Ushauri: Kanipiga na mkoba wake akaniumiza alafu ananiomba msamaha

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,733
26,867
Wakuu heshma zenu!!
Wakuu naombeni ushauri wenu!!

Jana wakati niko na shemeji yenu/wifi yenu tulienda kufanya shoping supermarket! Sasa wakati tuko mle ndani tukakutana na werembo wengine!!

Kusema na ukweli kuna mrembo mmoja alipita hata kama ni wewe lazma ungegeuza shingo maana upande wa 0713.

Nadhani muumba ulipapendelea sana!!sasa mimi nikageuza shingo kumtizama kumbe yule shemeji yenu ameshasogea mbele kama hatua 5 na mimi nilikuwa nimesimama naangalia ule mzigo.

Sasa yule shemeji yenu akaja speed na mkoba wake akanipiga nao kichwani mbele za watu akasema ""twende huko unashangaa nini"yaani wakuu nilijisikia aibu sana na isitoshe aliniumiza kichwa na mkoba wake ndani mle sijui aliweka vikopo gani maana kichwa kilivimba hadi leo sijaenda kazini, na tangu jana sijamwambia chochote anaanza kuniomba msamaha.

Wakuu nishaurini nimfanye nini!!
 
Wa stendiiii, huishi visa wewe.. Anyway , mi nakukubali sana
Kam ameliona kosa lake cha msingu kumsamehe tu, kutofautiana ni jambo la kawaida katika maisha...
 
Mkuu nimecheka sana.

Nilijua ni ndugu ya mbunge wa ulanga mhe. Goodluck. Sijui taarifa yake kama ilipokelewa na spika.

Pole kwa kuumia.
 
hv una watoto kweli ?

Kama umeshindwa kuvumilia ukiwa na mkeo sijui utavumilia lini na wapi
 
duh, sasa we upo na shem halafu unashangaa mizigo mingine we mtambo nn? Hata mi ningemnasa kofi kama angekuwa yeye ndiye anashangaa mwenzangu mwenye range rover, ilihali tupo tunatembea kwa teke!
 
Wakuu heshma zenu!!
Wakuu naombeni ushauri wenu!!

Jana wakati niko na shemeji yenu/wifi yenu tulienda kufanya shoping supermarket! Sasa wakati tuko mle ndani tukakutana na werembo wengine!!

Kusema na ukweli kuna mrembo mmoja alipita hata kama ni wewe lazma ungegeuza shingo maana upande wa 0713.

Nadhani muumba ulipapendelea sana!!sasa mimi nikageuza shingo kumtizama kumbe yule shemeji yenu ameshasogea mbele kama hatua 5 na mimi nilikuwa nimesimama naangalia ule mzigo.

Sasa yule shemeji yenu akaja speed na mkoba wake akanipiga nao kichwani mbele za watu akasema ""twende huko unashangaa nini"yaani wakuu nilijisikia aibu sana na isitoshe aliniumiza kichwa na mkoba wake ndani mle sijui aliweka vikopo gani maana kichwa kilivimba hadi leo sijaenda kazini, na tangu jana sijamwambia chochote anaanza kuniomba msamaha.

Wakuu nishaurini nimfanye nini!!
Mkuu, tafadhali msamehe tu kwani hajafanya makusudi. Haya mambo ya magegedeo na Papuchi wee acha tu!!
 
Mkeo wala hana kosa. Kosa ni la shingo yako na kichwa kugeuka kumuangalia huyo dada wakati ulishakata shauri kuwa na mkeo milele mpaka kifo kiwatenganishe
 
Mi mwenyewe ningegeuka napenda sana mibinuko,kwa raha ya kuangalia mbinuko hata angenipiga na nyundo maumivu yangekua si kitu.
 
Sikia, mwambie umemsamehe, tenga siku utoke tenanae, hakikisha siku hiyo hugeuki nyuma, unamlia taimingi, akigeuka kuangalia chochote ilimradi upande huo kutakuwa na mwanaume, mkate bonge ya kibao cha shingo hadi akate moto, mkirudi home nawe muombe msamaha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom