Ushauri: Hewa safi ni kinga na tiba, usizibe pua na chochote!

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
1,494
1,874
Kwa utafiti wangu mdogo, barakoa zinazuia upumuaji mzuri na uingiaji mapafuni wa hewa safi ya kutosha. Kama mtu ana tatizo la kupumua, kumwambia avae barakoa ni kuzidi kumwongezea tatizo la upumuaji na kuathiri mapafu yake.

Nashauri watu wapate muda mwingi wa kukaa sehemu zenye miti mingi na kupata hewa safi ya oksijeni. Walioko mijini kama Dar es Salaam, watembelee eneo la Chuo Kikuu, Changanyikeni, Kisarawe na kwingineko kwenye kijani kibichi na hewa safi, wakapunge upepo bila barakoa.

Na tukumbuke kuwa hewa safi, hasa oksijeni huongeza kinga mwilini na kuufanya mwili uimarike kiafya. Hewa safi ni dawa, ni tiba - usiizuie kwa barakoa kuingia puani na kisha kushuka mapafuni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom