Ushauri: Dhana ya kurudisha vijana vijijini wakalime

Nkuba25

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
2,341
13,020
Serikali ya awamu ya 5 imekuwa ikiwalaumu vijana kwa kutotaka kufanya kazi. Rais John Pombe Magufuli hadi amefikia hatua ya kuwaamuru wakuu wa mikoa na wilaya wawakamate vijana wanaokaa "vijiweni/mtaani" bila kazi na kuwapeleka kwenye mashamba ya kilimo ili wakalimishwe kwa nguvu.

Nimekaa nikajiuliza, ni kweli serikali imeshindwa kuwasaidia raia/wananchi wake mpaka waamue kuwakamata kwa nguvu na kuwafanyisha umanamba kwa nguvu?

Kupitia JKT na Bank ya Kilimo (Tanzania Agricultural Development Bank), serikali imeshindwaje kweli kuandaa mpango mahususi wa kilimo kwa vijana?

Nionavyo mimi, serikali inaweza kufanya namna hii:

Kwa ujumla, Serikali ina mashamba na mapori mengi sana sehemu mbalimbali hapa nchini. Wangeweza kuyatambua hayo mapori na mashamba ili wajue ukubwa wake na aina ya mazao ambayo yanaweza kuoteshwa hapo.

Baada ya hapo JKT na wizara ya kilimo wakapewa kazi ya kuandaa mpango wa kilimo. Huo mpango ukapelekwa Benki ya Kilimo kwa ajili ya mkopo (serikali ndio mdhamini).

JKT akaanzisha makambi ya kilimo na kuajiri vijana wa mtaani (hao wanaokaa vijiweni) kwa ajili ya kuwafundishwa kilimo. Vijana wanapoenda huko wanafundishwa kilimo cha kisasa, namna ya kilimo cha umwagiliaji, madawa, mbegu na kwa ujumla namna bora ya kulima ilo zao. Kwa hiyo junakuwa na makundi tofauti yanayofundishwa kilimo cha mazao tofauti. JKT watakuwa wanalima kwa large scale ili ikiwezekana mazao yauzwe nchi za nje. Hii program inaweza kuwa ya miezi 12 ili vijana wajue vizuri kilimo cha kisasa.

Faida kwa vijana/Serikali

1. Serikali inaweza kuamua kuwalipa posho kidogo kwa mwezi kwa kuwa hawa vijana wanazalisha hayo mazao ambayo mwishoni yataenda kuuzwa. Kwa hiyo vijana watakuwa wamepata kipato.

2. Baada ya hiyo miezi 12 watalazimika kujiunga kwenye vikundi vya watu 4- 6 na kuwezeshwa kupata ardhi na mikopo kupitia bank ya kilimo na wao sasa wakaanze kulima (hapa serikali inakuwa mdhamini). Na vijana wanashauri walime zao ambalo tayari mnunuzi wa hayo mazao anakuwa ameshapatikana.

3. Vijana wataacha kukaa vijiweni kama serikali inavyosema

4. Vijana watakuwa wamepata skills za kilimo cha kisasa

Kwa kufanya hivi serikali inaweza kuongea na wadau ili waanzishe viwanda. Hapa sasa hiyo Sera ya viwanda ndio inaweza kufanya kazi. Na hao vijana wa JKT wanaweza sasa kupata soko la uhakika la bidhaa zao.

Naomba kuwasilisha.
 
Kambi za kilimo ziko nyingi sana hii nchi, mfano mzuri ni kambi ya Kilimo inayosimamiwa na Rubada iliyoko Rufiji Mkoani Pwani, Nilibahatika kukaa katika kambi ile miaka hiyo nahangaika na haya maisha.

Kilichoko kule ni aibu, siasa zinaharibu sana hii nchi.

Vijana wanachukuliwa vijijini na Dar es Salaam wanakwenda kutelekezwa kule maporini wakilishwa ugali maharage kila siku, kambi haina hata mbegu ya mchicha, ardhi wanayohubiri kila siku kuwa wanayo iko kwenye mgogoro wa kimahakama mpaka leo.

