SoC01 Ushauri: Jinsi ya kuwasaidia wanawake waliotelekezwa na waume zao kulea watoto

Stories of Change - 2021 Competition

kipenseli2021

JF-Expert Member
Jul 17, 2021
829
781
UTANGULIZI

SMART MOTHER (SM)
,kabla ya kutafuta kwa kina ni jina gani zuri la kumpatia mama huyu ambaye anaangaika na kupambana hili motto wake awezi kupata mahitaji muhimu kama Elimu(Kwenda shule),chakula na mahitaji mengine,huyu ni mama ambaye yeye ndiye kichwa cha Familia anaye ongoza familia peke yake pasipo mwanaume au baba,

Kwa neno la mtaani wanapenda kumuita “SINGLE MOTHER” hila kwangu hile neno alijakaa sawa maana nahisi litazidi kumtia unyonge na ajione kama si kitu kwenye jamii

Lakini pia sio tu “SINGLE MOTHER” bali ni zaidi ya SINGLE MOTHER maana yeye tatizo sio tu kulea mtoto au watoto peke yake pasipo msaada toka kwa baba basi nimuite MAMA ALIYE TELEKEZWA NA BABA LAKINI ANAISHI kwenye mazingira magumu kupambana na hali ya maisha .

Lakini bado nasita naona ni jina gumu sana kwa ushujaa wa huyu mama ambaye anatumia akili kubwa ya UHASIBU japo ajawahi kupitia hata kozi fupi ya UHASIBU lakini ana uwezo wa kutafuta na kupanga matumizi kiasi kidogo cha pesa anacho kipata,huyu mama japo si MCHUMI lakini ana uwezo wa kupanga na kupangua mambo ya UCHUMI,huyu mama japo si MWALIMU lakini ana uwezo mkubwa wa kuwafundisha watoto wake kubeba beseni la vitumbua na kwenda kufanya biashara

Kutokana na sifa nyingi basi naomba nimuhite huyu mama jina zuri ambalo litazidi kumpa nguvu katika utafutaji wa maisha kwa ajili ya familia nimuihite SMART MOTHER

Nikimaanisha kama ifuatavyo SMART MOTHER ni binti au mama ambaye ametelekezwa na mwanaume na kumuachia majukumu ya kulea watoto katika mazingira magumu ,mama huyu ni kati ya umri wa miaka 18 hadi 45.

PENDEKEZO: UANZISHWAJI WA SMART MOTHER EMPOWER PROJECT

SMART MOTHER EMPOWER PROJECT ni mradi ambao unaweza kuendeshwa kwenye vyuo vya ufundi mfano vyuo vya ufundi vilivyopo chini ya Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hili kumpa mafunzo mafupi SMART MOTHER/mama aliye telekezwa na mwanaume na anaye ishi kwenye mazingira magumu kulea watoto wake kumsaidia kupata ELIMU inayo husiana na UFUNDI kwa muda mfupi hili aweze kujiajiri kwa ajili ya kujiongezea kipato.

PENDEKEZO: AINA YA MAFUNZO

Kwa kuwa mama huyu aliye telekezwa na baba/mwanaume anajukumu kubwa la kulea watoto basi napendekeza wapewe mafunzo ambayo ni rahisi kwa waho kujiajiri na baada ya mafunzo wapewe mkopo

  • Ushonaji na Utengnezaji wa batiki (wafundishwe utengenezaji wa bidhaa ndogo ndogo za kushona ambazo utoka kwa haraka na zina mahitaji ya haraka mfano ushonaji wa mabegi,vipochi vya simu,vitambaa,kofia nk)
  • Utengenezaji wa viatu na vito vya kutumia shanga(wafundishiwe utengenezaji wa vitu mbalimbali kama herein,viatu,shanga nk) kwa kutumia shanga,ngozi,mifupa,vifuu vya nazi
  • Upishi wa bites na vyakula mbalimbali (upishi wa vyakula kama keki,bites,vitumbua,chapati) yani vyakula mabayo vinahitaji kwa wingi katika jamii ambayo wataweza kuvisambaza ma ofisini
  • Branding na Packaging –ili kuongeza thamani katika bidhaa zao basi wafunidhwe jinsi ya kufanya branding ya bidhaa zao na jinsi ya kufanya packaging
  • Utengenezaji wa mkaa,sabuni,dawa za kudekia ma sinki ya choo na vitu vidogo vidogo vinavyo tumika sana majumbani
  • Utengenezaji wa majiko ya mkaa/kuchomea nyama,mifuniko ya vyombo,trunka,pawa za mboga,vyungu,vinu,miche nk
MAFUNZO YAO: Yalenge katika utengnezaji wa bidhaa ambazo zinahitaji sana kwenye jamii

WALENGWA:

Sifa za Wanafunzi hawa/Smart Mother

  • Wanawake walio telekezwa pasipo msaada wowote
  • Wanawake walio na watoto wanao ishi kwenye mazingira magumu
  • Umri 18-45
MUDA WA MAFUNZO

Wiki mbili hadi miezi mitatu

BAADA YA KUHITIMU MAFUNZO


Kuwaunganisha na mashirika au serikali kwa ajili ya kupatiwa mikopo

HITIMSHO

Tunaomba wadau mbalimbali waweze kuandaa mafunzo ya aina hii kwa wa mama waliotelekezwa na wanaume hili kuwasaidia kuweza kulea famila.

Imeandaliwa na Kipenseli 2021
 
Tunamsaidia huyu mama aliyetelekezwa kwa kumpa mafunzo na kumchaji alipe Laki Moja mpaka Milioni ? (Tusipoangalia hapo tutakuwa tunajisaidia sisi na sio yeye)

Kwanini msimfunishe bure siku akitajirika ndio awalipe ?, Au na yeye arudishe kwa jamii kwa kufundisha wengine
 
Tunamsaidia huyu mama aliyetelekezwa kwa kumpa mafunzo na kumchaji alipe Laki Moja mpaka Milioni ? (Tusipoangalia hapo tutakuwa tunajisaidia sisi na sio yeye)

Kwanini msimfunishe bure siku akitajirika ndio awalipe ?, Au na yeye arudishe kwa jamii kwa kufundisha wengine
No sio kumchaji pitia
 
No sio kumchaji pitia
Hivi nilikuwa naota au kuna sehemu ulikuwa umeweka laki moja mpaka milioni moja kwa mafunzo na umebadilisha ? Tuambiane Mkuu ama vipi nianze kutafuta daktari wa magonjwa ya kusahau na kusoma vitu ambavyo havipo...
 
Back
Top Bottom