MUTUYAMUNGU
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 1,724
- 4,045
UNAFAA KUWA MWALIMU...MAELEZO YAKO YAMEJITOSHELEZA.Kuna gari mbili wengi wanachanganya, Daihatsu Terios na kuna ingine ni Daihatsu Terios Kid!!
Terios ina engine yenye CC 1290 wakati Terios Kid ina CC 660.
Nimeitumia sana Daihatsu Terios, ni gari nzuri mno! Ina nguvu inapita popote pale iwe lami au rough road kufupi inafaa kwa sie wajasiriamali wa porini!!
Pia watu wanasema huwezi kwenda speed, nilikuwa nakanyaga mpaka 140 kwenye route ndefu!
Nishatoka nayo Mbeya to Arusha kupitia Dar (nilikuwa na ishu Dar nikapita hapo na kugeuza muda huo huo kuelekea Arusha) bila kuipumzisha!
Kifupi ni gari nzuri, fuel consumption yake ipo vizuri sana.
Kuhusu spare zinapatikana ila kwa maduka machache, mie nilikuwa napata gerezani kuna jamaa anaitwa Swahiba ana spare za kutosha za terios!! Na huwa haitaki spare fake, ila ukiiweka ni mkataba na unasahau!!
Staff mwenzangu nilimpeleka Lushoto na terios yangu, ilipanda kila kona kule mpaka alishangaa!!
Tuliporudi Dar akataka anunue kama ile ile! Kumbe hakuwa makini akanunia Terios Kid, alipoona haina nguvu kama yangu ndipo akaileta na kuniuliza umeifanyaje yako ina nguvu!! Nikamwambia umekosea yako ni kid na si terios 🤣🤣🤣
Aliiuza akanunua terios ya kawaida chini ya usimamizi wangu! Anaipenda kuliko chochote, fuel consumption nzuri, 4wd!! Muda wote safiii, so be careful katika hilo wakuu.
Tatizo lake haichanganyi fasta labda iwe na turbo, ukitaka kununua chukua yenye turbo ni nzuri zaidi!! Pia siyo gari yenye starehe 🤣🤣🤣