Cha ajabu kwenye ripoti zao "wakubwa" wanaandika kuwa wanatoa training za kutosha kwa vijana na wanavuta mpunga wa kutosha kutoka kwenye mabenki na taasisi za misaada, huku vijana wanaendelea kusota maporini.

Kambi zimegeuka vituo vya ngono tu maana huwezi kuwakusanya vijana wa miaka 18 mpaka 30 ukawarundika porini bila kazi, wakaacha kugegedana.

Tatizo hii nchi sio wananchi wala vijana, siasa na wajanja wanaiharibu sana hii nchi.
 
mkuu mimi uwaga najiuliza hivi tumerogwa na nani? Kama serikali ingechukua hatua za dhati katika haya unayoya zungumza.

Nchi hii kusingekuwa na vijana maskini, na chama cha mapinduzi kingetawala nchi hii milele.

Majipu yapo kila maali, kama rais akizidi kutumbu Mwishowe Atajikuta Mwenyewe, kila maali kumeoza.
 
Mkuu ni aibu sana, we acha tu.

Hii nchi vongozi wanaiharibu sana aisee, hawa wanaoitwa wakurugenzi wa idara za serikali ni watu wa hovyo sana.
Wanatafuna pesa za walipa kodi bila huruma.

Sasa ole wako ujichanganye uingie 18 zao, utakiona cha mtema kuni...
 
Kambi za kilimo ziko nyingi sana hii nchi, mfano mzuri ni kambi ya Kilimo inayosimamiwa na Rubada iliyoko Rufiji Mkoani Pwani, Nilibahatika kukaa katika kambi ile miaka hiyo nahangaika na haya maisha.

Kilichoko kule ni aibu, siasa zinaharibu sana hii nchi.

Vijana wanachukuliwa vijijini na Dar es Salaam wanakwenda kutelekezwa kule maporini wakilishwa ugali maharage kila siku, kambi haina hata mbegu ya mchicha, ardhi wanayohubiri kila siku kuwa wanayo iko kwenye mgogoro wa kimahakama mpaka leo.

Cha ajabu kwenye ripoti zao "wakubwa" wanaandika kuwa wanatoa training za kutosha kwa vijana na wanavuta mpunga wa kutosha kutoka kwenye mabenki na taasisi za misaada, huku vijana wanaendelea kusota maporini.

Kambi zimegeuka vituo vya ngono tu maana huwezi kuwakusanya vijana wa miaka 18 mpaka 30 ukawarundika porini bila kazi, wakaacha kugegedana.

Tatizo hii nchi sio wananchi wala vijana, siasa na wajanja wanaiharibu sana hii nchi.
Mkuu Asigwa

Kutoka kwenye post yako kuna kitu cha kujifunza hapo. Mimi sijawahi kufahamu kwamba kuna makambi ya vijana kwa ajili ya kulima.

Kutoka kwenye post yako inaonyesha kabisa hii Serikali haina dhamira ya dhati ya kusaidi vijana au taifa kuondokana na ili janga la umasikini.

Pia hii inaonyesha kwa kiasi kikubwa kwamba JPM hana mkakati juu ya kuwakwamua vijana na vilevile hajui hata afanye nini.
 
Mkuu hizi kambi zilikuwepo hata kabla Magufuli hajawa Rais.

Labda kama anakuja na mkakati mwingine wa kuzimulika hizi kambi kwa upya, lakini kama ni ngonjera zile zile na za kutumia wakurugenzi wale wale hakutakuwa na jipya hapo.

Watakuwa wanawapotezea tu vijana muda wao, bora uwaache wakae vijiweni wacheze kamali kuliko kuwarundika porini huko wakaambukizane ukimwi.

Kambi moja inachukua vijana takribani 200, na iko katika kati ya pori, vijana kuanzia asubuhi mpaka jioni hawana kazi zaidi ya kucheza karata na kupiga story tu, na bahati mbaya sana unemiksi watoto wa kike na wa kiume.

Unategemea nini.

Hizo kambi za kilimo kifupi ni madanguro tu, hamna kitu hapo.

Labda kama uongozi wote tangu huko juu utafumuliwa na kupangwa upya.
 
Back
Top Bottom