Ushauri Kama Tido Mhando hamumtaki mpeni hata millard hayo TBC ibadilike

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,516
Habari wadau..
Kiukweli TBC imerudi nyuma sana kwa maoni yangu.. sio ile TBC ya tunaangalia hadi EPL, sio ile ya kuangalia vipindi vya kisasa kwa Quality ya kisasa..

TBC ilikuwa hadi na midahalo ya ukweli, Tangu alivyoondoka Tido Mhando TBC inazidi kufa..Yaani hata uwe na Tv ya kisasa ya bei gani bado picha quality ya TBC ni mbovu na vipindi vibovu
 
Viva Millard Ayo...naona neema ikimkaribia kwani amekuwa akitajwa tajwa sana hivi karibuni !
 
Yeye si anafikiria kuwapa Ma Dr na Ma Profesa ukuu wa Taasisi za umma ndio ufanisi wake..
TBC inamfia Dr Rioba hivi hivi.
 
Vitu vya serikali mkuu vingi haviko vizuri, nyumba za askari, ofisi za halmashauri, TTCL ilivyo pia hairidhishi n.k.
 
usimtafutie balaa la bure dogo milard,watamlazimisha kuvaa misuti na misuruali yenye marinda wakati yeye kashazoe kulipuka na makapelo,mapensi...

baadae mtamlaumu tu sababu hamjui kuwa tatizo sio akina ayoub bali ni funding ndogo kutoka serikalini.
 
TBC apo ni shida aka kasumba ka Kila Taasisi MD awe Na Master au PHD itamtokea Puani
 
Tatizo kubwa la TBC ni ukosefu wa watu wanaosikiliza mawazo.

Hata aende Malaika TBC haiwezi kubadilika, kwa sababu wenye maamuzi makubwa na TBC ni CCM.
Nimegundua hata Dr Rioba tunamlaumu bure tu.

Huwezi ukafanya jambo kwa maono yako pale, lazima utaondolewa.
 
TBC haina tofauti na TTCL kwa ushauli wangu pale pangebaki kama Museum tu.
Kipindi kizuri plale TBC ni [HASHTAG]#UBONGO[/HASHTAG] KIDS over.
 
Sasa
Tatizo kubwa la TBC ni ukosefu wa watu wanaosikiliza mawazo.

Hata aende Malaika TBC haiwezi kubadilika, kwa sababu wenye maamuzi makubwa na TBC ni CCM.
Nimegundua hata Dr Rioba tunamlaumu bure tu.

Huwezi ukafanya jambo kwa maono yako pale, lazima utaondolewa.
ata Quality za picha na vipindi???????
 
usimtafutie balaa la bure dogo milard,watamlazimisha kuvaa misuti na misuruali yenye marinda wakati yeye kashazoe kulipuka na makapelo,mapensi...

baadae mtamlaumu tu sababu hamjui kuwa tatizo sio akina ayoub bali ni funding ndogo kutoka serikalini.
Umenichekesha sana mkuu....nilikua najiiba kuchungulia uzi so kinachoendelea naambiwa kikao baadae kujadiliw
 
hivi na watangazaji wao wanawatoa nchi gani wamepauka sana. jamani hakuna hata make up kidogo?
 
Viva Millard Ayo...naona neema ikimkaribia kwani amekuwa akitajwa tajwa sana hivi karibuni !

Neema ipi mkuu?

Kuwa CEO wa TBC sio neema mkuu, kule unaenda kupoteza hata kale kaheshima kadogo ulikonako "japo utakuwa unalia ndani ya VX"
 
yani Millard ndo akapige mihayo TBC na vimishahara vyao vya mawazo na amri za kijinga
wamchukue bashite c kijana pia
 
Wampeje sasa, millard ayo ana fedha na uzoefu wa kuendesha tv?
Youtube ni tofauti sana na tv ndugu
Youtube account hata wewe unaeza kua nayo
 
Back
Top Bottom