USHAURI: CHADEMA Arusha tuma ujumbe wa shukrani mnapopokea pesa za M4C | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI: CHADEMA Arusha tuma ujumbe wa shukrani mnapopokea pesa za M4C

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kashaijabutege, Mar 26, 2012.

 1. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Watanzania na watu wengine wenye mapenzi mema na nchi yetu wameguswa na mpango wa M4C (Movement for Change) uliozinduliwa na CHADEMA usiku wa tarehe 22 Machi 2012; na baadhi yao wameanza kuchangia kwa njia ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.

  Nimegundua kuwa pesa inapofika ujumbe unatumwa kwenye simu ya mtumaji kutoka kwa mtandao ulioutumia kuwa CHADEMA Arusha imepokea mchango wako. Kasoro niliyoigundua ni kuwa CHADEMA Arusha hawatumi ujumbe wowote kwa aliyewachangia ama kumshukuru au kuthibitisha kuwa nao pesa imepokelewa katika akaunti yao. Vilevile, simu zinazotumika hazipokelewi na yeyote unapojaribu kupiga ili kuhakiki.

  Ushauri:
  1. CHADEMA Arusha tengeneza ujumbe "default" wa kuwashukuru wanaowachangia.
  2. Wajue walipo na watumie risiti zao kama itakuwa rahisi kufanya hivyo.

  Swali: M4C ni kwa ajili ya Arusha tu au utafanya kazi nchi nzima?


  Kwa pamoja tunaweza.
   
 2. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  We unacheza na Chagaz nini?
   
 3. M

  Miruko Senior Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ushauri huu ungekuwa wa maana, endapo ujumbe wa M-Pesa, au Tigo-Pesa na Airtel Money ungeonyesha namba ya simu ya mtumaji, lakini kwa uzoefu wangu namba hiyo huwa haitokei bali jina tu...Je, ujumbe huo wa shukrani watautumaje kwenye jina la mchangiaji?
   
 4. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Kamanda tunashukuru kwa ushauri wako,tutalifanyia kazi,tuone jinsi ya kuboresha.M4C si kwa ajili ya Arusha pekee yake,ni mpango kamili wa kushirikisha umma katika ujenzi wa chama,na ni mpango endelevu.
   
Loading...