Uchaguzi 2020 Ushauri: Ili kuepuka hujuma Fomu zote za wagombea ubunge na udiwani wa CHADEMA zipitie ofisi za kanda kuhakikiwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
91,182
2,000
Huu ni ushauri ninaoupeleka kwenye ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mh John Mnyika kwamba wagombea watakapozichukua fomu hizo kutoka kwenye ofisi za Tume ama kwa Wakurugenzi baada ya kuzijaza basi ni vema zikahakikiwa na ofisi kubwa kabisa za kanda ili kuondoa uwezekano wowote wa kukataliwa na maofisa wa Tume ambao wengi ni makada wa ccm.

Baada ya kuhakikiwa zitolewe nakala za kumbukumbu na kuhifadhiwa ili kuondoa uwezekano wa maofisa wa Tume kuongeza uchafu wao , utaratibu huu una gharama na usumbufu kidogo lakini ni muhimu kufanyika ili kuhakikisha ule mpango wa Chadema kutwaa nchi na hatimaye kuwakata minyororo ya utumwa watanzania unatimia .

CCM haina uwezo wa kushinda uchaguzi kwenye sanduku la kura , mbinu pekee wanayoweza kuitumia ni kuhujumu wagombea wa Chadema kwa kuwapora fomu baada ya kuwateka ama kukataa kupokea fomu zao kwa njia ya kishamba ya wapokeaji kukimbia ofisi zao ama kutengeneza makosa kwa kusingizia chochote kile

Tukiweza kuwadhibiti katika mambo haya hawa watu ni wepesi kuliko pamba, hawaungwi mkono na wananchi, na hata hao migambo wamechoka kutumika kudhulumu haki za raia, tunaishi nao mitaani na tunajua wanachokisema.

Mungu ibariki CHADEMA
 

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
25,337
2,000
Hoja yangu si kutokujua kujaza fomu , ni kuepuka hujuma za kibwege za makada wa ccm
Hoja yako imekuja baada ya kukithiri mapingamizi yanayotokana na makosa yanayofanywa na wagombea wenu makosa ya wazi ambayo ni dhahiri kwamba jamaa hawawezi kujaza hizo fomu hivyo ili kuficha hiyo aibu ukaona Chama kiwasaidie kwakuwa hawajiwezi na mtaambulia aibu kwa Mara nyingine tena.

Hitimisho hapa ni kuwa wagombea wenu hawajiwezi hata kujaza fomu tu.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
91,182
2,000
Kumekucha !
Subpost 2 - Ndio Kumekucha. Leo tar 12.08.2020 Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Cham ( 640 X 640 ).jpg
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
25,999
2,000
Sasa hivi ni kuwabana...mbinu zao ni zilezile.
1. Kuwazuia mawakala wa CDM nje hadi saa nne ama tano ili humo ndani wafanye yao
2. Kuwateka wagombea wa CDM siku moja kabla ya uchaguzi
3. Kuwapora form wakiwa njiani wakati wanazirejesha
4. Ku edit form za CDM zionekane na mapungufu ili waondolewe
5. Kitumia police kuingiza sanduku ndani ya kituo ambalo lina kura tayari zilizokwisha kupigwa
6. Kumshikisha rushwa wakala wa CDM ili wafanye yao ( vituo vinatakiwa kuwa na camera)
7. Kuanzisha fujo ili Police wawaondoe wananchi wote kituoni then wafanye yao
8. Kumpa chakula wakala wa CDM kilicho na dawa za kumlewesha kidogo na analala kama masaa mawili ili wafanye yao
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,417
2,000
Hoja yako imekuja baada ya kukithiri mapingamizi yanayotokana na makosa yanayofanywa na wagombea wenu makosa ya wazi ambayo ni dhahiri kwamba jamaa hawawezi kujaza hizo fomu hivyo ili kuficha hiyo aibu ukaona Chama kiwasaidie kwakuwa hawajiwezi na mtaambulia aibu kwa Mara nyingine tena.

Hitimisho hapa ni kuwa wagombea wenu hawajiwezi hata kujaza fomu tu.

Acha utoto dogo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom