Ushauri juu ya biashara ya viatu na vipochi vya kike

Secret person

JF-Expert Member
Sep 23, 2019
242
358
Habari Wakuu.

Nimekuwa nikifanya biashara ya Viatu vya mtumba simple za wadada na Raba kwa Dar ambapo Uwa nilianza kwa kupoint Hivi viatu soko la karume Alfajiri sana unajihimu.

Kwa sasa nimepata wazo la kwenda kufanya biashara hii katika mkoa wa Iringa ambao ndo asili yetu na sababu kubwa ya kutaka kwenda huko ninaamini ndo ninatoboa.

Kiuhalisia kwa Upande wa Iringa ninachojua nina Ndugu so uhakika wa kukaa upo.

Nilikuwa ninaomba ushauri wenu wakuu.

Mtaji ninao 200K na stock zaidi ya Pair 30 ambazo uwa natembeza kwa Dar.
 
Mkuu unakimbiaje DSM unaenda porini boss , anyway maisha popote kila lakher....!!! But nachoona umekosa strategically plan Tu hapa bongo
 
Changamoto gani unazoziona ziko Dar hadi kushindwa kutoboa kirahisi? Je changamoto hizi hazipo Iringa?

Mimi naona ni kama mvuvi anaye lalamika samaki baharini hakuna akaenda kuvua mtoni.
Changamoto kwanza Kupata Eneo la Uhakika ni shida Suala lingine Mkuu Dsm Wauza raba Tupo Wengi sana Mjini boss...
 
Mkuu unakimbiaje DSM unaenda porini boss , anyway maisha popote kila lakher....!!! But nachoona umekosa strategically plan Tu hapa bongo
Unachoongea kinaweza Kuwa sahihi Boss sijapata. Exposure kutoka kwa watu wanaofanya biashara hii.
 
Changamoto kwanza Kupata Eneo la Uhakika ni shida Suala lingine Mkuu Dsm Wauza raba Tupo Wengi sana Mjini boss...
Wewe biashara yako si ni ya kutembeza, eneo la nini? Anza kutembeza kwanza. Tafuta vijana wengine waaminifu kama wawili hivi wakutembezee. Wewe unawapa raba pea kadhaa na unakuwa umemwambia kila pea unataka shs ngapi..yeye anajiongeza cha juu. Mdogo mdogo...utafika tu
 
Back
Top Bottom