Ushauri: CHADEMA amkeni jamani, Slaa uko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri: CHADEMA amkeni jamani, Slaa uko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by politiki, Jan 30, 2011.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Imefika mahala chadema kuanza kuongoza mabadiliko ndani ya nchi yetu lakini chadema hawaonekani kuijua nafasi hii, nchi nzima asilimia kubwa wanapinga kuhusu swala zima la DOWANS hii ni hot cake issue lakini chadema wameshindwa kuonyesha leadership kwa kuwaonyesha wananchi nini cha kufanya? chadema kama chama makini walitakiwa kuwa on top of this issue hasa ukizingatia kuwa the whole country is against it and all they need is leadership to show the way.

  Chadema wanatakiwa kutumia power of the people ku stop DOWANS kwa kuitisha maandamano makubwa nchi nzima kupinga swala zima la malipo kwa DOWANS na kuwaeleza wananchi ukweli kuhusu DOWANS, madhara na ubaya dhidi ya nchi yetu. Kitakachotokea kwenye maandamano hayo kwa maana ya mwitikio na hasa ukizingatia asilimia kubwa ya wananchi wanapinga swala hili, ukichanganya na mambo yanayotokea Tunisia na Misri, It is very likely kwa CCM ku drop off the whole ridiculous deal kwa sababu moja tu nayo ni kuogopa/kuofia power of the people na si vinginevyo. kwenda kwenye media tu kila siku kupinga DOWANS hakusaidii kama ambavyo imeonyesha so far imefika mahala pa kuonyesha vitendo nayo ni kutumia People's power ku stop DOWANS.

  Mnashindwa nini hasa ukizingatia mko kwenye upande wa wananchi na mnaungwa mkono na nchi nzima kwenye hili??? Mnasubiri nini kitokee muamke usingizini jamani??

  Naomba majibu.
   
 2. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Chadema mko wapi? Moto mlioanza nao unaanza kuzima, Dr huu ndio wakati wa kupanda. Suala la DOWANS linahitaji mwongozo wako tuambie tufanya nini? Nini Msimamo wa CHADEMA! What next? CHADEMA amkeni WAKATI UNAOFAA NDIO SASA!
   
 3. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Habari ndio hiyo. Dr. Tafadhali ongaza campaign ya nchi nzima
   
 4. S

  Sinamatata Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHADEMA ni chama makini. Si kwamba hawalijui hilo, badi wanalipangia mikakati, kwani wanajua jinsi serikali ya CCM wanavyojipanga kuendeleza ubabe wa kumwaga damu za watanzania. Bado watanzania wako kwenye maobolezo ya msiba wa Arusha.
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Beneficiry wa Dowans ni Rostam Aziz.

  Rais wa serikali ya CCM,Mawaziri wake na Makada wa CCM ni watumwa wa Rostam, wanasubiri alipwe fedha za Dowans ili nao wafaidi makombo mezani pa bwana wao.

  Kuwazuia mbwa wenye njaa kali na utii mkuu mbele ya Bwana wao kunahitaji mkakati.

  Klele zote za akina Ngeleja ni kutaka kufaidi makombo Mezani pa Rostam Kam vile kwao Ni Antactica na Rostam Aziz ndo Mtanzania Asilia.

  HERI KUWA MBWA MWITU HURU MIKUMI KULIKO KUWA MWANACHAMA NA KADA WA CCM UTUMWANI
   
 6. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kwa nini unategemea Chadema kikuletee mabadiliko? Bado hujayaona yaliyotokea huko Tunisia na yanayoendelea kwa sasa huko Misri? Huko watu hawategemei vyama vya siasa kudai haki au kutetea haki zao. The recent trend may indicate that political parties are becoming useless. Hakuna mwanasiasa wala chama chochote cha siasa kilichoanzisha mapinduzi ya Tunisia na yanayoendelea huko Misri. Ni watu wenyewe ndio waliomua. They had enough and wanted changes and went on the street to fight for their rights without involving any political parties or politicians.

  Any changes in Tanzania will come from the people themselves including you; not political parties or politicians. Across the world people are increasingly becoming fed up with representative democracy where sovereignty is exercised by few people. Look like we're heading back to the classical democracy. Tunisia and Egypt are just the earliest examples.
   
 7. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2011
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sio lazima mabadiliko yaje kwa kuingia mitaani na kuimba tunataka hayo mabadiliko, pamoja na kwamba huu ndio muda wa Chadema kuleta hayo mabadiliko inatakiwa tuelewe kwamba inahitaji mikakati na "timing" muafaka kufanya hivyo vinginevyo inaweza kuleta madhara zaidi kuliko mabadiliko.

  Mimi naamini Chadema wapo na wanayaona haya yanayotokea, tukiwa kama wanachama waaminifu tuwasubiri watatuambia ni wakati gani muafaka wa kufanya nini. Kwa haraka naweza kuona move ya UV-CCM kama mbinu mpya ya CCM kuchanganya vijana haswa wasomi, nimesikia kwa gazeti leo asubuhi ati UV-CCM wanataka kuandamana tena kushirikisha vijana wa vyuo kulazimisha bodi ya mikopo ifutwe.

  Msidanganyike, tangu lini tumbili wakaandamana kutaka nyani wafukuzwe porini? Haitowezekana kamwe, hii ni mbinu mpya na kikubwa wanachotaka ni kuwachota vijana wasomi wa nchi hii baada ya kuona Chadema imeshika hatamu kwa vijana hao. Tuelewe kwamba CCM watahangaika sana wakati huu, tuwe makini kuwasoma zaidi ndio tujue cha kufanya wakati wakiendelea kuhangaika maana hofu za mambo kama ya Tunisia, Misri na kwingineko zinawapa taabu sana pia.

