Ushauri: Je kwa hili nakosea?

GDK

Member
Jan 23, 2013
40
8
Mimi ni mhitimu wa UDSM wa zaidi ya miaka sita sasa. Nimefanya kazi kwenye benk na mashirika ya kimataifa kama matatu tofauti mpaka sasa. Kwa sasa nina mwaka sina kazi baada ya mkataba wangu kuisha na hapa mjini (Dar) naishi kwa misheni town pamoja na kikampuni changu ambacho nimeanzisha ingawa bado si cha kutegemea sana na nina familia na mtoto mmoja. Wakati wa majukumu yangu nilibahatika kupata vijisenti nikajenga nyumba nzuri tu Mwanza ambapo nilikuwepo kwa muda mwingi wa ajira yangu kabla ya kuhamia Dar ambapo kwa sasa napanga.Wakati nahama Mwanza kama bahati mama yangu mzazi ambaye nae yupo kwenye mashirika ya kimataifa akapelekwa Mwanza nikaona isiwe tabu akae hapo ingawa ana uwezo wa kujilipia na yeye binafsi Mwana yupo kikazi tu ila nyumbani kabisa Dodoma na hataki kujishughulisha na ujenzi wowote hapo Mwanza.

Kutokana na kuyumba baada ya mkataba wangu kuisha na kupambana hapa na pale. Baadhi ya wadau wamenishauri niiuze nyumba ya Mwanza nije Dar nijipange upya kwa kujenga tena na nibakize ka mtaji ka kulisha familia wakati nasubiri mipango mingine ipatikane. Nikaona ni wazo zuri ukizingatia nina familia na nikaona ninaweza kuiuza na nikafanya uungwana nika mlipia mama apartment ya mwaka mmoja ili ajipange vizuri.

JE NI SAHIHI KWA HILI WAZO? MAANA NAANZA KUPATA HABARI NDUGU WANADAI NATAKA KUMFUKUZA MAMA? JE KUNA ATHARI ZOZOTE ZA TAFSIRI ZA KIJAMII KWA MAAMUZI AMBAYO NAWEZA KUYAFANYA? MAMA HAPENDELEI NIIUZE ETI ITANISAIDIA MBELENI ILA NIMEBANWA KWA SASA WADAU. NAOMBA USHAURI WENU.
 
Mimi ni mhitimu wa UDSM wa zaidi ya miaka sita sasa.Nimefanya kazi kwenye benk na mashirika ya kimataifa kama matatu tofauti mpaka sasa.Kwa sasa nina mwaka sina kazi baada ya mkataba wangu kuisha na hapa mjini (Dar) naishi kwa mesheni town pamoja na kikampuni changu ambacho nimeanzisha ingawa bado si cha kutegemea sana na nina familia na mtoto mmoja.Wakati wa majukumu yangu nilibahatika kupata vijisenti nikajenga nyumba nzuri tu Mwanza ambapo nilikuwepo kwa muda mwingi wa ajira yangu kabla ya kuhamia Dar ambapo kwa sasa napanga.Wakati nahama Mwanza kama bahati mama yangu mzazi ambaye nae yupo kwenye mashirika ya kimataifa akapelekwa Mwanza nikaona isiwe tabu akae hapo ingawa ana uwezo wa kujilipia na yeye binafsi Mwana yupo kikazi tu ila nyumbani kabisa Dodoma na hataki kujishughulisha na ujenzi wowotw hapo Mwanza.

Kutokana na kuyumba baada ya mkataba wangu kuisha na kupambana hapa na pale.Baadhi ya wadau wamenishauri niiuze nyumba ya Mwanza nije Dar nijipange upya kwa kujenga tena na nibakize ka mtaji ka kulisha familia wakati nasubili mipango mingine ipatikane.Nikaona ni wazo zuri ukizingatia nina familia na nikaona ninaweza kuiuza na nikafanya uungwana nika mlipia mama apartment ya mwaka mmoja ili ajipange vizuri.JE NI SAHIHI KWA HILI WAZO? MAANA NAANZA KUPATA HABARI NDUGU WANADAI NATAKA KUMFUKUZA MAMA? JE KUNA ATHARI ZOZTE ZA TAFSIRI ZA KIJAMII KWA MAAMUZI AMBAYO NAWEZA KUYAFANYA? MAMA HAPENDELEI NIIUZE ETI ITANISAIDIA MBELENI ILA NIMEBANWA KWA SASA WADAU. NAOMBA USHAURI WENU.

