Ushauri katika kutimiza malengo

Sep 20, 2020
60
125
Naomba kuchukua Nafasi hii kukushauri ewe kijana katika suala Zima la kutimiza malengo yako!

1. Muonekano wako sio guarantee ya kufanikiwa kwenye maisha!
Vijana wengi hupoteza fedha zao katika mavazi bila kujali kuwa mavazi hayana dhamana yoyote itakayo kusaidia wakati wa shida! Pambana kwa malengo, Timiza ndoto zako kwanza mavazi Yapo tu Ila rasilimali ya Muda ulionao Sasa ndio nyenzo peekee.

2. jitajidi Sana kuficha malengo yako yawe Siri! Aliwai kusema Fid q! Mafanikio ni Kama nguo ya ndani ! Hakikisha hawaijui rangi! Hakuna mtu anaependa maendeleo ya mwenzie hivyo kuwa makini Sana katika kuficha malengo yako! Mana Kuna watu wapo kwa ajili ya kukurudisha Nyuma.

3. Weka ukomo katika kutimiza ndoto zako! Deadline!
Ukiweka ukomo wa kufanikiwa katika Jambo Fulani Basi itakuwa njia rahisi ya kufikia Jambo lako kwa wakati lakini pia itakuwa sababu ya kuwa na juhudi binafsi ili uweze kufikia ndoto zako.

4. katika kutimiza malengo, jaribu kutimiza malengo ambayo yatabadilisha maisha yako kwa muda mfupi

Kuwa bize Sana katika kufanikisha Mambo ambayo ukiyakamilisha itakuwa sababu ya kubadilisha maisha yako! Note upekee katika Jambo la kipekee ndio njia pekee ya kukufikisha mahali pa kipekeee!

5. Amini katika ndoto zako!

Kila kitu kinawezekana, usijaribu kubadilisha mawazo yako kwasababu ya mtu Fulani! Ila badilisha ndoto zako ilo kufikia hatua Fulani muhimu..

Mwisho! Ni Bora uonekane mchafu leo! Ila ujenge na kuipendezesha kesho yako! Kwasababu watakao nufaika na kesho yako sio ulionao Sasa Ila ni wale utakao kuwanao kesho!

Ahsante
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom