Mimi ni mhitimu wa UDSM wa zaidi ya miaka sita sasa. Nimefanya kazi kwenye benk na mashirika ya kimataifa kama matatu tofauti mpaka sasa. Kwa sasa nina mwaka sina kazi baada ya mkataba wangu kuisha na hapa mjini (Dar) naishi kwa misheni town pamoja na kikampuni changu ambacho nimeanzisha ingawa bado si cha kutegemea sana na nina familia na mtoto mmoja. Wakati wa majukumu yangu nilibahatika kupata vijisenti nikajenga nyumba nzuri tu Mwanza ambapo nilikuwepo kwa muda mwingi wa ajira yangu kabla ya kuhamia Dar ambapo kwa sasa napanga.Wakati nahama Mwanza kama bahati mama yangu mzazi ambaye nae yupo kwenye mashirika ya kimataifa akapelekwa Mwanza nikaona isiwe tabu akae hapo ingawa ana uwezo wa kujilipia na yeye binafsi Mwana yupo kikazi tu ila nyumbani kabisa Dodoma na hataki kujishughulisha na ujenzi wowote hapo Mwanza.
Kutokana na kuyumba baada ya mkataba wangu kuisha na kupambana hapa na pale. Baadhi ya wadau wamenishauri niiuze nyumba ya Mwanza nije Dar nijipange upya kwa kujenga tena na nibakize ka mtaji ka kulisha familia wakati nasubiri mipango mingine ipatikane. Nikaona ni wazo zuri ukizingatia nina familia na nikaona ninaweza kuiuza na nikafanya uungwana nika mlipia mama apartment ya mwaka mmoja ili ajipange vizuri.
JE NI SAHIHI KWA HILI WAZO? MAANA NAANZA KUPATA HABARI NDUGU WANADAI NATAKA KUMFUKUZA MAMA? JE KUNA ATHARI ZOZOTE ZA TAFSIRI ZA KIJAMII KWA MAAMUZI AMBAYO NAWEZA KUYAFANYA? MAMA HAPENDELEI NIIUZE ETI ITANISAIDIA MBELENI ILA NIMEBANWA KWA SASA WADAU. NAOMBA USHAURI WENU.