kila mtu anakumbwa na matatizo kaka, kukimbilia kuuza nyumba uliyojenga kwa kisingizio kuwa unataka kutatua matatizo au tatizo ulilonalo si sahihi hata kidogo cuz unaweza kuuza nyumba yako na matatizo yakaendelea kukukabili vile vile sasa sijui hapo utauza nini tena? ni vyema mtu unapokabiliwa na matatizo ukatafuta means ya kukabiliana nayo na sio kuuza asset yako uliyokwisha jiwekea........nafikiri unatakiwa kuchekecha kichwa zaidi ili kukabiliana na changamoto inayokuandama kuliko kufikiria nina kitu fulani nataka nikiuze kinisaidie kutatua tatizo langu, usitafute jibu jepesi kwa swali gumu unalotakiwa kulijibu kiufasaha mkuu
 
samahan mkuu ni nyumba ya aina gan uliyojenga mwanza ambayo ukiiuza utakuja jenga Dar na hapo hapo utamlipia mama yako apartment na kuongeza mtaji kwny shughuli zako isije ikawa kweli unataka mtoa tu,alf ukapata Lana usijenge tena
 
kibol umempa jibu sahh kabsaa usiuze nyumba kaka vumilia hayo matatizo ni mapito utauza leo ml 20 kesho unapata ml 100 kaza but hii ndo dsm usitake kuishi kama wazir kwakuuza mali yako

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hiyo nyumba ya mwanza inathamani ya sh ngapi?. Katika mchanganuo umesema unataka uanze kujenga dar,pili umpangishie hela mama yako na mwisho ubakize kiasi kidogo kwa ajil ya familia. Umeshaangalia gharama za ujenzi wa nyumba hapa dar? USHAURI;Tumia hiyo asset ya nyumba kuomba mkopo kwenye mabenki naamini utapata ili uendeleze hiyo company yako.
 
Usiuze utalaanika hata kama ni yako

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
kibol umempa jibu sahh kabsaa usiuze nyumba kaka vumilia hayo matatizo ni mapito utauza leo ml 20 kesho unapata ml 100 kaza but hii ndo dsm usitake kuishi kama wazir kwakuuza mali yako

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

hapo kwenye blue ndipo nilipopapenda sana mkuu, tunapopata matatizo lazima tukabiliane nayo barabara
 
Nashukuruni sana wadau.Gharama za ujenzi dar nilishafanya utafiti wadau na thamani ya nyumba kwa sasa ni 140mil kutokana na evaluators ambao wamefanya hii kazi January mwaka huu.Iko pazuri sana sababu nilimnunua mtu kipindi hicho 40mil (2009) na nikaiweka kisasa sababu ilikuwa ya kizamani.Kiongozi apartment Mwanza nzuri 500,000 kwa mwezi so 6mil kwa mwaka.Nyumba na kiwanja dar ka 90mil na 25mil nipige jeck kampuni niendelee na ujasiliamali niachane na mambo ya kuendelea kutafuta kazi.Ila ushuri wowote nauchukua na ntaufikiria wadau.
 
Ungekuwa nazo 3 ningekushauri uza tena kwa faida lakini iyo moja do not dare na kama ishu ni gharama za kupanga mjini nenda mwanza ukapige mzigo huko
 
Mimi ni mhitimu wa UDSM wa zaidi ya miaka sita sasa.Nimefanya kazi kwenye benk na mashirika ya kimataifa kama matatu tofauti mpaka sasa.Kwa sasa nina mwaka sina kazi baada ya mkataba wangu kuisha na hapa mjini (Dar) naishi kwa mesheni town pamoja na kikampuni changu ambacho nimeanzisha ingawa bado si cha kutegemea sana na nina familia na mtoto mmoja.Wakati wa majukumu yangu nilibahatika kupata vijisenti nikajenga nyumba nzuri tu Mwanza ambapo nilikuwepo kwa muda mwingi wa ajira yangu kabla ya kuhamia Dar ambapo kwa sasa napanga.Wakati nahama Mwanza kama bahati mama yangu mzazi ambaye nae yupo kwenye mashirika ya kimataifa akapelekwa Mwanza nikaona isiwe tabu akae hapo ingawa ana uwezo wa kujilipia na yeye binafsi Mwana yupo kikazi tu ila nyumbani kabisa Dodoma na hataki kujishughulisha na ujenzi wowotw hapo Mwanza.

