Uchaguzi 2020 Ushauri: CHADEMA msitumie/mpunguze matumizi ya usafiri wa helicopter kwenye kampeni za Urais

Louis II

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
3,030
4,645
Salam Wakuu!

Ninafahamu mna Jukumu kubwa sana mbele yenu kama chama kinachotafuta nafasi ya kuingia ikulu kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru. Mnaenda kupambana na Raisi Magufuli ambaye kwa hakika ana wafuasi wengi sana na kwa hakika wanakubali utendaji kazi wake.

Hivyo, kama heading inavyoeleza ninapenda kuwashauri CHADEMA kupunguza kama si kuacha matumizi ya Helicopter katika kampeni za uchaguzo wa mwaka huu kama tulivyowazoea huko nyuma.

Nayasema haya nikifahamu kuwa Nafasi yenu pekee ya kumwaga Sera zenu itakuwa finyu sana hasa kwenye hizi media zetu zinazoegemea upande wa chama tawala CCM.

Acheni kutumia helicopter badala yake mtumie magari ili iwe rahisi kuwafikia wananchi wengi hasa wa maeneo ya vijijini. Habari za kutumia helicopter zinasababisha mubague maeneo ya kufika/kutokufika.

Otherwise, mimi sio mwandishi mzuri sana so nadhani ujumbe umefika.
 
Sio wapunguze. Suala ni kwamba wasitumie kabisa helicopters kwenye kampeni zao za mwaka huu.


CCM wako tayari kufanya lolote dhidi ya ushindi wa Chadema mwaka huu na Helcopters ndo usafiri hatari zaidi kwa wanasiasa
 
Sio wapunguze. Suala ni kwamba wasitumie kabisa helicopters kwenye kampeni zao za mwaka huu.


CCM wako kufanya lolote dhidi ya ushindi wa Chadema mwaka huu na Helcopters ndo usafiri hatari zaidi kwa wanasiasa
Umenena vyema.
 
Nakumbuka helikopta walikuwa wanauwezo kufanya mikutano mingi. Mikutano mi3 mpaka Minne mikoa tofauti.
Ila kiukweli hiyo mikutano haikuwa na tija sana kwa chama. Maana yake ni kwamba kuna maeneo yalikuwa hayafikiwi na kuona kama yanatengwa na chama.
 
Mh hivi hamjui Tundu Lissu anaumwa, hiyo mizunguko ya Gari hatoweza kumaliza kampeni, Hali yake bado c nzuri na zoezi la kampeni Ni very demanding
 
Umesikika vema Mkuu. Ni ushauri kuntu sana. Pia ni kwa sababu za kiusalama. "Tembo hakawii kulitia maji" huko hewani.
 
Chadema wamekuwa na Mpango wa kutumia chopa kwenye muda wa kampeni uliobakia. Well and good! Ila namshauri mgombea urais wao yeye atumie usafiri wa chini kwani kwake zimeonyesha mafanikio makubwa zaidi kwa kuweza kuwafikia wapiga Kura wengi zaidi kupitia msafara wake.
Chopa amwachie Mzee WA Anya Mbowe na Kama ACT watawajoin BM anaweza tumia pia
 
Back
Top Bottom