Ushauri(Gharama za Ujenzi nyumba ya kawaida ya vyumba 3)

Wengine ni wezxi na wengine wanakop[a na wengine ni wafanya biashara, wengine wamejiajiri na hawategemei hii mishahara ya kinyonyaji...... wewe ukilipwa na slave master wako 1M yeye kwa wiki anaingiza 7M kwa vibiashara vyake vidogodogo...... KUJIAJIRI!!!:fish2:
 
Wengine ni wezxi na wengine wanakop[a na wengine ni wafanya biashara, wengine wamejiajiri na hawategemei hii mishahara ya kinyonyaji...... wewe ukilipwa na slave master wako 1M yeye kwa wiki anaingiza 7M kwa vibiashara vyake vidogodogo...... KUJIAJIRI!!!:fish2:
mmmhhhh
 
Kwa kukisia: nyumba iliyokamilika (Fully finished house) kwa viwango unavyotaka kwa Dar es Salaam, itagharimu Tsh. 60 million hadi 100 million au zaidi kutegemeana na ukubwa wa nyumbwa yenyewe, na pia mahali gani, na kuna udongo wa aina gani kwenye plot yako. Hata hivyo, ninakushauri ufanye mambo kitaalamu na kama msomi, fanya yafuatayo:

1) Hakikisha kiwanja chako kina i) ramani ya upimaji (Cadastral plan) na ii) ramani ya topografia (Topographical map)
2) Mtafute mbunifu majengo (Architect) mweleze aina ya nyumba unayohitaji kujenga (mpe specifications)
3) Mpeleke mbunifu majengo akakione kiwanja, kisha mpe ramani ya topografia, na architech atakutengenezea michoro ya nyumba (architectural drawings for residential house)
4) Ukishapata michoro yako mtafute mkadiriaji gharama za majengo (Quantity surveyor au Building economist) akutengenezee gharama za ujenzi yaani (BOQ- Bills of quantities)

Ukishapata BOQ: hizo ndo gharama za ujenzi (mara nyingi hazitatofautiana na gharama halisi kwani, hutengenezwa kwa kufuata gharama za ujenzi za wakati huo)

Kumbuka kwamba kama unataka kuomba mkopo kutoka benki, kipengele [ 1] (i) hadi [4] ni vya lazima. na kufanya yote hayo itakugharimu kati ya sh. 1,000,000 - 2,000,000

Kumbuka pia kwamba kutotutumia wataalamu wa kukushauri maswala ya ujenzi ni ghali zaidi kuliko kutumia wataalamu.

Lakini pia wakati wa kujenga, hakikisha unapata fundi mwenye utaalamu na uzoefu, na sio fundi makanjanja. Pia hakikisha unasimamia au unaweka mtu unayemwamini sana kusimamia hasa materials na ununuzi wa materials kwa kuwa mafundi wengi ni wezi wa cement wakati wa kujenga.

Kwa ujumla gharama pamoja na masuala ya utaalamu; pia kuna factors zingine za kuzingatia, kwa mfano kama plot iko eneo lenye udongo wa mfinyanzi hapa DSM (Maeneo ya Mbezi, Kimara, Makongo) yenye udongo wa mfinyanzi, unahitaji kuwa na reinforcement kwenye msingi. Na maeneo kama ya Ukonga, Gongolamboto nk. yenye ardhi ya mchanga hauhitaji reinforcement kwenye msingi au utahitaji kidogo kulingana na aina ya mchoro wa nyumba yako.

Kwa haya machache nadhani umepata mwanga japo kidogo wa nini unachohitaji kufanya ili kuanza ujenzi wa nyumba yako.



Mkuu hapo kwenye No.1; Ni akina nani wanafanya hii shughuli sababu mimi nina kiwanja changu ila kina slope kwa kwenda chini, sasa nikipata hawa watu information zao zitanisaidia sana kutimiza ndogo yangu ya muda mrefu. Msaada wako mkuu ahsante.

NB: Mkuu hiyo cadastral plan nahisi ninayo, si ndiyo ile inatolewa na ardhi? Ila kizungumkuti kinabaki kwenye Topographical map
 
Back
Top Bottom