Ushauri: CHADEMA toeni tamko la kuwataka wabunge na madiwani wanaotaka kujiunga CHADEMA wasubiri mwaka 2020

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Nawashauri viongozi wa CHADEMA kujitofautosha na wale wa CCM kwa kuwashauri wabunge na madiwani wanaotaka kuhamia CHADEMA(kama wapo wenye nia hiyo) wasubiri mpaka mwaka wa 2020 ili kuokoa fedha zinazotumika kugharamia chaguzi ndogo.

Vile vile eleweni watu wa chama fulani huenda wameona biashara waliokuwa wanaifanya ni ya kijinga na sasa wanataka na nyinyi muonekane kama wao mbele ya umma na zaidi mshindwe kukosoa wanachokifanya kwani na nyinyi mtakuwa mnafanya kosa lilelile hivyo wanaweza kuwashawishi watu wao wahamie CHADEMA ili ku-balance equation (waliosoma Chemistry wanaeleea).

Jiulizeni ni nani wa kujiuzulu udiwani au ubunge alafu aje abaki raiwa wa kawaida tu huku akipoteza mishahara na kupunguza mafao yake?

Kuna uwezekano pia wa baadhi kuhamia CHADEMA leo hii alafu ikifika 2020 wakatangaza kujiuzulu huku wakitoa tuhuma mbalimbali kwa chama na viongozi kwa lengo la kutaka kukidhoofisha chama wakati wa uchaguzi.

Tafadhali tusifurahie wala kuendekeza haya mambo bali tuyakemee.
 
Niliweka uzi humu asubuhi nadhani bado upo , Kuna mlundikano wa barua za maombi ya kujiunga na chadema kutoka kwa wanaccm
 
Hili jambo mimi siliafiki kwani linaweza kuja kutugharimu mwaka 2020.Tuwe makini sana.
kwa vile viongozi wa Chadema wako humu na wewe ni miongoni mwa wanajf wanaoheshimiwa sana Chadema Makao Makuu kwa michango yako , basi bila shaka ushauri wako umechukuliwa .
 
Huyu jamaa salary slip ni mchagga? Kama sio, ushauri wame hatutaufanyia kazi
 
Nawashauri viongozi wa CHADEMA kujitofautosha na wale wa CCM kwa kuwashauri wabunge na madiwani wanaotaka kuhamia CHADEMA(kama wapo wenye nia hiyo) wasubiri mpaka mwaka wa 2020 ili kuokoa fedha zinazotumika kugharamia chaguzi ndogo.

Vile vile eleweni watu wa chama fulani huenda wameona biashara waliokuwa wanaifanya ni ya kijinga na sasa wanataka na nyinyi muonekane kama wao mbele ya umma na zaidi mshindwe kukosoa wanachokifanya kwani na nyinyi mtakuwa mnafanya kosa lilelile hivyo wanaweza kuwashawishi watu wao wahamie CHADEMA ili ku-balance equation (waliosoma Chemistry wanaeleea).

Jiulizeni ni nani wa kujiuzulu udiwani au ubunge alafu aje abaki raiwa wa kawaida tu huku akipoteza mishahara na kupunguza mafao yake?

Kuna uwezekano pia wa baadhi kuhamia CHADEMA leo hii alafu ikifika 2020 wakatangaza kujiuzulu huku wakitoa tuhuma mbalimbali kwa chama na viongozi kwa lengo la kutaka kukidhoofisha chama wakati wa uchaguzi.

Tafadhali tusifurahie wala kuendekeza haya mambo bali tuyakemee.
Hahahaa....... Mlibahatika kumchuuza Nyalandu tu!
 
kwa vile viongozi wa Chadema wako humu na wewe ni miongoni mwa wanajf wanaoheshimiwa sana Chadema Makao Makuu kwa michango yako , basi bila shaka ushauri wako umechukuliwa .
Kuongoza Chadema ni utume na kujitwisha Msalaba by Freeman Mbowe!
 
Back
Top Bottom