amakyasya
JF-Expert Member
- Jun 26, 2013
- 3,480
- 907
Nimetoa ushauri huo kwa sababu Mrema mwenyekiti wa TLP na mbunge wa Vunjo amejitahidi sana kuitetea CCM katika mijadala mingi ndani na nje ya bunge kama fadhila yake kwa mafao ya unaibu waziri mkuu pamoja na marupurupu mengine ya serikali ya CCM. Na kwa hali iliyopo kisiasa kuna kila dalili CCM kuzidiwa spidi ambapo mwaka 2015 kitakuwa chama cha upinzani kwa hiyo msije mkamsahau mzee huyu kama atabahatika kushinda ubunge tena.