Ushauri: Dada zetu wa kilokole legezeni masharti muolewe

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
15,705
14,600
Samahani sipo hapa kusema dini ya mtu lakini hili limekuwa tatizo la muda na karne kwa karne kwa karne inatosha jamani.

Vijana wangu wanalalamika sana kuwa wasichana wa kilokole hawashikiki, wanasema kuwa ukimtongoza msichana wa kilokole anakuwa na masharti ya fuatayo:

1. Sitaki mahusiano ya boyfriend na girlfriend ni dhambi kama unanipenda nioe.

2. Lazima wewe ulienipenda uwe umeokoka kama mimi (msichana) last sivyo siwezi kukubali mana wewe ni wa mataifa (mdhambi)

3. Akikukubali lazima muende kwa mchungaji kwanza mchungaji akuone akikukubali ndio akuoe kwa masharti ya kanisa.

4. Hakuna kutembea (kuzini) pamoja mpaka ndoa la sivyo kwaheri nenda kwa wanawake wa kidunia.

Wanawake wengi wa kilokole wanachukua muda mrefu kuolewa kwasababu wanamsubiria Mungu, this is confusing kwakweli.

Najua Yesu aliagiza watoto wa nyumbani kwake waolewe na vijana wa nyumbani kwake at the same time Yesu huyu huyu alikaa na wenye dhambi akina sisi.

Sasa kumtenga binadamu mwenzio kisa hajaokoka naona kama sio sawa,
wengine mnasema mtasubiri mpaka wakati wa bwana, kumbukeni Biblia imesema siku za kuishi wanadamu ni miaka 70 mpaka 80.

Wengine mnasema Sarah mke wa Ibrahim alizaa akiwa na miaka 90,
wewe utakaa duniani miaka 90 uje uzae ulee saa ngapi kwa nguvu gani?
Zama za kuishi miaka 1000 ni za agano la kale sio jipya.

Wewe una 40 haujazaa haujalea haujasomesha hapo una miaka 20 mbele ya nguvu za kutafuta maisha ya kulea watoto na kusomesha kabla Mungu hajakuchukua.

Mimi ninadhani kwamba haya mambo ya kubana na kuweka masharti imeshakuwa too much mengine mnamsingiziaga Mungu tu, kwani Mungu kakwambia umsubiri au kakwambia zaa ukaongezeke ukaijaze dunia?

Wadada walokole wa kwa Yesu tunaomba muwe realistic ukimpata mwanaume mwenye msimamo na maisha yupo focus na maisha hata kama hajaokoka mkubalie.

Waswahili wanasema mwanaume humsikiliza sana mwanamke aliempenda huwezi jua katika hubiri hubiri yako na matendo mema yako ukambadilisha mpenzi/ mumeo japo sio wote wanabadilika ila Mungu anatoaga neema mwisho wa siku mbeleni wanabadilikaga.

Fanyeni Uinjilisti kwa akili zaidi na kwa ujanja zaidi kukaa miaka 40-50 kanisani sio nzuri jamaa hata Mungu anawashangaa.

Mungu alimpa kila binaadamu chini ya jua akili, tumieni akili vizuri mkikomboa wakati mana siku zimeisha Yesu anakaribia kurudi.

Ni hayo tu jamani wale warembo waliookoka legezeni sheria /masharti muolewe.


 
Mtu kuokoka ni lazima kwanza awe very stressed! Yaani ukimkuta huko ni sawa na gari ulolikuta garage baada ya kutumika sana!! Sasa hao wadada huwa and hawataki tena kurudi kule walikotoka ndo maana wanakuwa na mashart kuliko mkopo wa benki
Jaman sio hivyo watu wakiokoka wanabadilishwa wanakuwa viumbe vipya
Bora ukawowe huko kwa viumbe vipya kuliko duniani
 
Kama hujaokoka na ukao mwanamke mlokole ujue utateseka........
True Story
Sio kweli jaman
Kwani mwanamke anakufanya nini?!
Maana Kwanzaa mwaminifu asilimia 100 hachepuki anakuombea name kufunga kwa ajili yako

Yani mwanaume akioa mlokole anaweza mchepukia hapo hapo puani mwake mkewe akajua akamwambia Mungu akubariki Mungu anakupenda sana
 
Kwa Mujibu wa maandiko "Apataye Mke apata kitu chema naye amejipatia kibali kwa Mungu"

Azinie na mwanamke hana akili .....uwezekano wa kulegeza masharti haupo. Ukimpenda mwanamke wa Kilokole aliyekolea neno usitegemee lolote zaidi ya Ndoa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom