barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Wakuu mtanisahihisha kama nakosea,au kama naingilia ya watu basi mtanikosoa...Lakini nia yangu ni njema tu.
Hapa jirani na mji wangu kuna nyumba moja ya ibada.Katika hiyo nyumba ya ibada kuna mwalimu na watoto wanaojifunza dini kila siku muda wa baada ya masomo ya elimu dunia.
Karibu ya nyumba hiyo ya Ibada kuna uwanja wa wazi,ambapo sisi hapa mtaani huutumia kama sehemu ya mazoezi kwa nyakati za asubuhi na jioni.
Mimi ni sehemu ya watumiaji wa uwanja huo pamoja na wananzengo wenzangu wa mtaani wanaopunguza viribatumbo.Uwepo wangu hapa hata hawa watoto wa shule hii ya elimu ya dini wanautambua.
Sasa,kwenye hiyo shule kuna mwalimu wa dini,kiukweli anawachapa sana sana watoto.Iwe wasichana au wavulana wanakula sana makwenzi na kupigwa bakora.Na watoto hawa ni kati ya miaka 06 hadi 14.Weekend hii jioni milikiwa pale kupasha misuli na kijana wangu.Mtoto mmoja akatoka kwenda kukata fimbo katumwa na yule mwalimu wa dini,fimbo kwa ajili ya kuwachapia wale watoto.
Mbaya zaidi huyu mwalimu anachapa watoto kwenye vidole na upande wa nyuma wa miguu(Kwenye vistrung).Watoto wanalia sana,wanaumizwa sana.Sijajua kama wazazi wanajua aina hii ya upigwaji wa watoto,lkn kiukweli huyu mwalimu anawachapa sana watoto tena wakati mwingine kwa viboko vinavyovuka idasi ya kawaida.
Sasa watoto wengi hupitia ninapoishi kunywa maji watokapo hapo shule,niliwadadisi juu ya vipigo vya weekend ile,wakasema mmoja alichapwa kwa sababu alikuwa anawasimulia wenzake juu ya mechi ya Arsenal huko Ulaya,wakati mwalimu alishakataza wasiangalie wala kushabikia team za Ulaya,mwingine alikula fimbo baada ya wenzake kumshtaki kuwa shuleni alikaa dawati moja na wanaume wakati mwalimu alishakataza,lkn yule mtoto alijitetea kuwa mwalimu wa darasa anataka darasani wakae kwa kuchanganyika.Bado alitandikwa sana fimbo za mgongo.
Kama mzazi ninaguswa sana;ninawiwa kufanya kitu ili walau kupunguza "kipigo" hiki kinachoweza kujenga usugu kwa hawa watoto.Wasiwasi wangu ni kuonekana "naingilia" kazi za watu.Lakini ukweli nashindwa tu kuelezea,lkn hawa watoto wanachapwa sana na fimbo za mianzi.
Katika mazingira kama haya,yenye mchanganyiko wa imani,elimu,malezi na wazazi...Ninaweza kufanyaje??
Tushauriane kwa busara...Asante