Ushauri juu ya kuoa

Muwazi

JF-Expert Member
May 16, 2014
355
81
1: Usioe kwa sababu umechoka
kula kwa mama lishe>>Mke sio
mpishi kama umechoka kula kwa
mama lishe jifunze kupika.
2: Usioe kwa sababu umechoka
kufua na kupika >>Mke sio
housemaid, kama umechoka kufua
ajiri mtu akufulie.
3: Usioe kwa sababu rafiki zako
wote wameoa >>Mke sio
mashindano maana hataishi na
marafiki zako wala sio zawadi kwa
wazazi wako bali wewe ndiwe
utakayeishi naye.
4: Usioe kwa sababu unataka
kufungua kanisa sasa unatafuta
mama mchungaji
5: Usioe kwa sababu wazazi
wanakulazimisha maana dada zako
wote wameshaolewa.
6: Usioe kwa sababu mpenzi au
mchumba amepata mimba yako.
7: Usioe kwa sababu unataka
kumuonyesha msichana aliyekuacha
kuwa bado upo juu.
8: Usioe kwa sababu unamhurumia
msichana uliyenaye ukimuacha
atachanganyikiwa.
9: Usioe kwa sababu wazazi wako
wanampenda na kumkubali
msichana huyo.
10: Kuliko kumuoa msichana kwa
kumhurumia na si kumpenda
itapelekea kuteseka moyoni maisha
yenu yote ni afadhali umwambie
ukweli kungali mapema
11: Kuoa ili kujionyesha kuwa ume-
move on baada ya kuachwa ni
kujikomoa mwenyewe.
Oa ukiwa na uhakika kuwa huyo
ndiye chaguo lako pekee na upo
tayari kuishi naye katika hali zote,
ndio mpango wa Mungu katika
maisha yako na ndiye
unayempenda kwa moyo wako
wote.
 
Acha habari zako yaani wewe dume zima na goroli zako 2 upike?? tabia za kuelekea ushoga hizo mkuu! pika mwenyewe,mimi sipiki ng'o,ebo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom