Ushauri jamani... Mtoto wa kutelekezwa ananikosesha amani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri jamani... Mtoto wa kutelekezwa ananikosesha amani!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by futikamba, Aug 20, 2011.

 1. futikamba

  futikamba JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2011
  Joined: Jan 18, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wapendwa MMU,

  Salaam kwenu wote in the name of love.
  Wadau, kuna kijana mwenzetu mmoja amekumbwa na mkasa mzito saana. Miaka kama 2 imepita, akiwa kwenye daladala aliachiwa mtoto na mwanamke aliekuwa amevaa hijabu mpaka machoni kama wale mataleban. Basi, huyu kaka yetu ikabidi amchukue huyu kiumbe na kuishi/kumlea kama mwanae nae. Sasa juzijuzi mwanamke mmoja akajitokeza akidai kwamba yule ni mwanae. Mshkaji ni bachelor hana mke. Sasa yeye anasema anampenda sana huyo mtoto na hataki kumkosa, huku mwanamke anamsumbua. Leo ameniambia amehama nyumba sababu ya usumbufu. Tusaidiane mawazo, je afanye nini ili aweze kujiridhisha?
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Huyo mwanamke apelekwe Polisi tu
   
 3. Yasmin

  Yasmin JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  waoo guardian angle!
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Amwambie huyo mwanamke kama kweli ndie mama mzazi wa mtoto na anamtaka mtoto aanzie kwa kujireport police...alafu aandae pesa ya kwenda kufanya DNA test kuhakikisha ndio yeye...ikishajulikana aandae kifungu alichotumia mshkaji kumlea mtoto tangu siku hizo mpaka leo hii (mahesabu apange mwenyewe hata akiyatripple hapa labda anaweza akawa mdogo) alafu akishampa hiyo list ya majukumu atafute mwanasheria kujua kama kuna namna anaweza kumaintain mahusiano na huyo mtoto hata kama mama yake ataruhusiwa kumchukua.

  Mimi ningekua judge nikaletewa kesi kama hii huyo mwanamke angeipata... anamwachia mtu asiyemfahamu ni wa aina gani mtoto kwenye dalala alafu baada ya miaka miwili anakuja kumchukua kama vile ni KITU ?!

  Ohh alafu naomba kuuliza...amempatapataje huyo rafiki yako?!Maana kwa Bongo sidhani kama ni rahisi kiasi hicho kumpata mtu usiyemfahamu!!
   
 5. bht

  bht JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  anamkimbiaje mtu ambaye hana uhakika kama ndo mama wa mtoto? Na atakimbia mpaka lini?

  Cha kufanya ni kuishughulikia hili suala kisheria zaidi, atoe taarifa police na mengine yafuate toka hapo


  Inawezekana kabisa hata akawa muongo tu, kachorewa ramani na wanaojua ukweli kuhusu huyo mtoto na sasa wanataka kumfix huyo mlezi wa mtoto.

  Attachment yake kwa mtot naweza kumwelewa kabisa, maana miaka miwili si haba, mapenzi yamejengeka kwa mtoto, lakini hili lisimpumbaze, afate taratibu za kisheria.

  Futikamba, huyo mtoto ana umri gani sasa?
   
 6. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  police nao wanaweza mgeuzia kibao kwa nini hakureport, swala gumu, ila bora tu uende police
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  huyu kaka naye anamakosa tena makubwa sn sbb alipaswa kuripoti polisi mara baada ya kugundua kw kaachiwa mtoto na mama keshatimua kwani hy mama anaweza akawa aliripoti kw kapoteza mtoto akakaa kimya miaka 2 then kaibuka na kujidai kampata mwizi wake, kijana atalipishwa fine ya kutosha+jela+ viboko.
   
 8. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huyo mama achukuliwe DNA kama alivyosema Lizzy, kisha aangaliwe history yake asije akawa na kichaa cha msimu, maana kutelekeza mtoto si issue ndogo
   
 9. bryleen

  bryleen Member

  #9
  Aug 20, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli huyo mama kiboko zaidi hapo ni DNA ndio itamaliza kila k2 hakuna kingne.ila kama ni wke kweli cdhani kama hata huyo mtoto atampenda mama yake
   
 10. G

  Gobe Isiah Member

  #10
  Aug 20, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi napata mashaka kidogo!?huyo jamaa isijekuwa wanafahamiana na huyo mama au alimpa mimba mama huyo wa watu akataka kukimbia ikabidi atumie njia ya kumpa mtoto wake kwenye dala dala alafu baadae akamtaarifu kuwa huyo ni mwanao!!kwa hali ya kawaida si rahis mtoto wa kiume aachiwe mtoto then asiripot mahali popote na wakati yeye ni bachellor-!'?? Mimi nahis wanafahamiana tu! So kama vipi wakubaliane tu jinsi ya kumlea mtoto wao akue vzr huku akimjua baba na mama halisi!
   
 11. m

  muhanga JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ahamie kwa waeskimo au amazon labda huko hatamfuata lakini hapa hapa dar lazima atampata tu.
   
 12. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kuna uwezekano mkubwa huyo mama alikuwa anajua anachokifanya miaka 2 iliyopita. Kuna uwezekano alikuwa anafuatilia kwa karibu maendeleo ya mtoto.

  Unless otherwise kama rafiki yetu alihusisha vyombo vya usalama wakati huo yaani kupata haki za kisheria kulea mtoto...Mama mtoto .anatakiwa kwanza akapumzishwe jela Segerea kwa kosa la kutupa mtoto kabla hajasikilizwa dai lake la mtoto..
   
