Siku hizi kila anapokwenda ni kupokea nyimbo za sifa tu na mapambio, tofauti na wakati wa kampeni watu watatema nyongo zote walizozitunza kifuani kwa miaka mitano na kumtapikia, itakuwa kazi kwake kujisafisha.
Asipoanza leo kuzoea maswali mazito mazito, magumu na vijembe kutoka kwa wapinzani wake, zitakapoanza kampeni hatajua wamepanga kuhoji maswali gani na kuishia kutoa majibu yasiyoridhisha na kwa hasira.
Imagine anafika Iringa anakuta kuna swali wanataka kujua zile 2.4t alizipeleka wapi, anafika Mbeya Sugu keshamwaga sumu ya hasara inayoletwa na ATCL kwa uamuzi wake wa kununua ndege kwa pupa.
Anakwenda Arusha anakutana na issue ya hasara ya Tanzanite pamoja na kujenga ukuta wa mabilioni, na data anapewa lazima achanganyikiwe.
Anaenda Mwanza anakuta wapinzani wamehoji kwa nini wale maaskari wa dhahabu waliachiwa pamoja na kushikwa red-handed.
Anarudi Dar anaulizwa yale makontena ya makinikia na issue ya kishika uchumba cha $300m zitalipwa lini, na issue ya nyumba za serikali zilizouzwa kiholela imefikia wapi, wakazi wa Kimara nao wanakumbushia fidia yao.
Anaenda Dodoma wanamkumbusha lini atahamia Dodoma, anafika Singida anakumbushwa matibabu ya Lissu na ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji, kama una moyo mdogo lazima umtoe mtu roho.
Anafika Mtwara anakumbushwa suala la korosho, hadi leo wakulima hatujalipwa, lazima afure na kusingizia ni njama za wapinzani wanaotumiwa na mabeberu.
Anafika Kigoma mwisho wa reli anakumbushwa ya MKIRU, Azory, Ben, na kwa nini wakazi wengi wa Kigoma wanahisiwa sio raia wa Tanzania.
Anaenda Kagera anakumbushwa rambirambi za tetemeko, yaani mambo yatakuwa mengi na muda wa kuyajibu atakuwa hana, matokeo ni hasira.
Kama hataruhusu leo mikutano watu wateme nyongo, na kuanza kuzoea kashikashi hizi, ninavyomjua wakati wa kampeni ataona kama ni personal attack lazima wengi wataishia jela kwa mashtaka ya uchochezi na kumtukana rais kumbe ni masuala ya kawaida sana kwenye kampeni.