USHAURI: Busara itumike kumsaidia kiafya msemaji wa Simba(Haji Manara).

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,115
35,129
Kuna vipande vya video vinasambaa mtandaoni vikimuonyesha msemaji wa Simba Haji Manara akiwa jukwaani uwanjani wakati Simba ikicheza(Sina uhakika kama ni kule DRC dhidi ya AS Vita Club) huku akionekana anagugumia kwa maumivu kifuani huku akishika kifua kwa upande wa kushoto, akihema kwa shida baadaye akionekana akiwa hana utulivu na kukosa amani na furaha. Baadhi ya wataalamu wa afya wanasema huenda Haji Manara alipatwa na shambulizi la moyo kutokana na msongo mkubwa wa mawazo(Over stress) au taharuki ya kupitiliza(Panic attack) kiasi cha kupelekea yote hayo. Na moja ya mapendekezo yao ni kuhakikisha Simba inampeleka kwa wataalamu wa Afya wa moyo ili kumchunguza zaidi na pia ikiwezekana kumpumzisha na mambo ya soka kwa sasa(kama sio maisha yake yote) ili mwili upate namna ya kuhimili na kurejea sawa na vile vile kuepusha kujirudia tena kwa kitu hicho cha hatari ambacho kitabia kina mtindo wa kujirudiarudia na kuhatarisha maisha ya mtu.

ANGALIZO.
Jambo hili limetwa humu kwa misingi ya Kitaalamu na kiutu, na wala sio kiushabiki. Maoni yetu yajikite hapo.
 
Hahahahaha. 5. THIS IS SIMBA.
This is mimba
FB_IMG_1547923049975.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom