chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 11,977
- 20,616
Nilimsikia Rais wetu mpendwa Mama Samia akisema tuanzishe Benki ya Vijana. Kwa kuwa alileta wazo, basi mimi naongezea katika wazo lake, Benki zilizopo zinatosha, ila serikali iweke dirisha maalum kwa ajili ya vijana.
Nina maana kwamba, kama serikali ilipanga kutumia bilioni hamsini kuanzisha Benki, basi hizo hela ziwekwe katika mabenki yaliyopo. NMB-Posta, CRDB na kadhalika, kijana akitaka kukopa anakwenda huko.
Kuanzisha Benki upya kabisa ni shughuli pevu, na pia serikali itakuwa imejiondoa katika mtego wa vijana kuona hiyo ni mikopo ya kisiasa, na pia mabenki hayo yana uzoefu wa kushughulika na mikopo.
Ni hayo tu.
#matege
RIHel Stone