  Wananchi wakishaamua mambo yatakuwa magumu sana kwao, kwahiyo kikubwa watachojaribu kufanya kwa sasa ni kuhakikisha makundi ya watu hayawezi kuwa mobilized kufanya mambo makubwa na kwa Tanzania ya sasa hawataweza maana wamepoteza muda wao kula kuliko ku-control nchi.

  Things have already gone out of control, it's just time to tell when to kick them off the power..!
   
 8. birungi

  birungi JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  sio chadema tu,
  hata wana ccm hili wanaliona na linawauma sana kuhusu dowans.
  kama ni kuandamana kushinikiza serikali basi yawe maandamano ya wananchi wa vyama tofauti.tukisema chadema wawe viongozi wa haya maandamano doh....chama kitapauka kwa purukushani za polisi.
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Ulikuwa unamaanisha wanachama waaminifu wa Chadema? Kumbuka kuna wengine ni wafuasi na sio wanachama. Wengine ni wanachama lakini sio waaminifu. Wengine ni wanachama au wafuasi wa vyama vingine. Tanzania ni nchi ya mfumo wa vyama vingi. Pia wapo ambao ni neutral. Wengine wengi wala hawana time na siasa. Kwa hiyo sio vizuri kugeneralise mambo namna hivyo.

  Ulikuwa unamaanisha wanachama waaminifu wa Chadema? Nafikiri ni vizuri kuongelea haya masuala kitaifa zaidi kuliko kichama. Kumbuka kuna wengine ni wafuasi na sio wanachama wa Chadema. Wengine ni wanachama wa Chadema lakini sio waaminifu. Wengine ni wanachama au wafuasi wa vyama vingine. Tanzania ni nchi ya mfumo wa vyama vingi. Pia wapo ambao ni neutral na wengine wapo kitaifa zaidi. Wengine wengi wala hawana time na siasa. Kwa hiyo sio vizuri kugeneralise mambo namna hivyo.

  Nakubali sio lazima mabadiliko yaje kwa kuingia mitaani na kuimba tunataka hayo mabadiliko. Lakini wakati mwingine kunakuwa hakuna njia nyingine zaidi ya kuingia mtaani. By they way ni haki ya kila Mtanzania kuingia mtaani kupinga jambo asilopndezwa nalo. Ni haki ya kikatiba. CUF wanaandamana Jumatano kupinga malipo ya Dowans. Kwa hiyo ukiwa kama mwanachama mwaminifu wa Chadema hautaunga mkono hayo maandamamo?

  Moja ya matatizo yanayotukabili kuwa tunapenda kuaadress mambo kichama, badala ya kitaifa. Kwenye maandamno, nk watu wanabeba bendera za chama badala ya bendera ya taifa. hatuna ile kitu inaitwa utaifa. Matokeo yake tunajikuta tumejigawa. I am sure kuna wanachama na wafuasi wengi tuu wa CCM hawapendezwi, kwa mfano na issue ya Dowans. Lakini kama ukiandaa maandamano ya CUF kupinga Dowans kulipwa sidhani kama kama watakuja, simply because ni maandamano ya CUF. Kwa kweli inabidi kujifunza kuandaa mambo kitaifa. Hii itasaidia kutunganisha badala ya kutugawa kiitikadi.

  We need to take positive things coming from the Tunisia and Egypt.
   
 10. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  We need an Ignation saomewhere! and that has to be CHADEMA
   
 11. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  CUF wao wanafanya maandamano tarehe 3/2011 kupinga malipo ya Dowans hivyo CDM could join
   
 12. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  I agree we need an ignation somewhere. But must not necessarily be Chadema. Ignation should come from the people themselves regardless of whether thy support chadema or not
   
 13. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  We will see if they join. Instead utasikia Chadema nao wameandaa maandamano yao next week.
   
 14. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2011
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  EMT na BIRUNGI nimewapata vyema sana, kimsingi ushauri wangu ni kwamba yote yanawezekana. Mimi nilimjibu mwanachama wa Chadema ambaye recently aliwataka viongozi wa Chadema wawashe moto, hata hivyo hakuna jambo zuri kama pale wananchi wote bila kuangalia tofauti za itikadi zao kuamua kwa vitendo kwamba wanataka mabadiliko...HAWATOZUILIKA. Hata hivyo kwa Tanzania bado munkari wetu haujawa na moto wa kutosha, saaaana naona kama Chadema wanasaidia kuchochea huo moto ushike kasi na ndio maana wakati mwingine tunafanya kuwasikiliza ili moto wetu uwe kwenye mwelekeo mmoja.
   
 15. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2011
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hili linahitaji uelewa wa kina kujua kwanini, tujue kwamba watawala weshawagawanya hawa wapinzani kwahiyo wanalazimika ku-operate kivyao wakati fulani fulani. La msingi hapa tuwe makini kwamba sisi wananchi tunataka nini kwa wakati gann, ikitokea sisi wooooote basi tukaamka na kwenda mtaani tukiwa na nia moja, tukiwa na lengo moja, na tukiwa na mwelekeo mmoja...basi naamini wala haitochukua muda kusikia mkwere amepakimbia hapo magogoni. Lakini hili litatokea kama Askari nao watakuwa wagumu kidogo, tatizo hapa wagumu wetu (wajeshi) wamepewa limbwata maana hata wakilala kwenye nyumba za bati wakiambiwa watutwange virungu wao wanatwanga tu. Wengine wamepangisha kwetu ukiwauliza wanakwambia "Arooo...tatizo hii ndio kura / kula yetu kwahiyo tunarazimika kufuata amri"
   
Loading...