Ushauri: Chadema ianzishe mfuko wa kulinda kura

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,874
310
Ikiwi idadi kamili ya wabunge wa Chadema bado kukamilika, lakini kwa hesabu cha chap-chap na kutokana na mishahara ya wabunge, Chadema itategemea kutengeneza around 2mil Tsh per day!

Ingekuwa busara na wananchi wangefurahi kuona kama sehemu ya pesa hii inatumika katika kuanzisha mfuko wa kulinda kura. Kusudi kuu laweza kuwa kuhakikisha Chadema inapata mwakilishi huru mmoja katika kila kituo cha kupiga kura ifikapo mwaka 2015!
Hii itasaidia katika kuhakiki idadi ya kura za ubunge na urais, na kwa asilimia kubwa kuzuia uchakachuaji!

Nadhani wakianza huu mchakato wenyewe, watajenga imani kubwa kwa wananchi, na hata kuwa rahisi huko mbeleni kupata michango kutoka kwetu na hata mashirika ya nje!
 
Asante kwa hilo. Mimi kwa nyongeza tu nadhani mfuko huo ungeweza kuwa mpana zaidi ya kulinda kura. Ungeweza kuwa mfuko pia wa kukuza mtandao wa chama nchini ili yafunguliwe matawi nchi nzima.
 
Asante kwa hilo. Mimi kwa nyongeza tu nadhani mfuko huo ungeweza kuwa mpana zaidi ya kulinda kura. Ungeweza kuwa mfuko pia wa kukuza mtandao wa chama nchini ili yafunguliwe matawi nchi nzima.

kufungua matawi nchi nzima ni la lazima. Nisingedhani kama ni jambo la kuwashauri. Maana wao kama chama cha siasi hili lingekuwa juu kwenye agenda yao.
 
Back
Top Bottom