 13. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,163
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  Hata kama itathibitika kuwa yeye ndo mama halisi bado naona hastaili kupewa mtoto! Awe anakuja kumsalimia hapo kwa jamaa, sina imani na akili za huyo mama.
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  umeona gaga eeh! Huyo mkaka kama hakureport nae ana makosa. Angemweleza hata mjumbe wake kama anaogopa police.
   
 15. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Waende wakapime DNA kama ni mama wa mtoto kweli alipe gharama za matumizi ya hiyo miaka miwili halafu ampe huyo mama mtoto wake. Atakimbia mpaka lini?
   
 16. m

  mtotomzuri Member

  #16
  Aug 20, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mh,whatever the case,i think u should go to police,hata kama hukuripoti mwanzoni kama uliachiwa mtoto bado police watakusikiliza tu kwa sababu mtoto umemtunza na wenyewe wana njia zao za kujua kama huyo mtot hapo alipo yupo kwny mikono salama au vp,huyo mama yawezekana hana ugonjwa wa akili wala nini,go to police mambo yatakuwa shwari tu kwani hata Mungu amekuona jinsi unavyomtunza huyo mtoto,kumkimbia huyo mama haina maana kwani atakutafuta popote ulipo,itakuwa ana control maisha yako kwani kila utachofanya utakuwa unamfikiria yeye tu which is not gud,kukata mzizi wa fitina just go to police!
   
 17. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #17
  Aug 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Hii story inasikitisha saana... ila tu imenipa maswali mengi saana ambayo naona kama yamepelekea kua na gaps nyingi katika the whole issue... Nashanga saana kitendo cha huyo mwanamke kutelekeza mtoto katika dala dala alafu at the end akajua ni nani alimchukua... maana anaefanya hivo anapokua katika hio situation hujiweka mbali wala hanusi kwa hofu ya kukamatwa.... Kuna hii pia ya kusema huyu jamaa ni barchelor - alafu akaweza lea huyo mtoto for two years bila kuoa... does it mean kua ana mfanya kazi kwake... How did he manage?? (naomba kujuzwa if you donn't mind) for mpaka kalea huyo mtoto ni dhahiri alikua ni mdogo mno ama kichanga....
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Aug 21, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  This story sounds a bit far-fetched but for now I'll grant you the benefit of the doubt. Kwanza unasema ilikuwa kwenye daladala ndipo huyo mwanamke akamwachia jamaa huyo mtoto. Alimwachia kwa minajii ipi? Walikuwa wamekaa pamoja? Walishuka kituo kimoja? Kama hawakushuka kituo kimoja basi huyo mwanamke itakuwa alishuka kwanza.

  Sasa wakati huyo mwanamke anashuka jamaa hakupiga kelele kuwa huyo mwanamke anaacha mwanae huku nyuma? Hakumwambia konda wala dereva kuwa kuna dada au mama kaacha mwanae? Na hiyo daladala haikuwa na watu wengine? Manake nijuavyo daladala zetu mara nyingi sana huwaga haziko tupu na hata kama ziko tupu lazima dereva na konda watakuwepo.

  Yaani yeye anaachiwa mtoto ambaye hata hamjui halafu anakaa kimya tu na kumchukua huyo mtoto na kwenda kuishi naye na kumlea kwa miaka yote hiyo? Je alifanya jitihada zozote za kwenda polisi baada ya huyo mwanamke kushuka?
  The way you have presented the story just doesn't sound plausible!! I would freak out if somebody were to just leave their child with me and got off the bus just like that. I would scream to high heaven to bring it to the attention of everyone in the bus and my next stop would be at the police station and not my house.

  Huyo kaka hana ndugu na jamaa? Na kama anao, je, walimuuliza huyo mtoto ni wa nani na yeye aliwajibu nini? Na kama walimuuliza, hakuna hata mmoja aliyemwambia kwamba itakuwa ni vyema akienda kuripoti polisi?

  Utaleaje mtoto uliyeachiwa kwenye daladala kama vile ni wako? Mtu gani wa kawaida anaweza kufanya hivyo? It is just not making sense.

  Huyo mwanamke kampatapataje huyo jamaa? Na huyo jamaa hajamhoji huyo mwanamke kwa nini alimtelekeza huyo mwanae kwenye daladala? Huu mkasa mzima hauingii akilini mwangu kabisa.
   
 19. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hii news ni ngumu kuikubali!sidhan kama utaweza kuachiwa mtoto ukakubali ki rahis rahis tu hv hv!ingebd aende kwny vyombo vya habar,polis,ustaw wa jamii ili kujarib kusaka wazaz wake!akishindwa ndio akae nae!manake angekufa jamaa yako huyo angempeleka wap?binadam sio kuku unawwza kukaa nae hata kama hujui katokea wap!
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Aug 21, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Si ndio hapo! Yaani mtu unaachiwa mtoto na mtu hata usiyemjua, tena kwenye daladala halafu na wewe unaamua kumchukua huyo mtoto na kwenda kumlea kwako kama vile ni wako....kwangu haingii akilini kabisa kwa mtu mzima mwenye akili timamu kufanya kitu kama hicho.

  Unajua watoto wana mahitaji mengi sana. Kuna doctor visits kwa mfano, ambazo mzazi au mlezi unatakiwa kuzifanya kufuatilia afya na makuzi ya mtoto. Sasa huyu jamaa sijui yeye alifanyafanyaje tu. Sijui alienda na kuanzisha faili jipya la huyo mtoto au sijui hata hakuwa anampeleka huko kwa daktari.

  Halafu eti baada ya miaka 2 anajitokeza mwanamke na kudai kuwa huyo mtoto ni wake? WTF??
   
Loading...