Ushauri: CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola, viweke mkakati kuaminisha umma kuwa siasa si jambo zuri,na wapinzani hawaaminiki

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,955
20,526
Pamoja na kwamba tayari mkakati umeshaanza kufanya kazi, nashauri uimarishwe. Lengo kuu iwe kuaminisha umma kwamba shughuli ya siasa si nzuri, ni ya kupoteza muda tu na inaweza kumuharibia mtu maisha.

Lengo kuu ni kuondoa kundi kubwa la watu, hasa watumishi wa umma na wafanyabiashara na wasomi kuingilia nafasi zetu za kisiasa.

Tulizoea kula kwa amani lakini kuna makundi yanaibuka kutaka kuvamia meza ambayo kila kiti kina mtu.

Unapendekeza mkakati gani utumike? Naona huu wa kuwashitaki unazoeleka,japokuwa una nguvu, vijana wanaojifanya kukosoa mitandaoni sasa wanahenya, hata wanaocheka picha zetu,

Nimefuatilia mtandaoni, wananchi waliopigia kura waliounga mkono juhudi wamejiapiza kutopanga foleni ya kupiga kura, hii ni njia nzuri inaonyesha wapinzani ni watu wa hovyo tu wasiostahili kupoteza muda kuwapigia kura. Hii ni faida kwetu kwa kuwa either watatupigia kura sisi, au wataacha kupiga kura halafu wanachama wetu watapiga,tutashinda

Pendekeza mkakati mwingine
 
Tuwe na utawala wa ki imla Kama Korea ya kaskazini,ama kama Saidia na nchi za kiislam.
Jiwe awe mfalme basi tumalizie kazi
 
Back
Top Bottom