Ushauri: Kambi ya Jeshi ijengwe baada daraja la mto Rufiji ili kudhibiti uhalifu

Mwamanda

Senior Member
Feb 24, 2009
150
49
Kutokana na matukio yanayoendelea kutokea katika maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri na maeneo ya barabara kuu iendayo Mtwara nashauri kambi ya jeshi ijengwe baada mto Rufiji katika msitu mkubwa kuelekea Muhoro pia iwe na detach ndogo ya Navy ili ifanye ulinzi katika pwani hiyo na delta ya mto Rufiji.

Mtakumbuka delta ndio iliyotumika kuficha méli ya kijerumani wakati wa vita kuu ya pili.
 
Tukio dogo kama hilo haliwezi sababisha kambi ijengwe huko
Vinginevyo watajenga makambi mchi nzima
 
hivi mnadhani tuna roho za ziada eeehee? kazi yetu ni kupambana na adui wa nje na kulinda mipaka. kazi ya kulinda raia na mali zao ni kazi ya polisi
 
Kambi sio ufumbuzi wa tatizo. Bali kujua chanzo na sababu za mauaji hayo kila siku.
 
Kutokana na matukio yanayoendelea kutokea katika maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri na maeneo ya barabara kuu iendayo Mtwara nashauri kambi ya jeshi ijengwe baada mto Rufiji katika msitu mkubwa kuelekea Muhoro pia iwe na detach ndogo ya Navy ili ifanye ulinzi katika pwani hiyo na delta ya mto Rufiji.

Mtakumbuka delta ndio iliyotumika kuficha méli ya kijerumani wakati wa vita kuu ya pili.
Hadi leo meli ya Kijerumani ipo mto Rufiji.
 
Ule msitu baada ya daraja la mto Rufiji umekuwa na matukio ya uhalifu muda mrefu kiasi kwamba pale Ikwiriri panakuwa geti linalozuia Magari kutembea baada ya saa12 jioni kuogopa kuporwa mpaka upewe escort ya polisi na pia kutokana kuwa na mapori mengi pamekuwa vigumu kuweka ulinzi wa kutosha .Pia tusisubiri mpaka watu wadhurike ndio tuwasake.
 
Back
Top Bottom