Ushauri: Dada karudi kwa wazazi ni mwaka sasa

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,030
Habari zenu wakuu,

Dada yangu aliolewa mwaka jana na mwenzake na kukawa na sherehe, viapo, n.k. Baada ya ndoa ikapita miezi kama mitatu hivi akarudi kwa wazazi akiwa na mimba akakaa hapo akajifungua fresh mtoto wa kike.

Cha ajabu anaendelea kukaa hapo kwa wazazi hadi sasa, kuna kipindi niliskia aliambiwa aende kwa mume wake ila asubuhi akarudi nikabaki na mshangao. Mume wake hana tatizo kabisa na anapigania sana ndoa irudi, ana kazi shirika binafsi na analipwa fresh tu.

Najua dada yangu ana kiburi fulani hivi ila nashindwa kabisa kujua niwe na msaada upi aende kwa mume wake. Mimi nilishahama hapo kwa wazazi ila naendaga sana kusalimia

Naombeni ushauri please, maumivu nayoyapata pamoja na wazazi ni makali maana hata huyo mtoto sio wetu bora hata mimi mwanaume ningepeeleka mtoto hapo nyumbani
 
Mtoto mdogo roho inakuuma dada akikaa home na mtoto wake, ukikua nyie ndo wale mnaua ndugu zenu kisa vitu vya kipumbavu...
Huyo dada yako anakuombaga maziwa ya mtoto..
Acha roho ndogo kuwa tu casual wala hili sio swala la kumuumiza mwanaume , hili muachie mama yako wala stori zake hazikuhusu.
 
Alikaa ndoani miezi mitatu tu akarudi, hakuja kwa ajili ya kujifungua bali ndoa tayari ilishavunjika.

Hakuona vema kuyasema hayo kwa vile ilikuwa mapema sana, kama shemeji hana tatizo fanya uhamie kwake mlamu.

Huenda dudu jeusi linamtisha, kama hakuwa na uzoefu kabla!
 
Huwezi jua anashida gani, kaa nae wewe na wazazi wako mjadiliane mjue nini tatizo
 
Asante JF Mungu akulinde JF na uzidi barikiee JF. Kila aina ya tukio utalisoma JF.

Mtoa mada na wewe rudi kwa wazazi iwe ngoma droo.
 
Back
Top Bottom