kuwa tangu sasa hatutapokea wala kutafuta fedha kutoka nchi za nje kwa ajili ya maendeleo yetu.

  La, SIVYO;
  Tutaendelea kutumia fedha; na mwaka hata mwaka tutatumia fedha nyingi zaidi kwa maendeleo yetu ya aina mbalimbali. Kwahiyo
  itakuwa ni dalili moja ya maendeleo yetu. Lakini hii ni kusema kwamba tangu sasa tutajua nini ni shina na nini ni tunda la maendeleo yetu. Katika vitu viwili hivyo FEDHA na WATU ni dhahiri kwamba watu na JUHUDI yao ndiyo shina la maendeleo, fedha ni moja ya matunda ya juhudi hiyo.

  Tangu sasa tutasimama wima na kutembea kwa miguu yetu badala kupinduka na kuwa miguu juu vichwa chini kama hali ya nchi yetu ilivyo sasa. Viwanda vitakuja, na fedha zitakuja, lakini msingi wake ni WANANCHI na JUHUDI yao na hasa katika KILIMO. Hii ndiyo maana ya kujitegemea.

  Kwa hiyo basi, mkazo wetu na uwe
  (a) Ardhi na Kilimo
  (b) Wananchi
  (c) Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, na
  (d) Uongozi bora
   
Loading...