Ushauri: ITV, Channel TEN na EATV, nunueni mitambo yenu ili mrushe Live matangazo ya wagombea urais

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Vituo vya television vya ITV, Channel TEN na EATV hivi hawaoni aibu 'kuiba' matangazo ya watia nia ya kugombea urais? Mpaka sasa vituo hivyo vimekuwa vikichukua matangazo ya vituo vingine kisha kuita live. Hivi Mengi anakosa mitambo yake mpaka anyonye matangazo AZAM TV au Clouds? Ni aibu kubwa sana.

Mkutano wa Lowassa vituo vilivyorusha live kutoka Arusha ni Clouds TV na Azam huku ITV, Channel Ten na EATV wakichukua katika vituo hivyo.

Wakati wa Wassira waliokuwa wakirusha live ni Star tv huku ITV na Channel Ten wakinyonya Star Tv..

Mkutano wa Mwigulu ulirushwa na AZAM TV na Star Tv huku ITV na channel Ten, EATV wakichukua Star Tv.

Hii ni aibu kubwa kwa ITV kutotumia mitambo yake kurusha Live, kama wanapewa fedha ya crew n.k. wanaitafuna bure.
 
Hapana mkuu,hii ni kawaida sehemu zote. Ni makubaliano tu ya kibiashara. Labda waichukue km changamoto kwao kuwa inabidi wajipange na wawe na uwezo wa kurusha live kutoka hata sehemu 3-4 tofauti kwa wakati mmoja
 
Mleta mada nafikiri uelewa wako kuhusu masuala ya mawasiliano na hasa broadcasting, yako chini ya kiwango cha wastani lkn natumaini michango ya wadau humu JF imekusaidia kuelewa zaidi.
 
Mleta mada nafikiri uelewa wako kuhusu masuala ya mawasiliano na hasa broadcasting, yako chini ya kiwango cha wastani lkn natumaini michango ya wadau humu JF imekusaidia kuelewa zaidi.

Ipo siku utajua ninamaanisha nini. Ulitazama ubora wa matangazo kutoka arusha kupitia ITV? Kuna wakati walihaa kubadilisha channel kutoka Azam to Clouds.

Ubora wa ITV unajulikana na kinachorushwa ni tofauti kabisa. cc to idoyo wale wa UEFA ubora ni super no 1 utalinganisha na live ya Clouds tv, wao link wanatumia internet ya 2G kupeleka picha.
 
Huwezi linganisha ITV na Clouds, ITV wapo miaka mingi. Nguvu yao ni kubwa sana, wana mitambo mingi kuliko Clouds TV leo! ITV ni ni zaidi ya TV ya taifa ndio tofauti na tasisi za serekali hakuna sehemu TBC ina angaliwa na Clouds TV, hata bar taarifa ya habari za hizo channel zote ulizo taja haziangaliwagi ITV ni super brand.
 
Mleta mada, shida yako nini? Kwani matangazo si unayapata? Sasa wakijiunga na steshen nyinyine wewe inakuuma nini? Jaribu kuangalia habari za kimataifa steshen yoyote, zooote zinachukua taarifa kutoka BBC, Aljazeera, n.k. Kwa hiyo ulitaka na hiyo waende wapeleke mitambo?
 
Ipo siku utajua ninamaanisha nini. Ulitazama ubora wa matangazo kutoka arusha kupitia ITV? Kuna wakati walihaa kubadilisha channel kutoka Azam to Clouds. Ubora wa ITV unajulikana na kinachorushwa ni tofauti kabisa. cc to idoyo wale wa UEFA ubora ni super no 1 utalinganisha na live ya Clouds TV, wao link wanatumia internet ya 2G kupeleka picha.
Unaongelea ubora au kuchukua matangazo kutoka chaneli nyingine?
 
Mwaka 2004 itv walirusha matangazo ya moja kwa moja toka uwanja wa Taifa na yalionekanekana africa mashariki na kati na yalihudhuliwa na wakuu wa nchi za africa mashariki.
 
Vituo vya television vya ITV, Channel TEN na EATV hivi hawaoni aibu 'kuiba' matangazo ya watia nia ya kugombea urais? Mpaka sasa vituo hivyo vimekuwa vikichukua matangazo ya vituo vingine kisha kuita live. Hivi Mengi anakosa mitambo yake mpaka anyonye matangazo AZAM TV au Clouds? Ni aibu kubwa sana.

Ninge comments sana,maana kama mleta Post hata maana ya Live inakupa shida,basi hata watu wakueleze vipi huwezi kuelewa.

Ila tambua kwamba CCN na hata Aljazeera na BBC kuna matangazo mengi tu wanajiunga na vituo vingine kwenye baadhi ya matukio.Hakuna chombo chochote duniani cha habari duniani chenye Coverage sehem zote.Hata robo ya dunia hakuna.lazima kipitia baadhi ya channels nyingine.
Na yapo matangazo ya moja kwa moja pia ambayo ITV huonyesha live na vyombo vinginge kushika kupitia kwake.

Sasa sijui shida yako ni kupata habari,au unaleta Siasa ndani ya vyombo vya Habari
 
victor moshi ITV hawajawahi kua na OB van, huazima toka Mlimani TV, issue ya Lowassa na Arusha, Azam TV alikua official Media patner, vitio vyote vilichkua feed toka Azam, wacha kupotosha!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom