USHAURI: CHADEMA,CCM,CUF tumieni helkopta zenu sasa kuokoa maisha ya raia

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
23,914
23,077
Hali ni mbaya sana katika maeneo mengi nchini ambayo mvua inanyesha kwa sasa. Kwa maeneo ya Dar-es-salaam Kigogo, Jangwani, Mkwajuni hali inatisha kwa mujibu vituo vya redio Dar. Maisha ya raia yako hatarini.

Ushauri wangu, vyama vya siasa ambavyo vilitumia helkopta kufanya kampeni katika chaguzi zilizopita(CHADEMA,CCM,CUF) , zitumie helkopta hizo sasa kuokoa maisha ya raia. Helkopta hizo sidhani ni kama ni kwa ajiri ya kampeni tu wakati raia ambao wanawapigia kura wako katika hatari ya kupoteza maisha. Raia hatutawelewa kama mtashindwa kuchukua hatua katika hili.
 
Ulichosema ni kweli kabisa. leo inabidi ijulikane kama hizo helikopta ni kwaajili ya kuwafikia watu, inabidi pita zirumike kuokoa maisha ya watu haohao
 
Ndiyo ni nyepesi kwa sababu imekaa kiumbea zaidi. Helkopta za uokozi si lazima tutegemee za CCM, CUF, CHADEMA ambazo tunajua kabisa kuwa wanakodi. Helkopta zetu za umma, ambazo serikali inazimiliki kwa niaba yetu zipo, Jeshi la Polisi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, bila shaka na vifaa vingine kutoka kwa jeshi la wokovu (huwa nalisikia tu hili lakini lipo).

Tulipaswa kwanza kuanza kuitaka serikali i-respond haraka kwa kutumia rasilimali zetu hizo, kabla hatujawaomba wadau wengine kama hao tajwa na wengine wengi wenye helkopta zao binafsi na vifaa vingine vya namna hiyo vinavyoweza kusaidia uokoaji.
 
Kwa mtazamo wangu kuihuisha CCM kuokoa maisha ya watanzania ni kutwanga maji kwenye kinu! Tangu lini CCM ikathamini maisha ya wa-TZ? Ikifanya hivyo basi kuna sababu. Nachoweza kukiunga mkono ni kama chama mbadala wa CCM kitaweza kufanya hilo - basi itakuwa jambo jema sana. Na kama hakiwezi, basi kijipange usoni kiwe na budget ya majanga kama haya!
 
1:hamna chama kinachomiliki helkopta.huwa wanazikodi kutoka South Africa na maeneo mengine kwa ajili ya kampeni.
2:si kila helkopta inaweza kutumika kwa ajili ya uokoaji.
 
Ndiyo ni nyepesi kwa sababu imekaa kiumbea zaidi. Helkopta za uokozi si lazima tutegemee za CCM, CUF, CHADEMA ambazo tunajua kabisa kuwa wanakodi. Helkopta zetu za umma, ambazo serikali inazimiliki kwa niaba yetu zipo, Jeshi la Polisi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, bila shaka na vifaa vingine kutoka kwa jeshi la wokovu (huwa nalisikia tu hili lakini lipo). Tulipaswa kwanza kuanza kuitaka serikali i-respond haraka kwa kutumia rasilimali zetu hizo, kabla hatujawaomba wadau wengine kama hao tajwa na wengine wengi wenye helkopta zao binafsi na vifaa vingine vya namna hiyo vinavyoweza kusaidia uokoaji.

Mkuu hili ni suala la dharura, hivyo sidhani kama huu ni muda wa kufanya hicho unachotaka kifanyike. Kinachotakiwa njia yoyote ambayo ni ya haraka kuokoa maisha ya raia inatakiwa kutumika.

Hivi unajua maana ya neno Umbea?
 
Mkuu 21dec2012

1:hamna chama kinachomiliki helkopta.huwa wanazikodi kutoka south africa na maeneo mengine kwa ajili ya kampeni. Hiyo inajulikana kaka, tunachosema na kuwa chama makini lazima kuweka maslahi ya wananchi wake mbele.

Na tukiongelea vyama mbadala wa ccm ambavyo (kwa mtazamo wangu) ndivyo vyenye mtazamo unaoonesha kuyajali maisha ya watanzania, palihitajika kuwa na mikakati ya kusaidia majanga yanapotokea!

Kuna vitu tunaweza kuvifanya hata tukiwa nje ya madaraka - let us be realistic bana. Kama hatuna uwezo wa kuvifanya saa hizi - it's ok, but tujipange kwa ajili ya kesho! Tukijipanga na kuwa na mfuko wa dharura kwa chama - ikitokea dharura kama hii si tunazikodisha bana?? - tukubali changamoto wakuu; isiwe kila kitu ni cha kupinga tuu!