Kutokana na kuyumba baada ya mkataba wangu kuisha na kupambana hapa na pale.Baadhi ya wadau wamenishauri niiuze nyumba ya Mwanza nije Dar nijipange upya kwa kujenga tena na nibakize ka mtaji ka kulisha familia wakati nasubili mipango mingine ipatikane.Nikaona ni wazo zuri ukizingatia nina familia na nikaona ninaweza kuiuza na nikafanya uungwana nika mlipia mama apartment ya mwaka mmoja ili ajipange vizuri.JE NI SAHIHI KWA HILI WAZO? MAANA NAANZA KUPATA HABARI NDUGU WANADAI NATAKA KUMFUKUZA MAMA? JE KUNA ATHARI ZOZTE ZA TAFSIRI ZA KIJAMII KWA MAAMUZI AMBAYO NAWEZA KUYAFANYA? MAMA HAPENDELEI NIIUZE ETI ITANISAIDIA MBELENI ILA NIMEBANWA KWA SASA WADAU. NAOMBA USHAURI WENU.

kama una uhakika na ujasiliamali unaotaka kuuanza,usiuze hio nyumba bali ifanye dhamana ya kuchukulia mkopo....
 
kuuza Mwanza na kujenga Dar yataka mahesabu makali sana, ushauri wangu uza kama mahesabu yako yanakubali ila kua makini.
 
kama utapata mteja wa kummuzia hata 120mil uza tuu,halafu ukiuuza usikimbilie kujenga nyingine bali nunua kiwanja pekee huku ukifanya miradi ya kuongeza kipato zaidi.Mama yako mueleweshe malengo yako
 
Kwa alivyojieleza ni kijana bado na watoto wadogo na mwenza. Angekuwa single tungemshauri akakae mwanza ale huo mshahara wa mama anaekaa kwenye asset aliyochuma na mkewe, lakini vilevile ameona biashara hapa Dar na sio mwanza. Situation yake sio ngeni kwa watu wa private sector lazima uwekeze harakaharaka kwenye kitu kitachokufaa kazi ikiisha. Inashangaza huyu mama kutokuwa sensitive na mwanae, pengine huwezi mwambia alipe kodi lakini alipaswa kukupatia fedha hata kama hailingani na kodi. Pili kama mzazi alipaswa kukuuliza unaishije nje ya ajira na kama anaweza kukukopesha mtaji ila naona huyu ni wale wanaoona ndio muda wakufaidi vya mwanae at expence of vijukuu na mkwe! Ushauri wangu uliza nyumba huku dar iliyokamili na mfiungie safari mwanza umweleze kuwa huna jinsi inabidi nyumba uuze na utampatia kodi ya nyumba ingine. Mueleze umeishapata ya kununua Dar na salio uinue biashara yako, hapa inabidi uwe ngangari au uende na mtu mwenye kukuelewa nia yako. Hao ndugu hayawahusu la wangekupa mtaji ili uinue biashara yako. Mimi nilikuwa nawekeza kwenye viwanja na kuviuza, ila tu isijekuwa unauza na kutanua utajuta. Maisha ukiishakuwa na familia usichanganye asset kubwa na ukoo utaleta ugomvi bure. Uombe sana Mungu akusimamie.
 
Kama hesabu zako zinakaa vyema uza tu, kwani si ulijenga mwenyewe, hao ndugu walikusaidia kujenga au kwa hali uliyo nayo sasa hivi mama na ndugu zako wanakusaidiaje?
Ni kweli mama anasema itakusaidia baadaye, lakini wakati wenyewe ndio huu au mama kama anakupenda sana basi akubali kukulipa kodi si yupo kazini? au kama hata weza basi akubali kupanga nyumba nyingine then hiyo upangishe hapo atakuwa ameosha anajali na sio kusema itakusaidia baadaye wakati sasa hivi unakufa njaa.
 
Wadau naombeni ushauri wa mwisho kabla ya kufanya maamuzi magumu? niko nje ya mji kwa sasa ila hali yangu ni mbaya sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom