Ushauri: Iundwe bodi ya mikopo ya rufaa kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili kupunguza urasimu

Afrikasana

JF-Expert Member
Oct 27, 2021
320
283
Jana niliandika uzi nikimuomba Mh. Rais aingilie kati suala la mikopo ya elimu ya juu.

Leo eti wamefungua dirisha ili watu wakate rufaa. Hivi nyie watu wa bodi aliyewaroga ni nani?

Mtu ameomba mkopo tangu mwaka wa kwanza mathalani,mmemnyima akakata rufaa mkamnyima.

Akaja mwaka wa pili akaomba tena mnamnyima tena mnampa fursa ya kukata rufaa hivi mnafikiri kwa kina kweli?

Mtu ambaye sababu zake nizile zile kila mara mnamnyima. Mtu niyatima ameambatanisha cheti cha kifo na kimethibitishwa VIZAZI NA VIFO.

Mnamgomea mara tatu na hamumuambii mapungufu yake,mnamuambia tena akate rufaa. Au mnataka watu wakafukue maiti za wazazi wao waje nazo hapo ndio mtaamini kama niyatima?

Mnamkubaliaje mtu akate rufaa kwasababu zilezile ambazo mnazikataa kila mara?
Hivi hii nchi haina wasomi wanaofikiria zaidi ya hao hapo HESLB?

Basi iundwe bodi ya mikopo inayoshuhulikia rufaa za waombaji na sio bodi hiyo ya blaablaa inayokusanya fedha kibao za kulipia fomu kwaajili ya kuombea mkopo na hawawapi watu
Kama ikiundwa bodi hiyo ya rufaa itakua kama chombo cha kufanya tathmini juu ya uzembe, ubinafsi,kutowajibika,kibri na kukosa uzalendo kwa hiyo bodi ya wakandamizaji.
Tanzania ni yamaskini na matajiri,wenye wazazi na yatima pia.

Mh. Rais hiyo bodi isambaratishe,wakurugenzi wabadilishe, ahsante
 
Pole sana mkuu. Hao bodi ya mikopo wamekaatu hapo kufanya wanavyoona wao inafaa hawawajali wahitaji.
So far hakuna anayewagusa kwasababu bodi imekua kama chanzo cha mapato na sio kuwainua watanzania wasio jiweza

Ila wazo la kuundwa kamati ya rufaa ambayo itapitia malalamiko ya waliokosa niwazo zuri sana.
Huo ndio uzuri wa jamiiforum maana hoja hutolewa na masuluhisho mbalimbali pia yanapatikana
 
Naona kama kuna ubaguzi na unyanyasaji mkubwa sana ndani ya bodi.
Wamekua hawasaidii baadhi ya wahitaji na majibu yao nimabovu.
Ukiingia ofisini wanaangalia kila pembe shida yao ni rushwa.
Matajiri wametoa rushwa wanapewa hela masikini na yatima wanataabika
 
Bodi ya mkopo ni jipu la kutumbuliwa ,madudu mengi mno
Huyo mkurugenzi wa mikopo uchambuzi na upangaji mikopo Veronica Nyahende anafaa kuondolewa hata kabla jua halijazama.
Rushwa,majibu mabaya,uongo uongo sasa hata anaongozwa na ubinafsi hata yatima hawajali na maskini. Lakini kama ana watoto yatakuja kukuta kizazi chake
 
Pole sana mkuu. Hao bodi ya mikopo wamekaatu hapo kufanya wanavyoona wao inafaa hawawajali wahitaji.
So far hakuna anayewagusa kwasababu bodi imekua kama chanzo cha mapato na sio kuwainua watanzania wasio jiweza

Ila wazo la kuundwa kamati ya rufaa ambayo itapitia malalamiko ya waliokosa niwazo zuri sana.
Huo ndio uzuri wa jamiiforum maana hoja hutolewa na masuluhisho mbalimbali pia yanapatikana
Hilo limethibitishwa na CAG hivyo mkurugenzi wa bodi aendelee kujitathmini
 
Back
Top Bottom