Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,530
- 217,797
Huu ni ushauri ninaoupeleka kwenye ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mh John Mnyika kwamba wagombea watakapozichukua fomu hizo kutoka kwenye ofisi za Tume ama kwa Wakurugenzi baada ya kuzijaza basi ni vema zikahakikiwa na ofisi kubwa kabisa za kanda ili kuondoa uwezekano wowote wa kukataliwa na maofisa wa Tume ambao wengi ni makada wa ccm.
Baada ya kuhakikiwa zitolewe nakala za kumbukumbu na kuhifadhiwa ili kuondoa uwezekano wa maofisa wa Tume kuongeza uchafu wao , utaratibu huu una gharama na usumbufu kidogo lakini ni muhimu kufanyika ili kuhakikisha ule mpango wa Chadema kutwaa nchi na hatimaye kuwakata minyororo ya utumwa watanzania unatimia .
CCM haina uwezo wa kushinda uchaguzi kwenye sanduku la kura , mbinu pekee wanayoweza kuitumia ni kuhujumu wagombea wa Chadema kwa kuwapora fomu baada ya kuwateka ama kukataa kupokea fomu zao kwa njia ya kishamba ya wapokeaji kukimbia ofisi zao ama kutengeneza makosa kwa kusingizia chochote kile
Tukiweza kuwadhibiti katika mambo haya hawa watu ni wepesi kuliko pamba, hawaungwi mkono na wananchi, na hata hao migambo wamechoka kutumika kudhulumu haki za raia, tunaishi nao mitaani na tunajua wanachokisema.
Mungu ibariki CHADEMA