2:si kila helkopta inaweza kutumika kwa ajili ya uokoaji. - sawa kama si kila helcopta inaweza uokoaji, lakini kama ni za kukodi na tukawa na means ya kukodi zilizo maalum kwa ajili ya kuokoa - si jambo jema hilo?
 
Hali ni mbaya sana katika maeneo mengi nchini ambayo mvua inanyesha kwa sasa. Kwa maeneo ya Dar-es-salaam Kigogo, Jangwani, Mkwajuni hali inatisha kwa mujibu vituo vya redio Dar. Maisha ya raia yako hatarini.

Ushauri wangu, vyama vya siasa ambavyo vilitumia helkopta kufanya kampeni katika chaguzi zilizopita(CHADEMA,CCM,CUF) , zitumie helkopta hizo sasa kuokoa maisha ya raia. Helkopta hizo sidhani ni kama ni kwa ajiri ya kampeni tu wakati raia ambao wanawapigia kura wako katika hatari ya kupoteza maisha. Raia hatutawelewa kama mtashindwa kuchukua hatua katika hili.

Helikopta sio baiskeli kuna procedure zake. (1) helikopta ya kuokoa ina vifaa vyake maalum na sio kila kampuni inayokodisha helikopta inavyo hivyo vifaa. Vilevile lazima uwe na mtaalam wa kutumia hivyo vifaa.

(2) Huwezi kupata kibali kutoka serikalini ya kuingiza helikopta kuokoa watu kama huna hivyo vifaa na huyo mataalam.

(3) Process ya kupata kibali cha helikopta ya kawaida inaweza kuchukua hata wiki moja.
(4) Chama cha siasa hakiwezi kupata kibali cha kuingiza helikopta nchini kufanya shughuli ambazo hazihusiani moja kwa moja na siasa.
(5) Kuna logistics za kurusha helikopta ambazo nazo zinahitaji muda. Watu wanaoweza kurusha helikopta bila hivyo vikwazo ni polisi na jeshi peke yake. Kusema vyama vya siasa vijihusishe na huu uokoaji kwa kutumia helikopta ni hoja nyepesi isiyokuwa na mshiko.

NO research No right to speak. Leteni hoja zenye tija. Kama kweli una nia ya kutaka kuwaokoa hawa watu kwanza tuambie wewe binafsi umeshafanya nini zaidi ya kudonoadonoa keyboard ya kompyuta yako?
 
Mkuu try to think beyond the material reality vyama haviusiki hapa serikali inapewa
bajeti nzuri tu kwa ajili ya
maafa tena iko ofc ya PM, hii
kazi ina wenyewe. Vyama
vikiingilia ni kuwa vinaingilia
utaratibu. We uliza Ofisi ya
Maafa inafanya nini?
 
wakifanya hivyo ujue kabisa mkipanda mnatozwa hela na ikitokea ujue kabisa tanzania tunaanza kuendelea..

ubinafsi ubinafsi ndio unatutafuna...RIP tz
 
Hali ni mbaya sana katika maeneo mengi nchini ambayo mvua inanyesha kwa sasa. Kwa maeneo ya Dar-es-salaam Kigogo, Jangwani, Mkwajuni hali inatisha kwa mujibu vituo vya redio Dar. Maisha ya raia yako hatarini.

Ushauri wangu, vyama vya siasa ambavyo vilitumia helkopta kufanya kampeni katika chaguzi zilizopita(CHADEMA,CCM,CUF) , zitumie helkopta hizo sasa kuokoa maisha ya raia. Helkopta hizo sidhani ni kama ni kwa ajiri ya kampeni tu wakati raia ambao wanawapigia kura wako katika hatari ya kupoteza maisha. Raia hatutawelewa kama mtashindwa kuchukua hatua katika hili.

Ushauri ni mzuri ukiliangalia hili suala philanthropically(humanitarian) Ila ukiliangalia kiwajibu utakuwa hapo umeiingiza CDM kimakosa. Umepatia kwenye CCM na CUF kwa kuwa ndiyo wenye serikali na wana mamlaka ya kukusanya kodi na kuitumia kwa ajili ya kulinda uhuru wa nchi na uhai wa watu wake bali hilo ni jukumu halisi la serikali ya CCM na CUF kupitia vyombo vya uokoaji kuhakikisha inalinda maisha ya wananchi kwa kutumia kodi yao.

CDM inaweza kuingia kama charity tu yaani kujitolea kwa ajili ya Public benefit kama ina uwezo bila kuwa na uhalali wa kukusanya kodi. Kwa hiyo hili ni suala la serikali 100%. The primary responsibility of any Govt is to protect its people. Tanzania hatuna structure za kuzuia maafa bali tuna structure za kiulaji za kuombea maafa ili watu wachote hela. Huu ni mzigo unaopaswa kuelekezwa squarely kwa serikali ambayo inaongozwa na CCM na CUF.
 
Back
Top Bottom