Ushauri: Kapata supp, mwalimu anataka apewe rushwa ya ngono ili amfaulishe

Paa

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
1,449
2,924
Wanabodi, nina ndugu yangu (wakike) kafeli somo moja katika mitihani yake ya mwisho wa semester, (ana supp). Sasa wakati huu wa likizo mwalimu wa hilo somo kamtafuta kwenye simu kaomba ngono ili aje kumfaulisha mtihani wa supp asije kupata carry.

Wasi wasi wangu ni kuwa dogo anaweza kufaulu mtihani wa supp lakini mwalimu akamfelisha kama hatakubaliana na ufedhuli wa mwalimu

Pia kwa utaratibu wa chuoni hapo kama mwanafunzi atashindwa kufaulu mtihani wa supp kwa somo hata moja, itabidi mwanafunzi huyo arudie kulisoma somo hilo moja tu mwaka mzima wa masomo (yaani hataweza kuendelea na masomo mengine mpaka afaulu hili alilolata sup)

Nimewaza kuripoti swala hili TAKUKURU, na kwenye uongozi wa chuo ili dogo asije akadhulumiwa haki yake kwa sababu ya tamaa za mtu.Japo ni kweli anaweza kuwa alishindwa kufikisha maksi zinazohitajika somo husika kihalali, lakini sidhani kama ni vizuri mtu kuitumia nafasi hiyo kumkandamiza.
NB:Ushahidi wa SMS anazotuma mwalimu upo.

Kabla sijafanya maamuzi, ninaomba kupata experience kutoka kwenu, ni namna gani bora niitumie kupata muafaka mzuri wa hii issue?
 
Nakushauri kama wewe ni mwanaume unayetongoza watoto wa watu wengine usiende chuoni wala takukuru. Mwambie dogo akuforwadie hizo msg then mvae ticha kiutu uzima. Mwambie ulikuwa na nafasi ya kwenda takukuru na kumwaribia kazi.Lakini ukikumbuka kila mtu anaghafilika na kuwaza familia yake itakapopata taabu kwa ujinga wake umeona uje uonane naye man to man. Naamini atakuelewa na atakushukuru. Dogo aendelee kujisomea na naamini atasapua l.
 
Japo mwalimu hatamuachia walahi Degree za kuvuana chupi nyingi sanaa
 
Mabinti wanamitihani kweli alafu ukute ticha mwenyewe mzee dha
Usilipoti chuo maana binti atapoteza yaani sup zitaongwzeka
Uko takukuru sina uhakika mpaka sasa kesi ni nyingi lakini wahusika wanadunda mtaani
Unatoa ushauri gani? king360
 
Chuo gani hicho huruhusiwi kuendelea na masomo mengine ukicarry?
Soma hiyo section 16.1.7
Screenshot_20190919-075903_Drive.jpeg
 
Nakushauri kama wewe ni mwanaume unayetongoza watoto wa watu wengine usiende chuoni wala takukuru. Mwambie dogo akuforwadie hizo msg then mvae ticha kiutu uzima. Mwambie ulikuwa na nafasi ya kwenda takukuru na kumwaribia kazi.Lakini ukikumbuka kila mtu anaghafilika na kuwaza familia yake itakapopata taabu kwa ujinga wake umeona uje uonane naye man to man. Naamini atakuelewa na atakushukuru. Dogo aendelee kujisomea na naamini atasapua l.
Huyo ticha inaonekana sio mara yake ya kwamza kufanya huo upuuzi na sidhani kama asipoona consequences anaweza kuacha kirahisi.. dawa yake ni kumletea takukuru na makamera ya azam ,tbc ,clousd hadi shilawadu...
Huu upuuzi lazima uishe.. dada zetu wanateseka.. imagine dada wa miaka 21 alale na zee la miaka 50 bila ridhaa yake kisa tu kafeli mtihani mmoja.
Ifike wakati tusifumbie macho makosa ya namna hii maana kesho hata sisi tutakuwa wazazi na watoto wetu au dada zetu watafanyiwa upuuzi huu na mabazazi ya hivi
 
Mwalimu kapataje namba ya mwanafunzi? Sio kwamba mwanafunzi ndo kampigia simu mwalimu na mwalimu akaona upenyo wa kuomba penzi? Kesi za namna hii huwa zina pande mbili. Watoto wakishindwa masomo hutafuta visingizio ikiwemo kuwaingiza kwenye 18 walimu.
Namba za wanafunzi zinakuepo kwenye admission information zao, na kama mwalimu akizihitaji anapata tu bila shida.
Yeye ndio kaniambia kuwa mwalimu anamsumbua, sidhani kama ameyataka mwenyewe. Ngoja niendelee kupeleleza
 
Back
Top Bottom