Ushauri: IGP Mangu badilisha sare za polisi ziwe za kimbinu zaidi

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,397
Jeshi la polisi linakabiliana na changamoto mbalimbali na kila kukicha kunatokea changamoto mpya.

Kuna kila sababu ya jeshi hilo sasa kubadili sare za vijana wake na ziwe za kimbinu (combat trousers) zaidi yaani kuwa na mifuko mingi na pia kuwa za kimbinu zaidi (tactical) ili kuweza kubeba visaidia kazi kama spray, touch, virungu na mikanda yenye mikoba.

Pia umefika wakati kwa polisi wa kike kuachana na sare za sketi ambazo ni kikwazo katika utendaji wa kazi zao kimbinu iwe vituoni au kwenye malindo.

Polisi wa Tanzania wana uhuru wa kuchagua ni aina gani ya sare wanahitaji kuzivaa kulingana na hali ya hewa pia kwani kuna wakati wanaweza kuvaa fulana tu kwa juu na suruali zao zikawa za kawaida.

Pia ni kutokana na mazingira halisi na sio kila mara kuonekana wapo more relaxed yaani hawana kazi.

bh_performance_pant_khk_16.jpg

womens_taclite_1_1.jpg

Sare ya polisi wa kike inakuwa inaleta maudhui halisi ya kazi ya jeshi la polisi.

Ila maoni yangu ni kwamba IGP Mangu sasa afikirie kubadili sare za polisi wetu na angeanza na kubadilisha sare za polisi wa kike na wavae suruali.

Polisi wa kike nao wanapovaa suruali wanakuwa wapo wanajiamini na wanaweza kufanya kazi zao kwa kujiamini zaidi na kusaidiana na wenzao wa kiume pale wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali.

Hio pia ni moja ya kinga dhidi ya ajali kazini na usalama wao kiujumla wanapokuwa wamebeba visaidia kazi nilivyovitaja hasa "spraying powder".

Haipendezei sana kuona vijana wako wamebeba mabegi migongoni katika kukabiliana na changamoto wakiwa kazini.

Katika kubeba begi inaweza kuwafanya polisi kuwa na wakati mgumu hasa wa kufanya "restraining" kwa mhalifu kwamba mhalifu anaweza kutumia begi hilo kumziba pumzi askari.

Nafahamu kwamba mpaka sasa ni askari wa FFU pekee ndio wenye kuvaa combat gear pekee lakini hii ingekuwa ni sare kwa jeshi zima la polisi.,

Unachotakiwa kufanya ni kutafuta wazabuni ambao watakuletea sampuli ya sare mbalimbali ambazo baadae utachagua ile inayofaa yenye ubora na unafuu.
 
Kweli kabisa wa kike watupie na vikuku miguuni wa kiume watupie modo za kubana ili twende na wakati
 
Mbona wapo WP wanavaa surubale?

Dah" sasa mkuu surubale haijakaa kimkakati zaidi.

Unawaona hao wadada hapo mbele?

rwanda-1.jpg


rwanda-national-police.jpg

Huyu polisi wa kike anakuwa anajiamini anapokwenda kutembelea wananchi ili kujua matatizo na shida zao mahali popote pale.

1455220382DSC_0259.jpg

Polisi wa kike wa Rwanda wakiwa na sare za polisi ambazo ni nzuri kimbinu na kikazi.
 
Pia na vifaa vya mawasiliano kama redio za masafaa wawe nao wote na watembee na virungu.Unakuta ajali imetokea au tatizo ananza kupiga simu badala ya kutumia redio za masafa.
 
Back
Top Bottom