Ushauri juu ya unywaji wa soda

Mossesaginga

Member
Jul 14, 2021
6
9
Lakini ni dhahiri kwamba soda imekuwa ikihusishwa na magonjwa lukuki; saratani, figo, mifupa, mstuko wa moyo. Pia, unywaji wa vitu vya sukari pia unasababisha kuwa na unene, kitambi na upungufu wa madini muhimu mwilini. Soda haina umuhimu wala faida mwilin.

Orodha hiyo ya athari za unywaji soda pia inahusisha kuzeeka haraka. sumu zilizo kwenye soda zinazeesha mapema. Yaani kijana mdogo miaka 20 hujikuta anaonekana kama wa miaka 40.

.Soda ina kemikali inayoitwa phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya calcium kwenye chakula. Madini hayo ni muhimu kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kwenye mwili wa binadamu.

soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu. Sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kuua figo. Hupunguza kiwango cha maji mwilini kwa kuwa ina kiwango kikubwa cha madini ya sodium.


Ushauri ni vizuri kubadili mfumo wa maisha na kuanza kunywa vitu ambavyo haviharibu mwili kama vile kunywa juisi ya matunda badala ya soda.
 
Back
Top Bottom